Monday, May 31, 2010

BINTI AFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA JIWE

Mtoto wa kike mwenye miaka 13, Tauhida Haji Abdul-rahman, amefariki dunia hapo hapo na mwenziwe Time Burhani Haji (12) amejeruhiwa baada ya kuangukiwa na jiwe wakati wakichimba mawe huko Mkwaju Mgoro, Micheweni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi, alisema Tauhida alifariki alipokuwa anachimba mawe na wenziwe kwa ajili ya kuvunja kokoto.

Alisema, katika harakati hiyo ya kuchimba mawe, jiwekubwa lilichomoka jiwe kubwa lililomuangukia na kupoteza uhai wake ambalo pia lilimjeruhi Time.

Kamanda Bugi alisema tukio hilo lilitokea Mkwaju Mgoro, Micheweni mnamo majira ya saa 7:00 mchana.

Kamanda alisema hali ya Time ambaye amejeruhiwa amelaza katika hospitali ya Micheweni anaendelea kupata matibabu huku hali yake ikielezwa kuwa siyo mbaya sana

Alisema mabinti hao walikuliwa wakichimba mawe kwa ajili ya kuvunjwa kokoto ili kuziuza

Kamanda alitoa wito kwa wachimbaji mawe kuwa na tahadhari katika kazi h yao hiyo hasa katika kipindi cha mvua kutokana na ardhi kushibwa maji hali ambayo inasababisha ardhi hiyo kuwa laini.

Daktari dhamana wa hospitali wa Wilaya ya Micheweni, Hamad Ali Hamad, alisemabinti aliyefariki aliumia kifua na mbavu huku aliyejeruhiwa aliumia mguu na mbavu.
.
Soma Zaidi ...

WANAWAKE 21 WAJITOKEZA KUWANIA UONGOZI ZANZIBAR

Wanawake 21 wa Zanzibar wametangaza nia ya kugombea nafasi za uongozi kupitia vyama mbali mbali vya siasa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Oktoba mwaka huu.

Wanawake hao ni wale ambao wamenufaika na mradi wa kuwawezesha wanawake kijamii na kiuchumi, Zanzibar (WEZA) unaoendeshwa katika Mkoa wa Kusini Unguja na Kaskazini Pemba tokea 2008.

Wanawake 13 kati ya hao wanatoka Mkoa wa Kaskazini Pemba na wanane ni kutoka Mkoa wa Kusini Unguja.

Waratibu wa Shehia za mikoa hizo wamesema wamefurahishwa na uamuzi wa wanawake hao kutaka kugombea uongozi na kwamba hayo ni maendeleo makubwa ikizingatiwa kuwa katika chaguzi zilizopita wanawake walikuwa hawajitokezi kwa wingi kugombea.

Mratibu wa Shehia ya Tumbe Magharibi, Salma Tumu, ambaye Shehia yake imetoa wanawake watano wanaogombea, amesema jitihada za kuwawezesha wanawake wa Zanzibar kujiamini kijamii na kiuchumi zikiendelezwa lengo la kupata asilimia 50 ya wanawake katika uongozi wa kuchaguliwa litafikiwa kirahisi.

Raya Majid Salim ambaye ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Tumbe huko Pemba amesema ameamua kugombea kwa sababu anajiamini kuwa anao uwezo wa kusimamia maendeleo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo ya kijamii yanayowakabili wanawake.

“Wanawake sasa tunafahamu haki zetu katika uongozi na kilichobaki ni kuzipigania ili kuzipata na kuzitumia kwa ajili ya kuharakisha maendeleleo ya jamii nzima-wanawake, wanaume na watoto”, alisema Raya Majid Salim.

Aliyataja matatizo yanayokwamisha maendeleo ya familia na taifa huko Zanzibar ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi na viongozi kuwa ni pamoja na watoto wa kike kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo na wanaume na wanawake wasio na kipato kukosa mitaji kwa ajili ya kuendesha miraji ya kiuchumi.

Khadija Omar Kibano ambaye anagombe udiwani wadi ya Mtambwe kaskazini amewataka wanawake nchini kote kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi wa mwaka huu kama wanavyojitokeza wanaume

Mradi wa WEZA unaendeshwa kwa mashirikiano kati ya Care Tanzania, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Austria na Care Austria.
.
Soma Zaidi ...

STARS VS BRAZIL KIINGILIO 200,000. KIWANGO CHA CHINI 30,000

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) jana lilitangaza kiingilio cha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, na Brazil itakayopigwa Juni 7 huku kiwango cha juu kikiwa sh 200,000.

Mechi hiyo itakayopigwa siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kiwango cha chini kabisa ni shilingi 30,000.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, hadi kufikia jana, tiketi hizo za sh 200, 000 ambazo ni za jukwaa VIP A, zimekwisha.

Alisema, kulingana na idadi ya viti vya jukwaa hilo, tayari kiasi cha shilingi mil. 140 zimepatikana na kutaka wananchi wajitokeze kununua tiketi za maeneo mengine.

Mwakalebela alitaja viwango vya maeneo mengine ambapo VIP B ni sh 150,000; VIP C sh 100,000; Viti vya rangi ya chungwa mkabala na VIP, itakuwa sh 80,000 huku viti vya rangi ya chungwa, nyuma ya magoli itakuwa sh 50,000.

Alisema viwango hivyo vimetokana na gharama kubwa za kuileta timu hiyo, hivyo kuifanya mechi hiyo kuwa ya gharama kubwa tofauti na mechi nyingine zilizowahi kuchezwa nchini.

Katika hatua nyingine, mchezaji Ricardo Kaka hatacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Zimbabwe na ile itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam baada ya jana kuumizwa na
Felipe Mello katika mazoezi.

Habari zinasema, Kaka amepata maumivu makali yaliyomfanya kuibuke mzozo mkali kati yake na Mello na kumfanya Kaka kususa na kuondoka mazoezini. Soma Zaidi ...

Sunday, May 30, 2010

Saturday, May 29, 2010

50 CENT ALIVYOJIANDAA NA "THINGS FALL APART"

50 Cent amepoteza uzito kwa ajili ya filamu yake mpya ijulikanayo kama, "Things Fall Apart". Katika filamu hiyo, 50 Cent anaigiza sehemu kama mcheza mpira ambaye anagundulika kuwa na saratani.

Alipungua uzito toka paundi 214 hadi 160 kwa kula lishe maalumu ya vimiminika pekee (liquid diet) na kufanya mazoezi ya -treadmill- kwa saa tatu kila siku kwa muda wa wiki nane.

"Nilifunga kula." Kwa sasa amerejea katika ziara zake na anasema, "Nimeanza kula. Nitarudia hali yangu kiafya muda si mrefu!" Soma Zaidi ...

Friday, May 28, 2010

TANGAZO LA MSAADA

NDUGU ZANGU
Assalamu 'alaykum

Kijana ambae picha yake imeambataniswa ni mgojwa wa kidonda ndugu. Tayari ameshakwenda hospitali nyingi hapa Zanzibar na Tanzania Bara lakini hali inazidi kuwa mbaya. Uchunguzi wa madaktari umegundua kwamba mishipa yake ya damu imeziba na ndio maana kidonda chake hakipoi (Angalia picha iliyoambatanishwa). Ameshauriwa kwenda India.

Tayari Shs 1,000,000/= zimeshakusanywa na kuna mtu amejitolea kutoa tiketi. Yupo mwengine ambae amejitolea kumpeleka. Fedha inayohitajika ni kama dola 4,000 hivi ambazo tumeona tuwaambie wenzetu ambao watapenda kutabaruk. Hizi si taarifa za kitapeli na naamini nyote mnanielewa. Na wala email yangu haijatekwa.

Kijana ni mzaliwa wa Tumbe (1987) lakini kwa sasa yupo Jang’ombe na anapatikana wakati wewote. Harakati na kumtafutia safari zimeshaanza. Hivyo tunakuomba na wewe utuunge mkono kwa chochote utakachojaaliwa. Unaweza kunipatia mimi 0777 420247 au mlezi wake Sheikh Omar ambaye husalisha sana sala ya Adhuhuri na hudarsisha msikiti wa Mtendeni karibu na tawi la chama cha wananchi makao makuu 0774 101166 au unaweza Kumuona ustaadh Maulid, anauza duka Malindi karibu na mkahawa wa Tausi.

Naomba tuwaarifu na wengine ambao watapenda kumsaidia huyu kijana na ambao hawamo katika orodha ya ujumbe huu.
Tafadhali pia watumie ujumbe huu ndugu zetu wengine ambao wanatunia mtandao.

Sote ni ndugu. Tumsaidie huyu kijana ili nasi Allah (SW) Atusaidie.

Shukran

Said Othman
Zanzibar AIDS Commission
P.0.BOX 2820
Shangani Kelele Square


Soma Zaidi ...

WAASI WA KISOMALI WASHAMBULIA KIJIJI KENYA

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislam wa Somalia wamekishambulia kijiji kimoja kilichoko katika mpaka wa nchi hiyo na Kenya. Wakaazi saba wa kijiji hicho cha Dadajabula kilicho Kenya walijeruhiwa.

Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mashahriki huko Kenya. James Ole Serian, amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa wanahisi washambuliaji hao ni wapiganaji wa kundi la al Shaabab.

Wiki iliyopita msemaji wa al Shaabab, Ali Mohammed Rage, aliionya Kenya kutojiingiza katika mzozo wa Somalia. Serikali ya mpito nchini Somalia imekuwa katika mkakati wa kufanya mashambulio makubwa dhidi ya waasi hao wa al Shaabab ambao wanailaumu Kenya kwa kushiriki katika mkakati huo.

. Soma Zaidi ...

NEW BRAND MIWANI YA JUA


Soma Zaidi ...

HAWA NAO!!!!!!


Soma Zaidi ...

MAHARAMIA WA KISOMALI WAKIMBILIA KISIWANI PEMBA

Watu tisa wanaodaiwa maharamia waliotaka kuishambulia meli ya Namtuna katika eneo la kati kati ya kisiwa cha Unguja na Pemba wamefukuzwa na halikopta ya askari wa umoa wa Ulaya na inadaiwa maharamia hao wamekimbilia Pemba.

Askari hao waliokuwa doria katika helikopta hiyo ya umoja wa Ulaya wamesema tukio hilo limekuja siku tatu tangu kutokea kwa tukio jingine katika kisiwa cha Sheli sheli.

Kiongozi wa opereseheni wa umoja huo unaofanya doria katika pwani ya Afrika ya Mashariki amesema wamepigiwa simu kuhusiana na kuwepo kwa tukio hilo kati kati ya visiwa vya Pemba na Unguja na hivyo kutuma helikopta hiyo na hatimae kuikoa meli hiyo na maharamia hao kukimbilia Pemba.

Amesema maharamia hao wameshindwa kuwafuatilia baada ya kuingia katika eneo la Pemba kutokana na sheria haziwapi mamlaka ya kuingi katika pwani ya Tanzania.

Akizungumzia tukio hilo mwana sheria mkuu wa serikali jaji Fred Tungelema amesema wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuweka mpango wa kuliwezesha jeshi kulinda maeneo yote ikiwemo bahari kuu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa kusini Pemba Hassan Nassir amesema tukio hilo bado halijathibitishwa na kusema maharamia hao kukimbilia kisiwani humo ni uvumi.

Hivi karibuni mkurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe amesema tatizo la maharamia katika pwani ya Afrika ya Mashariki limesababisha wenye meli kupandisha gharama za usafirishaji wa mizigo.

Akizungumza katika mkutano uliojadili ushiriki wa Zanzibar katika soko la pamoja la Afrika Mashariki amesema hali hiyo inaweza kudhorotosha shughuli za bandarini na kuongezeka kwa bei za bidhaa. Soma Zaidi ...

Thursday, May 27, 2010

MAHARAMIA HATARI WATUA NCHINI

Wimbi la utekaji wa meli linaloendeshwa na maharamia wa Kisomali limechukua sura mpya baada ya kuingia katika mwambao wa visiwa vya Pemba na Unguja.

Kufuatia hali hiyo, Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini umekiri kuwapo kwa maharamia tisa, baada ya meli yao ya kivita kuwanasa watekaji hao katika mwambao wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dar es Salaam jana, Balozi wa Ufaransa nchini, Jacques Champagne de Labriolle, alisema maharamia hao walikimbilia katika mwambao wa Tanzania baada ya kunaswa na vyombo maalumu vya meli ya kivita kutoka nchini Ufaransa iliyojulikana kwa jina la Eunavfor Atalanta, iliyowasili nchini jana alfajiri.

Balozi Champagne de Labriolle alisema meli hiyo ilikuwa na wanajeshi zaidi ya 50 wa Umoja wa Ulaya (EU), ambao walikuwa wakitokea nchini Somalia kulinda na kuzuia vitendo vitakavyofanywa na maharamia katika meli zinazopeleka misaada ya chakula nchini humo.

Akizungumzia tukio hilo, nahodha wa meli hiyo, Kamanda Fontarensky Guillautie, alisema waliwanasa maharamia hao wakiwa na boti mbili, ambao waliamua kukimbilia katika boti za wavuvi kwa lengo la kujificha.

“Baada ya kuwaona maharamia hawa waliamua kukimbia hadi kwenye boti za wavuvi kwa lengo la kujichanganya ili wasikamatwe… sisi kwa mujibu wa sheria zetu hatuna ridhaa ya kukamata watu wa namna hii katika mwambao wa Tanzania,” alisema Kamanda Guillautie.

Alisema waliwanasa maharamia hao baada ya kupewa taarifa za kuwepo njama za kutekwa kwa meli iliyokuwa na mzigo, ambayo haikufahamika mara moja ilikuwa inaelekea wapi, lakini kutokana na tukio hilo ililazimika kuingia Tanzania ili kujinasua kwenye makucha ya watekaji.

Balozi Champagne de Labriolle alisema hili ni tukio la kwanza kwa maharamia wa Kisomali kuingia Tanzania, ni vyema serikali ikawatafuta na kuwachukulia hatua za kisheria, kwa vile wanatishia usalama na kuzorotesha uchumi unaochangiwa na usafiri wa baharini.

“Ni vizuri vyombo vya dola vya hapa nchini vikafanya kazi ya kuwatafuta na kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafungulia kesi mahakamani watu hawa ambao wamekuwa tishio kwa nchi zinazofanya biashara kwa kutumia Bahari ya Hindi,” alisema Balozi Champagne de Labriolle.

Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini limesema limejizatiti vya kutosha kwa ajili ya kukabiliana na tukio lolote la utekaji nyara utakaofanywa na maharamia hao.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, aliiambia Tanzania Daima jana kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola limeweka mikakati mikali ya kudhibiti hali hiyo.

“Unajua suala hili limeanza mbali mno, sasa limeanza kusogea kwenye ukanda wetu, napenda kukuhakikishia kuwa sisi polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine tumejipanga vizuri kukabiliana na hali hii,
“Unajua suala hili ni la kimataifa, hatuwezi kulikwepa, tumejipanga, kuanzia ukanda wa pwani hadi hapa Dar es Salaam ili kuona meli zote zinasafiri salama,” alisema DCI Manumba. Soma Zaidi ...

RIPOTI YA OECD JUU YA MATUMAINI YA USTAWI WA UCHUMI

Shirika la Ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo, OECD, limesema katika ripoti yake kwamba ustawi wa uchumi katika nchi za ukanda wa sarafu ya Euro utafikia asilimia 1.2 mnamo mwaka huu, tofauti na utabiri wa hapo awali.

Hata hivyo, shirika hilo limezitaka nchi za ukanda huo zikabiliane na matatizo ya bajeti yanayoweza kuzorotesha mchakato huo wa ustawi.

Katika ripoti yake iliyotoa mjini Paris leo, shirika la OECD, limeonyesha matumaini kutokana na utabiri unaoashiria kwamba pato la jumla la taifa la nchi 16 zinazotumia sarafu ya Euro litastawi kwa asilimia 1.2 mnamo mwaka huu na asilimia 1.8.mwaka ujao.

Shirika hilo limetilia maanani katika ripoti yake kwamba uchumi unaanza kustawi tena hatua kwa hatua katika nchi za ukanda wa Sarafu ya Euro kufuatia hatua za kuufufua uchumi zilizotekelezwa na nchi hizo na kutokana na kukua tena kwa biashara ya dunia.

Hali nzuri katika sekta ya fedha,pia imechangia katika ustawi huo,ingawa pamekuwapo na hali ya kuyumba yumba katika sekta ya mabenki.

Hata hivyo,shirika la OECD limetahadharisha kwamba kurejea kwa hali nzuri kunaweza kutatizwa na hatua za kujaribu kurejesha nguvu ya ushindani na kutokana na udhaifu katika nchi zisizokuwa na nguvu kubwa kiuchumi katika eneo hilo.

Katika ripoti yake ya nusu mwaka,shirika hilo limesema ingawa kustawi tena kwa uchumi wa Ujerumani,kimsingi,kumekuwa imara,ustawi huo utaanza kuwa madhubuti katika nusu ya pili, kadri mauzo ya nje yatakavyonufaika na kustawi tena kwa biashara ya dunia.

Hata hivyo,nchi za ukanda wa Euro zinatakiwa ziendelee na mageuzi.

Lakini kwa jumla,uchumi utafikia asilimia 0.1 badala ya asilimia 1.5 kama ilivyokuwa mwaka jana, na baadae utastawi kwa asilimia 0.6 katika mwaka ujao.

Na licha ya udhaifu wa muda,kimsingi ustawi ni imara, na unaashiria ukuaji madhubuti katika siku za usoni.

Ustawi nchini Ufaransa ,yaani nchi inayoshika nafasi ya pili katika nguvu za uchumi baada ya Ujerumani,barani Ulaya, uchumi utakua kwa asilimia 2 mnamo mwaka huu na katika mwa ujao.
.
Soma Zaidi ...

Wednesday, May 26, 2010

HAWAVUMI LAKINI WAMO

Soma Zaidi ...

IMANI NYENGINE BWANA!!!!

Angalia mkono wa kushoto wa kipa Soma Zaidi ...

SIKU GARI YA RAIS "JK" ILIPOGOMA


Ilikua ni siku ya jumaatatu ambapo rais alikua katika ziara za kuzindua miradi ya maji katika Mkoa wa Dar-es-salaam.
Soma Zaidi ...

WAFANYAKAZI WOTE WA ATCL WAACHISHWA KAZI

Kamati ya kudumu ya Bunge na Fedha na Uchumi iliyokutana jijini Dar Es Salaam tarehe 25 Mei 2010 imeridhia mapendekezo na ushauri wa Ofisi ya Msajili wa Hazina ya kuwaachisha kazi wafanyakazi wote wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili kuipunguzia mzigo Serikali.

Ushauri huo umetolewa na mshauri wa Msajili wa Hazina bwana Godfrey Msella na kusema, "kama ATCL haibebeki, ni bora Serikali ibwage manyanga" na hivyo kufuatiwa na tamko rasmi la Mwenyekiti wa tume hiyo ya Bunge, mhe. Abdallah Kigoda.

Hatua kama hiyo iliwahi kuchukuliwa katika shirika la Bima la Taifa (NIC) na imependekezwa kuwa hatua hii isiiachie ATCL pekee bali ifike pia katika Shirika la Reli nchini (TRL). Soma Zaidi ...

TAIFA STARS VS RASIL JUNI 2 DAR

Timu ya soka ya Taifa ya Brazil inatarajiwa kutua nchini kwa ajili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itakayopigwa Juni 2 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, alisema mazungumzo ya ujio huo yanaendelea chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Tenga alisema, timu hiyo itakayokuwa njiani kuelekea Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia, itasaidia kupitia mechi hiyo kukinoa kikosi cha Stars kitakachokuwa kikijiandaa na mechi yake ya marudiano na Rwanda ‘Amavubi’.

“Ujio wa Brazil utakuwa na manufaa kwetu, kwani utasaidia kuipa mazoezi timu yetu ya taifa ambayo baada ya hapo itaelekea Rwanda kucheza mechi yao ya marudiano,” alisema.

Katika hatua nyingine, Tenga aliipongeza timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ kwa kushinda mechi yao ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake, baada ya kuitandika Eritrea kwa mabao 8-1 mwishoni mwa wiki.

Tenga alisema, ushindi huo usiwafanye wabweteke, kwani wapinzani wao watakwenda kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya mechi yao ya marudiano, hivyo kufanya mchezo kuwa mgumu zaidi.

Wakati huohuo, tiketi 380 za mashabiki waliojiandikisha kwenda Afrika Kusini kushuhudia fainali za Kombe la Dunia, zimeishawasili jijini ambapo TFF inawahimiza wahusika kwenda kuzichukua.

.
Soma Zaidi ...

Tuesday, May 25, 2010

WANAJESHI WANAWAKE

Israel

India

North Korea

Rusia

U.S.A


Hawa ni wa wapi?
Soma Zaidi ...

LIYUMBA JELA MIAKA MIWILI

Mahakimu kuwa katika jopo hakumaanishi kuwa katika kufikia uamuzi watafanana katika fikra, welewa na mtazamo na hilo limedhihirika katika hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba.

Jopo hilo jana lilitofautiana na kuweka rekodi ambayo itakuwa ya mfano hata kwa wasomi wa sheria, baada ya Hakimu Edson Mkasimongwa kutofautiana na mahakimu wenzake Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa.

Wote walikuwa wameunda jopo la kusikiliza kesi ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Liyumba, ambaye mahakimu Mlacha na Mwingwa walimwona ana hatia na hivyo kumhukumu kifungo cha miaka miwili jela.

Lakini kwa upande wa Mkasimongwa, alimwona Liyumba kuwa hana hatia kwa kuwa mahakama ilishindwa kuthibitishiwa kama kweli alitumia madaraka yake vibaya katika ujenzi wa jengo pacha la BoT.

Hata hivyo Mkasimongwa alisema kwa kuwa wengi wape, hukumu ambayo itahesabika kuwa ndio uamuzi wa mahakama itaanza kusomwa na kufuatia yake ambayo itabakia kuwa kumbukumbu ya mahakama na kuhifadhiwa katika jalada la kesi hiyo.

Mkasimongwa katika uamuzi wake alisema mshitakiwa hana kesi ya kujibu kwa sababu mashitaka dhidi yake hayakuthibitishwa bila kuacha shaka yoyote kama sheria inavyotaka kwa kuwa kuna maswali mengi yalikosa majibu.

Akisoma hukumu yake ambayo aliiita mbadala, alisema katika barua zilizoletwa mahakamani na upande wa mashitaka kama vielelezo zikidaiwa kusainiwa na mshitakiwa, hazina majibu kwamba ni kweli alifanya mabadiliko hayo na kama alikuwa na mamlaka hayo, vile vile haikuelezwa na upande wa mashitaka kuwa menejimenti nayo ilikuwa ikijibu nini.

“Kuna uwezekano mabadiliko yale yaliridhiwa na Gavana na menejimenti yote, isingeleta swali kama kungekuwa na majibu au maelekezo tofauti,” alisema Mkasimongwa akiongeza kuwa ilitakiwa barua zilizokuwa zikimjibu mshitakiwa ziletwe, ili kujua na Utawala na Gavana walikuwa na uamuzi gani. Hivyo aliridhika kusema hakuna matumizi mabaya ya ofisi aliyotenda mshitakiwa.

Hakimu Mlacha ambaye alisoma hukumu halisi alianza kwa kumkumbusha mshitakiwa mashitaka aliyofikishwa nayo mahakamani hapo ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 221.

Hata hivyo mashitaka hayo yalifutwa na mahakama baada ya kukosa hatia wakati upande wa mashitaka ulipofunga ushahidi wake, pamoja na ya matumizi mabaya ya ofisi aliyokuwa amebaki nayo.

Mlacha alisema katika hukumu hiyo aliyoanza kuisoma saa 3.50 hadi saa 7.20 mchana, kwamba bila shaka ushahidi ulionesha mshitakiwa alikuwa mtumishi wa umma katika kipindi chote cha mwaka 2001 hadi mwaka juzi kwenye Mradi wa 10 Mirambo (majengo pacha) anaodaiwa kubadili sura yake wakati ukitekelezwa, kwa mujibu wa mashahidi wanane walioletwa na upande wa mashitaka na wawili wa utetezi.

Aidha alisema, mahakama inapingana na ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi ambao ulitolewa na mshitakiwa na Bosco Kimela ambaye alikuwa Katibu wa Bodi ya BoT ambao walidai kuwa Liyumba hakuhusika na mabadiliko ya sura ya mradi na badala yake kuutupa mpira kwa Gavana wa wakati huo Daudi Ballali na Meneja wa Mradi, Deogratius Kweka.

Katika ushahidi wao, walidai kuwa ingawa mradi ulikuwa chini ya kurugenzi yake, lakini mshitakiwa hakuhusika kutoa uamuzi. Vile vile mahakama haikubaliani na ushahidi wao kuwa Gavana alimteua mshitakiwa kwa mdomo, kusaini barua kwa niaba ya BoT, kwa kile walichodai kuwa Kweka hakuwa mwajiriwa wa kudumu wa benki hiyo.

Hata hivyo, katika uamuzi wa mahakimu hao walikubaliana na ushahidi wa upande wa Serikali kwamba mawasiliano yoyote ya ndani ya ofisi za BoT yalifanyika kwa njia ya maandishi na si kwa mdomo kama Liyumba alivyodai kupewa jukumu la kusaini barua kwa mdomo huku kukiwa na ushahidi mwingine kwamba Gavana naye hakuwa na uamuzi wa mwisho bali Bodi ya Wakurugenzi.

“Katika mradi huo uliolengwa kutekelezeka kwa mujibu wa mkataba, inakubalika kuwa haukutekelezeka kama ilivyotakiwa, yalikuwapo mabadiliko makubwa, ushahidi ulionesha kwamba katika matumizi yote ya maendeleo Bodi ndiyo ilikuwa na mamlaka ya mwisho, lakini katika mradi huu, kanuni hiyo haikufuatwa, fedha zililipwa bila utaratibu,” alisema Mlacha.

“Mahakama inasema mshitakiwa alisaini barua zote zilizokuwa zikitoa maelekezo ya kubadili mradi na alifanya hivyo bila mamlaka kinyume cha sheria matumizi yaliyoongezeka na kuathiri BoT na bila shaka Taifa kwa jumla,” aliongeza.

Baada ya mshitakiwa kuondolewa mahakamani, ndugu zake walilia huku wakidai kutoridhishwa na uamuzi huo.

Hata hivyo wakili Majura Magafu anayemtetea Liyumba, alisema jana wangewasilisha notisi Mahakama ya Rufaa ili kuonesha nia yao ya kukata rufaa kwani ni imani yao kuwa ushahidi katika kesi hiyo haukuchambuliwa ipasavyo.

Mtuhumiwa huyo alikaa rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitatu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kutoa Sh bilioni 110.

Akiwa katika basi linalobeba washitakiwa lenya namba STK 4373, saa 7.41 mchana Liyumba alianza safari yake akitokea Kisutu kuelekea makazi yake mapya ambako atatumikia kifungo hicho cha miaka miwili jela.
.
Soma Zaidi ...

Monday, May 24, 2010

BURUNDI WAPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

Wananchi wa Burundi leo wamejitokeza kwa wingi kupiga katika uchaguzi wa serikali za mitaa, ambayo ni awamu ya kwanza kabla ya chaguzi nyingine, ubunge na urais June na Julai mwaka huu.

Uchaguzi huo uliahirishwa mara mbili hapo siku ya Ijumaa kutokana na matatizo ya kutokuwepo kadi na maboxi ya kuhifadhia kura. Hali hiyo, hali hiyo ilisababisha kuongezeka wasi wasi iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki. Hata hivyo, tume ya uchaguzi nchini Burundi imewahakikishia wananchi kwamba uchaguzi huo hakutakuwa na tatizo lolote.

Renate Weber, ambaye ni kiongozi wa waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya, alithibitisha kuwa idadi ya watu waliojitokeza ilikuwa kubwa.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema leo asubuhi, ambapo kiasi cha watu millioni 3.5 wenye haki ya kupiga kura wanatarajiwa kuwachagua madiwani wa serikali za mitaa. Uchaguzi huo ni kipimo muhimu kwa uchaguzi wa wabunge na ule wa rais.


Soma Zaidi ...

HAPA NI SKULI AU MAULIDINI????

Kwa kweli hii hali sasa imefika pabaya, imefikia mpaka wanafunzi kukalia mabusati? nikikumbuka wakati tukisoma sisi na hzi taswira za sasa napata picha ya kwamba tumerudi nyuma kwa miaka isiyopungua 30 kimaendeleo.
Soma Zaidi ...

HII SASA NOMA

Taa ya kandili ndani ya spitali moja huko Bongo baada ya kukosekana kwa huduma ya umeme.
Soma Zaidi ...

HUKUMU YA LIYUMBA LEO

Macho na masikio ya Watanzania wengi leo yanaelekezwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba (62).

Kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Edson Mkasimongwa, ambaye pia ni Msajili wa Baraza la Ushindani, ndiye anayetarajiwa kusoma hukumu hiyo inayosubiriwa kwa shauku kubwa.

Kusomwa kwa hukumu hiyo leo ni utekelezwaji wa amri iliyotolewa na kiongozi wa jopo hilo, Mkasimongwa, Aprili 22, mwaka huu, muda mfupi baada ya Liyumba anayetetewa na mawakili Jaji mstaafu Hillary Mkate, Onesmo Kyauke, Majura Magafu na Hudson Ndusyepo kumaliza utetezi wao.

Liyumba na Meneja Mradi wa Benki Kuu, Deogratius Kweka, walipandishwa kizimabani kwa mara ya kwanza Januari 27 mwaka jana na kufunguliwa kesi namba 27/2009, wakikabiliwa na mashitaka mawili ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma, mbapo Liyumba alidaiwa kuidhinisha mabadiliko ya ujenzi wa majengo ya minara pacha bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi wa BoT, hivyo kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Hata hivyo, Mei 27 mwaka jana Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, aliifuta hati ya mashitaka iliyokuwa ikiwakabili washitakiwa hao na kuwaachilia huru, lakini muda mfupi baadye walikamatwa tena na kupelekwa Kituo cha Polisi Salender Bridge na siku iliyofuata Liyumba peke yake ndiye alifikishwa mahakamani hapo na kufunguliwa kesi mpya namba 105/2009.

Aprili 9, mwaka huu, Liyumba alifutiwa shtaka la pili ambalo ni la kuisababishia serikali hasara hiyo. Mkasimongwa alisema jopo hilo limepitia kwa kina ushahidi uliotolewa na mashahidi wanane wa upande wa Jamhuri na vielelezo 12 na kupitia majumuisho ya kesi hiyo yaliyowasilishwa na mawakili wa pande zote mbili, jopo hilo liliona Liyumba ana kesi ya kujibu katika shitaka la kwanza la matumizi mabaya ya ofisi ya umma.

. Soma Zaidi ...

MASAUNI MASHAKANI

Jeshi la polisi nchini limesema linafanya uchunguzi wa nyaraka na vielelezo kuhusu umri wa mwenyekiti wa zamani wa jumuiya ya vijana ya chama cha mapinduzi UV-CCM, Hamad Masauni.

Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja baada ya Masauni kudaiwa kuhushi umri wake wakati wa kugombea wadhifa huo mwaka 2008.

Naibu kamishna wa jeshi la polisi anaekaimu ukurugenzi wa makosa ya jinai Piter Kibuyo amesema taarifa za vielelezo vya uchunguzi vitatolewa baada ya uchunguzi huo kukamilika.

Amesema katiba ya nchi inaeleza hakuna mtu alieko juu ya sheria hivyo iwapo Masauni ataonekana amehushi umri wake sheria itachukua mkondo wake

Masauni alitarajiwa kupokelewa leo kwa mapokezi ya aina yake, lakini umoja wa vijana wa UV-CCM, Zanzibar umesema hauhusiki na mapokezi hayo.

Uchunguzi uliofanywa na ndani ya Zanzibar umegundua kua mapokezi hayo yaliandaliwa na baadhi ya vijana wa CCM kutoka jimbo la uchaguzi analoishi Masauni.
. Soma Zaidi ...

MELI YA MEDITERRANEAN YANUSURIKA KUTWEKA

Meli ya MSC PEGGY ikiwa imefunga gati katika bandari ya Dar-es-salaam baada ya kunusurika kutekwa katika pwani ya Mtwara.
Soma Zaidi ...

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA BRITISH AIRWAYS WAGOMA

Mgomo wa siku tano wa shirika la ndege la Uingereza, British Airways umeanza leo baada ya viongozi wa shirika hilo na vyama vya wafanyakazi kushindwa kufikia makubaliano.

Kiongozi wa chama cha wafanyakazi cha Unite, Tony Woodley, aliwaambia waandishi habari jana Jumapili kwamba mgomo huo ungeweza kusimamishwa tu kama shirika la ndege la British Airways lingerudisha marupurupu ya usafiri kwa wafanyakazi wake.

Mkuu wa shirika hilo, Willie Walsh, ameapa kutekeleza mpango wa shirika hilo wa kubana matumizi.

Shirika la British Airways linapanga kupunguza matumizi kwa kiasi cha zaidi ya euro milioni 72 baada ya kupata hasara kubwa Ijumaa iliyopita, tangu lilipobinafsishwa mnamo mwaka 1987.

. Soma Zaidi ...

Sunday, May 23, 2010

STYLE IPI INARIDHISHA


Soma Zaidi ...

MAHUBIRI YALINICHOCHEA NIRIPUE UBALOZI

Mwanafunzi Nassib Mpamka (15), anayetuhumiwa kufanya jaribio la kulipua Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, amekiri na kudai kuwa alihamasishwa na mahubiri ya shehe wa msikiti wa Mtambani na kwamba wazo la kulipua ubalozi huo alikuwa nalo tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Mpamka, ambaye anashikiliwa na Polisi, katika madai yake alisema alitaka kulipua ubalozi huo baada ya kusikia mahubiri hayo aliyodai kuwa yalihusu majeshi ya Marekani kuua Waislamu duniani.

Hata hivyo, Katibu wa msikiti huo, Shehe Abdallah Mohamed, alipozungumza na gazeti hili juzi mara baada ya sala ya Ijumaa, alisema shule ya Mtambani ambayo awali Mpamka alidaiwa kusoma, haihusiki na kutoa mafunzo ya ugaidi na wala hakuna mwanafunzi wao aliyekamatwa akihusishwa na kashfa hiyo.

Shehe Mohamed alisema huenda kuna njama zinazoandaliwa na wahusika ambao hakuwataja majina, ambazo alidai lengo ni kuidhoofisha taasisi yao.

“Inawezekana uzushi wa jambo hili ukawa si wa bure, maana hata Marekani ilipotaka kuipiga Iraq ilianza kutoa visingizio vingi vikiwamo vya kuwapo silaha kali, kitu ambacho mpaka leo bado hakijathibitika,” alisema kiongozi huyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi, Peter Kivuyo akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu tukio hilo, alisema mtuhumiwa huyo alibainisha kuwa shehe huyo ambaye mpaka sasa hajatajwa jina, alikuwa akihubiri mara kwa mara kuhusu vitendo vya majeshi ya Marekani kuwaua Waislamu katika nchi mbalimbali duniani.

“Mwanafunzi huyo alisema kuwa mahubiri na mafundisho ya shehe huyo yalimgusa na mawazo yalijengeka akilini mwake, akapata wazo hilo tangu mwishoni mwa 2009… sasa sijui nisemeje, maana mafundisho mengine kwa kweli ni mabaya,” alisema Kivuyo.

Kivuyo alisema hivi sasa wanahojiwa watuhumiwa wawili, yaani Mpamka na mwenzake Amani Thomas (15), ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Biafra.

Thomas anadaiwa ndiye alikwenda na Mpamka kufanya jaribio hilo, lakini yeye alibaki katika eneo ambalo linatumika kuuzia maua lililo karibu na ubalozi huo, wakati Mpamka akifanya jaribio hilo.

Awali Kamishna Kivuyo alisema Mei 16 saa 2:30 usiku, Mpamka alifika katika viunga vya ubalozi huo katika eneo ambalo linaegeshwa magari ya kubebea maji na kurusha chupa iliyokuwa imejazwa mafuta ya taa na kuwekwa utambi kwa lengo la kulipua magari hayo. Kutokana na juhudi za walinzi wa ubalozi huo waliokuwa kazini, walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kumfikisha Polisi kwa mahojiano zaidi.

Kamishna Kivuyo aliongeza kuwa uchunguzi utakapokamilika, hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.

Awali gazeti hili liliripoti kukamatwa kwa Mpamka baada ya kudaiwa kuingia katika ubalozi huo kwa kupitia geti namba tatu na kujaribu kufungua koki ya tanki ya mafuta katika ubalozi huo.

Mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, siku iliyofuata maofisa wa usalama wa Taifa na polisi walifika katika shule ya sekondari ya Biafra na kuchukua wanafunzi wanane kwa ajili ya mahojiano kuhusu jaribio la kutaka kulipua ubalozi huo.

Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili na habari za uhakika kutoka ndani ya Polisi, ulibaini kuwa Mpamka ni mtoto yatima na alikuwa akiishi Kinondoni Moscow aribu na hoteli ya Livingstone, kwa shangazi yake aliyejulikana kwa jina la Chiku Simba.

Simba alipohojiwa na gazeti hili kama ana uhusiano na mtoto huyo, alijibu kuwa hamfahamu na akadai kuwa suala hilo halitambui na kwamba habari hizo amekuwa anazisikia tu kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, majirani wa kijana huyo walisisitiza kwamba kijana huyo alikuwa akiishi hapo na kwamba Simba ni shangazi yake. Baada ya kupata msisitizo huo, gazeti hili lilirudi kwa Simba kupata uhakika ambapo shangazi huyo alikiri kuishi na Mpamka na kukataa kuelezea zaidi.

Majirani wa Mpamka pamoja na marafiki zake wa mtaani, walieleza kushtushwa na habari za kijana huyo kwa maelezo kuwa mtoto huyo ni mkimya, hana mazoea na watoto wenzake na wala hana tabia ya kukaa vijiweni.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amekanusha kusema kwamba anatilia shaka ulinzi wa ubalozi huo, kutokana na tukio hilo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kova alisema yeye ndiye mwenye jukumu na wajibu wa kuhakikisha ulinzi wa balozi zote zilizoko katika kanda yake unakuwa wa uhakika na hivyo isingewezekana tena ajidharau.

“Haiji kwa mimi ambaye ndiye mlinzi wa balozi hizo ukiwamo wa Marekani, leo nigeuke na kusema ulinzi huo ni dhaifu na hivyo kuwa na shaka nao, pengine ilitafsiriwa vibaya niliposema ulinzi katika balozi umeimarishwa,” alisema Kamanda Kova.

.
Soma Zaidi ...

SMZ YAPATA "KIGUGUMIZI" KURIDHIA SHERIA YA RUSHWA 2007

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), kimesema Zanzibar imekumbwa na ‘kigugumizi’ na kushindwa kuridhia sheria ya kupambana na rushwa tangu ilipopitishwa na Bunge mwaka 2007

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kituo hicho Profesa Chris Maina Peter, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya haki za binadamu ya Zanzibar ya mwaka 2009 uliofanyika jana mjini Zanzibar.

Alisema tangu sheria hiyo kupitishwa imeshindwa kufanyakazi Zanzibar kwa vile inahitaji kuridhiwa na Baraza la Wawakilishi kwa vile masuala ya rushwa hayamo katika orodha ya mambo ya Muungano.

Hata hivyo alisema sheria hiyo ina umuhimu mkubwa katika kujenga misingi ya haki za Binadamu na utawala bora hasa katika vyombo vya kusimamia sheria.

Aidha alisema maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF yana nafasi kubwa ya kuondoa malalamiko ya watu kunyimwa fursa ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Alisema utafiti walioufanya wapo watu Unguja na Pemba hawajaandikishwa kutokana na urasimu wa vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi.

Hata hivyo alisema baada ya kufuatilia tatizo hilo kwa watendaji wa Idara ya usajili wa vitambulisho vya Mzanzibar Mkazi walisema vitambulisho vingi wanavyo baada ya wahusika kushindwa kujitokeza kwenda kuvichukua. Soma Zaidi ...

Saturday, May 22, 2010

KUWA MAKINI UNAPOVUKA TRAFFIC LIGHT

Soma Zaidi ...

JE TUMEJIFUNZA KUTOKANA NA CHAGUZI ZILIZOPITA?

Ndugu zetu,

Assalaam Alaaykum,

UMOJA, UHURU NA UADILIFU

Baada ya Uchaguzi wa 2005

Katiba ya Zanzibar ya 1984

Wakati Maalim Seif Sharif ni Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Katiba ya Zanzibar ilirejelewa na kuthibitishwa katika mwaka 1984. Ni ndivyo kabisa, kwa vile wakati huo nchi ilikuwa chini ya mfumo wa chama pekee (one-party system) katiba ya nchi kuwa ni yenye kulingana na mfumo wa kisiyasa ulikuwepo nchini wakati huo. Katiba hii ndio ilioendesha uchaguzi wa 1990, haikuwa sivyo kuwa hivyo, kwa sababu nchi ilikuwa katika mfumo wa chama pekee, na katiba halikadhaalika ilikuwa katika mfumo huo.

Kuletwa Nchini Mfumo wa Zaidi ya Chama Kimoja

Mnamo 1992 uliletwa nchini mfumo wa zaidi ya chama kimoja (multi-party system) na kufuta mfumo wa chama pekee (one-party system). Ilikuwa ni ndivyo kabisa mara tu baada ya kuletwa mfumo huo wa zaidi ya chama kimoja, wakati huo huo katiba ya nchi itengenezwe iwe yenye kulingana na mfumo wa kisiyasa uliopo nchini, yaani mfumo wa zaidi ya chama kimoja. Hili halikufanywa, nchi iliendelea kuishi katika katiba ya mfumo wa chama pekee hali ya kuwa nchi wakati huo ishaingia kwenye mfumo wa chama zaidi ya kimoja. Huu ni mpingano mkubwa wa kisiyasa na kiutaratibu wa uendeshaji wa mambo ya nchi.

Uchaguzi wa 1995

Uchaguzi wa 1995 ndio uchaguzi wa awali kufanywa tangu pale nchi kuingizwa kwenye mfumo wa zaidi ya chama kimoja. Lenye kushangaza ni kwamba kwa muda wa miaka mitatu hata kufika huu uchaguzi wa 1995 katiba ya nchi iliendelea kubakia ile ile ya mfumo wa chama pekee. CUF, wakiwa ni wakhusika na waathirika kwa kubaki katiba kongwe kwenye mfumo mpya ilikuwa ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanaingia kwenye uchaguzi kwa katiba ya zaidi ya chama kimoja, badala ile ya chma pekee. CUF waliingia kwenye uchaguzi kwa katiba ile ile ya chama pekee.

Uchaguzi wa 2000

Maara tu baada ya uchaguzi wa 1995 ilikuwa ni wajibu wa CUF kudurusu na kuzingatia matokeo ya uchaguzi huo na kujifunza kutokana na kasoro zake. Kuu ya kasoro hizo ni ile katiba kongwe, katiba iliokwisha pitwa na wakati. Madhumuni muhimu ya kuzingatia kasoro hizo ilikuwa ni kupanga nyenzo na mbinu za kuepuka zisitokee kasoro hizo kwenye uchaguzi ufuatiao, yaani ule wa 2000. CUF haikufanya hivyo, natija yake kasoro zilezile - kuu ya kasoro hizo ni vile kutumika katiba ileile, katiba kongwe iliokwisha pitwa na wakati - ziliokuwepo katika uchaguzi wa 1995 zilitokea tena, na kuongeza maafa baada ya uchaguzi.

Uchaguzi wa 2005

Maara nyingi baada ya uchaguzi wa 2000 na matokeo yake, CUF walikuwa wakiahidi Umma kwamba hawataingia kwenye uchaguzi 2005 mpaka katiba itengenezwe ilingane na mfumo uliomo nchini, yaani mfumo wa zaidi ya chama kimoja. Miezi michache tu kukaribia wakati wa uchaguzi, uongozi wa CUF uligeuza muelekeo wake na kuanza kusema kuwa CUF itaingia kwenye uchaguzi hata kama katiba haitageuzwa. Kitendo hichi kiliwatia khofu na wasiwasi wengi waliokuwa wakitarajia matengenezo nchini Zanzibar. Zaidi wengi walitambua natija ya uchaguzi itakavyokuwa iwapo CUF wataingia kwenye uchaguzi katika katiba kongwe, katiba iliokwisha pitwa na wakati. Wengi walinasihi kuwa CUF ni vyema wasiingie kwenye uchaguzi iwapo katiba haitatengenezwa. Wako waliofika kuwaeleza CUF kuwa natija za uchaguzi itakuwa ndio kama vilevile za uchaguzi zilizopita, yaani ule wa 1995 na wa 2000. Uongozi wa CUF uling’ng’ania kuingia kwenye uchaguzi kwa hali yoyote ile.

Muumini Hatafunwi na Nyoka Pango Moja Mara Mbili

Mafunzo ya Dini yetu tukufu yanatufunza kwamba Muumini haifai kutafunwa na nyoka pango moja mara mbili. Makusudio ni kwamba ni wajibu wa Muumini kuchukuwa kila hadhari baada ya kuumwa na nyoka. Waswahili wanasema: “Ukiumwa na nyoka, ukiona ung’ongo huogopa”. Hii ndio sifa ya Muumin, bali ni ndivyo kwa kila mwenye busara. Kwa nini tukaumwa na nyoka pango moja mara tatu, 1995, 2000 na 2005. Kitendo hiki si dharau tu, bali ni zaidi ya hivyo; si sio kuwa ni mpango wa makusudi kwa madhumuni makusudi. Hatujui uchaguzi wa 2010 utakuwa vipi, lakini tukilinganisha matokeo ya tangu 1995, tuna sababu ya kukhofia kwamba na uchaguzi wa 2010 utakuwa vilevile katika katiba ileile kongowe ya 1984. Je, ikiwa hivyo ni nani wa kulaumiwa, ni uongozi wa CUF au Umma wa Zanzibar? Penye uhai tutaona.

Tufanyeje?

Naileta makala hii humu barazani mwetu adhimu, si kwa kuwa haya niliojaaliwa kuyaeleza yupo asieyajuwa na kuyafahumu, bali madhumuni khasa ya kuleta maelezo haya ni kuomba mashauri ya ndugu zetu wa ukumbi huu nini la kufanywa ili kuendeleza juhudi za kufikia matengenezo ya nchi yetu.

Wa Billah Tawfiiq

Frouk

May 22, 2010

. Soma Zaidi ...

Friday, May 21, 2010

WABONGO NA MABANGO YA MWISHO WA DUNIA

Bango hili ambalo linaonesha tarehe mwezi na mwaka ambapo dunia itafikia mwisho wake lipo maeneo ya Ubungo kwenye kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani, ama kweli uendawazimu uko wa aina nyingi Soma Zaidi ...

UWANJA WA AMANI WAA WAAAAA!!!

Muonekano wa uwanja mpya wa amani baada ya ukarabati
Rais wa Zanzibar ambae ni mwenyekiti wa baraza la mapindizi mh, Amani Karume akikagua uwanja mpya wa Aamani baada ya kufanyia ukarabati na Wachina.
Soma Zaidi ...
Kitendawili cha timu ipi itatwaa ubingwa katika wa Ligi Kuu Zanzibar msimu huu kinazidi kuwa kigumu hasa kutokana na matokeo ya mchezo wa juzi kati ya Miembeni na Duma.

Mchezo huo ulimalizika kwa Duma ya Pemba kuilaza Miembeni bao 1-0. Timu hizo zilianza mchezo kwa kasi, huku zikionekana kukamiana zaidi lakini umaliziaji kwa pande zote ulikuwa tatizo.

Miembeni kila inapocheza, imekuwa ikipata mashabiki wengi wakiwemo wanawake, jambo ambalo si nadra kuonekana zikicheza timu nyingine ilijikuta ikipoteza mwelekeo wa kuwemo katika kinyang'anyiro cha timu zinazogombea ubingwa msimu huu.

Mchezaji Ali Ahmed, aliyefanikiwa kuifungia Duma bao pekee na la ushindi katika mchezo huo, dakika ya 22 na kudumu hadi mapumziko.

Licha ya Miembeni kucheza kwa kasi zaidi kipindi cha pili, huku wachezaji wake Khamis Mcha " Viali" Said Kuzu na Othman Omar "Mani" kuhaha huku na kule kutaka kukomboa bao hilo, lakini ulinzi wa Duma ulikuwa mkali na kuhakikisha timu hiyo haiondoki na pointi kiwanjani hapo.

Ushindi huo wa Duma umeifanya timu hiyo kufikisha pointi 22 na kukamata nafasi ya tatu nyuma ya Zanzibar Ocean View yenye pointi 23 na KMKM inayoongoza ligi ikiwa na pointi 24.
Soma Zaidi ...

10 WAOKOLEWA AJALI YA BOTI ZANZIBAR

Watu 10 wameokolewa baada ya mashua ya MV Muafaka kuzama ikiwa na magunia 200 ya mkaa katika mwambao wa Makoongwe Kisiwani Pemba.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hassan Nassir, alisema watu hao pamoja na wafanyakazi wa boti hiyo, waliokolewa juzi na boti ya wavuvi iliyokuwa ikielekea Mombasa nchini Kenya.

Alisema boti hiyo ya wavuvi iliwaona watu hao wakielea baharini na ndipo walipoamua kutoa msaada huo wa kuwaokoa na kuwapeleka katika kisiwa cha Kokota, Mkoa wa Kaskazini Pemba kabla ya kuchukuliwa na boti ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).

Hata hivyo, alisema mtu mmoja, Khalid Hassan, alipoteza nguvu na kuzama baharini wakati juhudi za kuwaokoa zilipokuwa zikifanyika katika eneo hilo.

Aliwataja abiria waliookolewa kuwa ni Ramadhani Abdallah (30), mkazi wa Mapinduzi, Said Juma Bakari (26), mkazi wa Mtambwe, Juma Haji Silima (54), mkazi wa Mtuhaliwa, Mcha Haji (22), mkazi wa Mkoani na Mohammed Khamis Muhidini (65), mkazi wa Mtuhaliwa na Hassan Ali Hassan (21).

Pia aliwataja mabaharia waliokolewa katika chombo hicho kuwa ni Khamis Suleiman Mohammed, Shaibu Khamis Faki, Ali Bakari na Khamis Hassan Mwalimu akiwemo pamoja na nahodha wa chombo hicho.

Kamanda Nassiri alisema nahodha wa chombo hicho aliachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika kuhusiana na tukio hilo.

Aidha, alisema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mashua hiyo ilikuwa na abiria 11.

Alifafanua kuwa mashua hiyo ilisajiliwa kwa kazi ya kubeba mizigo lakini nahodha huyo alibeba abiria saba katika chombo hicho.

Alisema mashua hiyo ilipakia magunia 200 ya mkaa katika kijiji cha Fumbani lakini baada ya kufika katika mwambao wa Makongwe, chombo hicho kilianza kuingiza maji na kulazimika kurudi walikotoka kabla ya kuzama.

Hata hivyo, Kamanda Nassiri aliwataka wananchi kujiepusha kutumia usafiri wa vyombo vya baharini visivyokuwa na usalama wa maisha yao.

Kisiwa cha Pemba kimekabiliwa upungufu wa usafiri tangu meli za Serikali MV Mapinduzi na MV Maendeleo kusimama kutoa huduma kutokana na uchakavu na meli ya MV Serengeti kuwaka moto ikiwa imetia nanga katika Bandari ya Malindi, Zanzibar. Soma Zaidi ...

Thursday, May 20, 2010

MWAKILISHI WA HRW AFUKUZWA BURUNDI

Serikali ya Burundi imefuta kibali cha kufanya kazi nchini humo,kwa mwakilishi wa Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu-Human Rights Watch, Neela Ghoshal. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Burundi imemwandikia barua Bibi Ghoshal ikimtaka asimamishe shughuli zake mara moja na kuondoka nchini humo ifikapo tarehe 5 mwezi ujao wa Juni.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya shirika hilo wiki iliopita kuchapisha taarifa kuhusu vurugu zinazoendelea Burundi kabla ya uchaguzi mkuu. Serikali ya Burundi imesema miongoni mwa mambo mengine, ripoti hiyo iliegemea upande mmoja ikiwa dhidi ya serikali na chama tawala. Shirika hilo limeelezea kusikitishwa kwake na uamuzi huo uliochukuliwa dhidi ya Ghoshal.

Mwezi Desemba, mwaka jana Burundi ilimfukuza nchini humo mkuu wa zamani wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi-BINUB, Youssef Mahmoud, kwa madai alikua karibu sana na upande wa upinzani. Maafisa wengine wawili wa Umoja wa Mataifa walifukuzwa nchini humo mwaka 2006 kwa madai sawa na hayo.
Soma Zaidi ...

MKUTANO WA MSUKOSUKO WA FEDHA ULIMWENGUNI BERLIN

Berlin , mji mkuu wa Ujerumani,wiki hii , ni shina la harakati za kuutatua msukosuko wa fedha ulimwenguni:Bunge la Ujerumani-Bundestag, likijadiliana juu ya mikopo kwa nchi za Umoja wa Ulaya, zilizokumbwa na shida za madeni.Wakati huo huo, wabunge wanavutana kuhusu fedha zitoke wapi za kupambana na msukosuko kama huu ukizuka tena . Isitoshe, inazungumzwa vipi , masoko ya fedha nayo yachangie kukabiliana na gharama za msukosuko huo.Hapo, kuna maafikiano lakini, tofauti zinazuka ni kwa aina gani ?

Nia ya kuyawekea vikwazo vikali vya kisheria masoko ya hisa, aliitangaza Rais Barck Obama wa Marekani, hapo Septemba, mwaka uliopita wakati wa mkutano wa kilele wa kundi la mataifa tajiri 20-(G-20) huko Pittsburgh,Marekani.Lakini, maneno yake hayakufuatia vitendo.Kwani, kuna masilhai tofauti kati ya nchi za kiviwanda na zinazoinukia na hivyo,jinsi ya kupitisha sheria hizo kuna misimamo tofauti.Miongoni mwa wale ambao hawataki tena kutumbua macho tu hali hii ikiendelea, ni waziri wa fedha wa Ujerumani Bw. Wolfgang Schäuble.Alisema katika Bunge la Ujerumani :

"Nime fadhahishwa mno na jinsi Jumuiya ya ya Kimataifa, inavyokabiliana na msukosuko huu wa fedha na wa mabenki.Ndio, kuna baadhi ya mambo yamepatiwa ufumbuzi tena haraka mno kuliko ilivyotazamiwa,lakini, bado hatahivyo, mambo yanakwenda pole pole mno.Kuna wakati mtu anahisi kuwa kasi imepungua."

Mapema Februari, mwaka huu, Bw.Schäuble,alisema juhuidi za kutunga sheria bora za kuyadhibiti masoko ya fedha, zisiache kutiliwa kasi hata ikiwa athari mbaya za msukosuko huu wa uchumi zimedhibitiwa.Akawaambia mawaziri wenzake wa fedha kutoka nchi 7 tajiri za kiviwanda (G-7) kuwa anapanga kandoni mwa mkutano wa kilele wa nchi tajiri-20,mwezi ujao wa Juni, nchini Kanada, kuitisha kikao cha maandalio kitakacho wajumuisha Viongozi wa Benki -Kuu,Idaraza za usimamizi wa shughuli za mabenki , Taasisi za fedha za Kimataifa na wataalamu wa sayansi za kiuchumi.

Ni mkutano ambao sasa unachukua sura nyengine kabisa .Msukosuko wa Mabenki na kuzorota kwa uchumi, umefuatiwa sasa na msukosuko wa madeni ya serikali.Ugiriki imefilisika kope si zake na nchi nyengine zanachama wa UU, zinaweza kufuata mkondo huo wa Ugiriki.Thamani ya sarafu ya Euro inaanguka.

Waziri wa fedha wa Ujerumani, anasema kwahivyo, yawapasa kuilinda sarafu yao ya pamoja ya Euro.Hivi sasa imezuka hali ya kuiingiliwa sarafu hiyo na hali katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa kadiri ambayo wakati wa kuasisiwa kwa Umoja wa sarafu ya ulaya (Euro) hakuna alietazamia...

Kutokana na shinikizo la kuzidi kwa msukosuko wa sarafu ya Euro, yabainika mengi ghafula sasa yanawezekana .Kwa mshangao wa wengi, juzi Jumaane, hatua ambazo hazikupata wingi wa kura kuzipitisha na serikali ya muungano wa vyama-tawala vya CDU-CSU na FDP, zilipitishwa.

Nae Kanzela Angela Merkel akasema: "Katika sekta ambayo Ujerumani kwa kujiamulia mambo pekee hakutailetea dhara, tutajiamulia wenyewe ; na tulioyapituisha, yatabakia kufanya kazi hadi sheria kwa Umoja wa Ulaya nzima , zimepitishwa."
.
Soma Zaidi ...

Wednesday, May 19, 2010

KENYA YAWA NCHI YA TANO KUTIA SAINI MAKUBALIANO

Kenya imetia saini leo mkataba mpya wa kugawana maji ya mto Nile baada ya nchi nne nyingine kufanya hivyo wiki iliyopita.

Ethiopia, Rwanda, Tanzania na Uganda zilitia saini mfumo huo wa ushirikiano katika bonde la mto Nile siku ya Ijumaa licha ya upinzani mkubwa kutoka kwa nchi za Misr na Sudan.

Waziri wa maji nchini Kenya Charity Ngilu amesema kuwa ni jukumu la Misr na Sudan sasa kuingia katika mkataba huo na kukubaliana na mataifa hayo kugawana maji ya mto Nile.

Makubaliano hayo mapya yanachukua nafasi ya mkataba uliotiwa saini mwaka 1959 kati ya Misr na Sudan ambao unatoa udhibiti kwao wa zaidi ya asilimia 90 ya maji ya mto huo.

mataifa ambayo mto huo unapitia yanataka kutekeleza miradi ya mabwawa ya umeme na umwagiliaji kwa kushauriana na Misr na Sudan, lakini bila ya Sudan kuwa na kura ya turufu iliyopewa na mkataba wa enzi za ukoloni na Uingereza mwaka 1929.

. Soma Zaidi ...

ALAIN ROBERT ALIPOPANDA BURJ KHALIFA



Alain Robert Spiderman wa kifaransa ambae ni bingwa wa kupanda minara na majumba marefu bila ya kutumia chombo chochote kwa ajili ya uslama wake, amepanda jengo la Burj Khalifa lilioko Dubai kwa takriban dakika 20 tu, jengo ambalo ndilo refu kuliko majengo yote duniani huku umati wa watu ukiwa unashuhudia kitendo hicho.
.
Soma Zaidi ...

WAZANZIBARI MSIOGOPE SOKO LA PAMOJA EAC

Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kuondoa woga baada ya nchi wanachama kusaini mkataba wa kuanzishwa kwa soko la pamoja la Jumuiya la Afrika Mashariki (EAC) linalotarajiwa kuanza utekelezaji wake Julai, mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mohammed Aboud Mohammed, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Baraza la Biashara Zanzibar (ZBC), uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, mjini hapa jana.

Alisema soko la pamoja la Jumuiya hiyo lina faida kubwa kwa nchi wanachama katika kukuza uwekezaji, kuongeza masoko na ajira kwa wananchi toka nchi wanachama wake.

Waziri Aboud alisema wafanyabiashara na wananchi wa Zanzibar, wanapaswa kujitayarisha ili waweze kulitumia vizuri soko la pamoja hasa katika masuala ya uwekezaji na masoko ya ndani ya nchi wanachama.

Hata hivyo, alisema soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki litatawaliwa na ushindani mkubwa na kuwataka wananchi kujenga mazingira mazuri yatakayowasaidia kunufaika na ajira ndani ya soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema serikali ya Muungano na ya Zanzibar, tayari zimeweka mazingira ya kulinda ajira za ndani ya Zanzibar kwa vile wageni watanufaika na ajira ambazo wataalamu wake hawapatikani ndani ya nchi.

Waziri Aboud alisema Zanzibar ni nchi ya visiwa lazima kuwepo na utaratibu wa kulinda ajira za ndani ndiyo maana serikali imeamua kuweka ajira maalum kwa wageni.

“Serikali ya Muungano imezingatia maslahi muhimu ya nchi kabla ya kuingia katika soko la pamoja na hakuna sababu kwa wananchi kuwa na woga kuhusu soko la pamoja,” alisisitiza.

Alisema Zanzibar inatarajia kunufaika na miradi mikubwa ya maendeleo kupitia jumuiya hiyo ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege Karume kisiwani Pemba, bandari huru, umeme wa pepo na mradi wa kilimo Zanzibar.

Alisema mradi wa bandari huru, unatarajiwa kujengwa katika eneo la Mpigaduri na utagharimu dola za Marekani milioni 400 na mradi wa umeme wa upepo dola milioni 70 wakati ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba utagharimu dola milioni 78 na mradi wa kilimo dola milioni 100.

Alifafanua kuwa miradi hiyo itasaidia utekelezaji wa Mpango wa serikali wa Kukuza Uchumi na Kupunguza umaskini kwa wananchi wa Zanzibar (Mkuza).


. Soma Zaidi ...

MAKONTENA 50 YAINGIZWA ZANZIBAR BILA YA KODI

Makontena 50 ya saruji yenye thamani ya Dola za Kimarekani 84,000 sawa na Sh. milioni 114.8 yameingizwa Zanzibar yakitokea nchini Pakistan bila kulipiwa kodi kupitia Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.

Uchunguzi uliofanywa umegundua kuwa makontena hayo yaliingizwa visiwani humu kufuatia msamaha wa kodi uliotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini.

Kibali cha msamaha wa kodi kimetolewa Mei 12, mwaka huu chenye kumbukumbu namba WF/EXEMPT/TA/2010/VOL.II/NO.2 akitakiwa Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Zanzibar kutotoza kodi ya ushuru wa forodha mzigo huo.

Shehena hiyo ya Saruji ililetwa Zanzibar na meli ya mizigo ya MV Concord ikitokea Karachi nchini Pakistan na kuwasili Zanzibar wiki iliyopita. Nyaraka za usafirishaji mzigo huo yenye kumbukumbu namba Karzan-091 ya Aprili 24, mwaka huu, inaonyesha makontena hayo yaliletwa na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Abdul Enterprises C/F Company ya Darajani mjini Zanzibar.

Kampuni hiyo imepewa kazi ya kuingiza saruji hiyo na Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ.

Kwa mujibu wa msamaha wa kibali cha msamaha wa kodi cha waziri saruji hiyo haitakiwi kutozwa ushuru wa forodha pamoja na Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT)

Hata hivyo, saruji hiyo imeanza kuingia katika soko la ndani la Zanzibar na kuuzwa katika maduka ya rejareja. Mzigo huo wa saruji uliingizwa nchini kwa kutumia nyaraka za usafirishaji zenye namba 20100425CON703ZNZ ya Aprili 25, mwaka huu.

Naibu Kamishina wa TRA Kanda ya Zanzibar, Hassan Mcha, alithibitisha jana makontena hayo kutolewa bila ya kulipiwa kodi kutokana na msamaha wa kodi uotolewa na Waziri wa Fedha Zanzibar.

Akizungumza na Nipashe Dk. Makame alithibitisha kutoa msamaha huo lakini alisema hana taarifa kama saruji hiyo imeanza kuingizwa katika soko la ndani la Zanzibar.
.
Soma Zaidi ...

CCM OYEEEEEEEEEEEE


Soma Zaidi ...

Tuesday, May 18, 2010

BOATENG AOMBA RADHI KWA KUMUUMIZA BALLACK

Kevin Boateng ameomba radhi kutokana na kumchezea rafu mbaya nahodha wa Ujerumani Michael Ballack katika mechi ya fainali ya kombe la chama cha soka cha Uingereza FA kati ya timu ya Portsmouth na Chelsea.Rafu hiyo imemfanya Ballack kuzikosa fainali zijazo za kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

Boateng ambaye anatoka Ghana lakini mzaliwa wa Ujerumani,ameliambia Gazeti la michezo la hapa Ujerumani Sport-Bild kuwa hakudhamiria kumchezea rahi hiyo Ballack.

Kocha wa Ujerumani Joachim Löw ametangaza kuwa sasa kiungo wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger ndiye atakayebeba jukumu la kusimamia kiungo katika kikosi cha Ujerumani.

Wakati huo huo, mahakama ya kimataifa ya michezo iliyoko uswis imetupilia mbali rufaa ya timu ya Bayen Munich kutaka kuondolewa kwa adhabu ya kutocheza mechi tatu inayomkabili kiungo wao Frank Ribery.Kufuatia hukumu Ribery hatoweza kuwemo katika kikosi cha timu kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya Jumamosi ijayo dhidi ya Inter Milan ya Italia Soma Zaidi ...

NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA AFGHANISTAN ABIRIA WAHOFIWA KUFA

Balozi za Marekani na Uingereza mjini Kabul Afghanistan, zimethibitisha kuwa raia watatu wa Uingereza na mmoja wa Marekani, walikuwa katika ndege ya kiraia iliyoanguka nchini humo.

Haijafahamika iwapo kuna abiria wowote waliyonusurika katika ajali hiyo, ambapo hali mbaya ya hewa imekuwa kikwazo kwa waokoaji kufika katika eneo la ajali

Ndege hiyo ikiwa na abiria 44 sita wakiwa ni raia wa nje, ilianguka jana katika mameneo ya milimani kaskazini mwa Afghanistan.Ni ndege ya shirika binafsi la Afghanistan liitwalo Pamir Airways. Soma Zaidi ...

Monday, May 17, 2010

WAFANYA BIASHARA WA ZANZIBAR WALALAMIKA KUTOZWA KODI MARA MBILI

Baraza la biashara Zanzibar limesema suala ya wafanyabiashara wa Zanziar kutozwa kodi mara mbili Tanzania bara linaweza kuathiri shughuli zao mara baada ya kuanza kwa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika mashariki Julai mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari katibu mtendaji wa baraza hilo Ali Vuai amesema licha baraza hilo kuyapatia ufumbuzi zaidi ya matatizo 60 yanayowakwamisha wafanyabiashara wa Zanzibar, lakini suala hilo haliko mikonini kwa Zanzibar.
Hata hivyo amesema suala hilo linaendelea kujadiliwa katika vikao vya kero za muungano vinavyohusisha mawaziri wa pande mbili za muungano chini ya mwenyekiti wake makamo wa rais wa Tanzania.

Aidha Vuai amesema katika kuwatayarisha wafanya biashara wa Zanziar kuingia katika soko la pamoja la jumuiya ya Afrika mashariki Jumanne ijayo litaendesha mkutano utakao wajumuisha zaidi ya wajumbe 300 kutoka ndani na nje ya Zanzibar.

Amesema lengo la mkutano huo ni kuwaemisha wafanyabiashara wa Zanzibar juu ya umuhimu wa kulitumia soko hilo pamoja na kuyapatia ufumbuzi matatizo yao watakayokabiliana nayo katika soko hilo.

Nae mkurugenzi wa Idara ya biashara Zanzibar Rashid Ali akizungumzia suala la misamaha katika soko hilo amesema misamaha ya bidhaa haitaombewa kwa mtu mmoa bali itaombewa kwa wafanyabiashara wote watakaoingiza bidha zinazoombewa msamaha. Soma Zaidi ...

MKUTANO WA WAISLAM NA SERIKALI WAANZA LEO UJERUMANI

Baraza jipya la waislam nchini Ujerumani leo linaanza mkutano wake wa kwanza mjini Berlin .Sambamba na hilo katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkali.

Majadiliano hayo kati ya wawakilishi wa serikali ya Ujerumani na wawakilishi wa waumini wa dini ya kiislam nchini Ujerumani leo yanaingia katika duru ya pili, baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Wolfgang Schäuble katika duru ya kwanza miaka minne iliyopita kuwasilisha ajenda muhimu mbele ya kamati hiyo.Sasa masuala hayo yako chini ya mrithi wake Thomas de Maizière kwa ufafanuzi zaidi.

Masuala hayo ni pamoja na elimu kwa maimamu katika vyuo vikuu vya hapa Ujerumani, mafunzo ya dini ya kiislam katika shule, mambo yaliyokatazwa katika uislam pamoja na chuki dhidi ya uislamu katika jamii ya Ujerumani

Kwa upande mwengine katika mkutano huo, kuna wawakilishi kutoka serikali kuu, serikali za mikoa pamoja na serikali za mitaa.Aidha kuna wajumbe wa vyama vinavyowakilisha takriban asilimia 20 ya waislam wa Ujerumani pamoja na watu binafsi waliyoalikwa kutoa mitizamo yao kwa niaba ya waislam wengine.

Hata hivyo Mwanzoni mwa mwaka huu waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani aliikatalia jumuiya mojawapao muhimu ya waislamu-baraza la waislamu,Milli Görüs kushikiriki kwa ukamilifu kwenye mkutano. Waziri huyo alieleza kwamba jumuiya hiyo bado ipo chini ya uchunguzi .

Lakini waziri wa mambo ya ndani wa sasa Thomas de Maiziere pia amesisisttza kwamba uamuzi huo ulikuwa sahihi.

Akizungumza hivi karibu waziri huyo alisema:

´´ Milli Görüs kwa muda mrefu imekuwa si miongoni mwa washiriki katika mkutano wa kiislam.Alimradi ni uchunguzi wa kisheria na siyo dhidi ya mtu binafsi, lakini pia juu ya tuhuma za vyama hivyo kutumiwa kwa ajili ya kufanya uhalifu, au ukwepaji kodi na tuhuma nyingine nzito,basi nakubaliana na uamuzi huo´´

Baraza la waislam lilitangaza kujitoa kabisa kushiriki katika majadiliano hayo na serikali.Chama kingine cha pili kwa ukubwa cha waislam nchini Ujerumani kilichomo katika baraza la waislamu nacho mnamo siku chache zilizopita kilitangaza kujiondoa kutoka katika majadiliano hayo.

Sababu kubwa ni kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani alikataa kwanza kufanyika kwa kikao cha ndani na waislam kuhusiana na suala la uwakilishi katika majadiliano hayo.

Lakini Waziri huyo wa Ndani de Maizière ameendelea kushikilia msimamo wake huo.

´´ Huko kungelikuwa sawa na kukataa misingi ya mkutano na hilo mimi nimelipinga vilevile.

Nasikitika kwa hayo lakini,mkutano unaweza kufanyika bila ya baraza hilo la waislamu´´.

Iwapo waziri wa mambo ya ndani ataendelea kutokubali kufikiwa kwa mwafaka basi mdahalo unaweza kufanyika nje ya mchakato wa mkutano. Huo ndi msimamo wa baraza Kuu la waislamu.


Aiman A. Mazyek ambaye ni Katibu Mkuu wa baraza hilo amemshutumu Waziri huyo wa ndani kwa kuuuweka mdahalo chini ya sera za wageni, hali suala hilo linawahusu waislamu milioni nne wanaoishi nchini Ujerumani.

´´Bilashaka bado hatujaufunga mlango , lakini tumesema tu ni kuwa kuna mipaka na kwamba hatuwezi kuendeleaa hivyo ati kwa sababu tu ya kushiriki.Tunataka kujadili uislamu katika misingi ya kanuni zetu lakini siyo kwa sera za wageni na za kuwahusisha wageni katika jamii ya kijerumani, uislamu hauhusiani na hayo, kwa hivyo tunaona kushiriki ni kama kupoteza nguvu ´´

Mkutano huo wa Berlin unafanyika siku moja baada ya kumalizika kwa kikao cha maimamu wa kiislam barani Ulaya huko mjini Vienna Australia, ambako wawakilishi kutoka Ujerumani Uingereza na Uholanzi, walielezea umuhimu wa kushirikiana na mamlaka husika pamoja na polisi katika kuzuia ongezeko la vijana wenye kufuata itikadi kali za kiislam.
Soma Zaidi ...

Saturday, May 15, 2010

FA Cup - Chelsea win Double as Pompey miss chance


Didier Drogba's free-kick gave Chelsea a 1-0 win over Portsmouth in an extraordinary FA Cup final at Wembley.

Drogba's strike came three minutes after Portsmouth's Kevin Prince Boateng saw a penalty saved by Petr Cech, while Frank Lampard also missed a spot-kick late on.

Carlo Ancelotti's first season at Stamford Bridge ended in glory as Chelsea won their first league and cup Double - a feat beyond even Jose Mourinho.

It was Drogba's third FA Cup final goal, after his exploits against Manchester United in 2007 and Everton in 2009. And on a day of landmarks, Ashley Cole won a record sixth FA Cup - three with Arsenal and three with Chelsea, all since 2002.

Portsmouth won the pre-match battle by a landslide. While their fans were out in force waving flags an hour before kick-off, the Chelsea end was half-empty until the traditional strains of 'Abide With Me' coaxed them off the concourses and into their seats.

The team was not so slow to get going, as Chelsea hit the woodwork five times in an amazing first-half onslaught. First Lampard struck a dipping 35-yarder that left David James totally stranded and clipped the outside of the right-hand post on 14 minutes. Then Drogba had two chances, both charged down superbly by Aaron Mokoena as Portsmouth put bodies on the line to protect their goal.

A minute later came a glorious opportunity for Portsmouth's Frederic Piquionne, who had most of the goal to aim at as he redirected a powerful Boateng volley, but shinned it to the only place where Cech could save it.

Chelsea responded by squandering an open goal of their own - an even more incredible miss. Ashley Cole dribbled to the left byline, drew James and laid the ball across to Salomon Kalou who somehow shot against the crossbar from three yards.

Next it was John Terry's turn to rattle the frame of Portsmouth's goal, as he headed a Florent Malouda free-kick onto the bar.

On 38 minutes Drogba battered a long-range free-kick that James pushed on to the bar. The ball dropped down and bounced away.

Drogba celebrated but the referee's assistant somehow correctly judged from 50 yards away that the ball was only three-quarters over the line. Shades of Geoff Hurst in 1966, but this time there was no goal. How Chelsea must have longed for a Russian linesman.

Drogba was at it again four minutes later, chesting the ball down and shooting low against the left-hand post from close range. He reacted by punching the goal frame. For once, the Ivorian's frustration was perfectly understandable.

Amid the madness, Michael Ballack sustained an ankle injury that forced him out of the game and could make him a doubt for Germany's World Cup campaign.

Portsmouth started the second period stronger, and within 10 minutes had the chance to pull off a remarkable reversal. Aruna Dindane danced into the box and the substitute Juliano Belletti brought him down with a crude challenge. Penalty.

The pressure was too much for Boateng, who hit a weak penalty low down the middle - Cech could hardly fail to save with his legs.

The punishment was swift and devastating. Chelsea hit the post a sixth time when Drogba struck his free-kick on 59 minutes, but this time it was en route to the back of the net.

The Portsmouth wall parted in the face of the Ivorian's dipping strike, and a wrong-footed David James could not prevent the ball finding the bottom-right corner.

Boateng pulled his shirt over his head, unwilling or unable to witness the almost immediate consequence of his blunder.

Lampard should have put the result beyond doubt on 88 minutes when he was brought down by Michael Brown, but shot wide of the left-hand post.

Although there was no late flourish from a Portsmouth side now destined to be broken up, they said goodbye to the big time in defiant fashion.
.
Soma Zaidi ...

Waziri mkuu wa Thailand aazimia kuendeleza makabiliano dhidi ya waandamanaji.

Watu 22 wauawa katika makabiliano nchini Thailand, 194 wajeruhiwa.


Waziri mkuu wa Thailand, Abhisit Vejjajiva amesema serikali haitarudi nyuma katika jitihada za kukabiliana na waandamanaji aliowataja kama wanaovunja sheria na kuunda makundi ya wapiganaji wanaojaribu kutisha serikali.



Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon ametoa wito wa kusitishwa kwa ghasia katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok huku wanajeshi na waandamanaji wanaoipinga serikali wakiendelea kukabiliana .

Wanaotoa huduma za dharura nchini humo wamesema kuwa idadi ya watu waliouawa imefikia 22 na wengine zaidi ya 194 wamejeruhiwa .

Ban ki Moon amewahimiza viongozi wa serikali na waandamanaji wanaovaa mashati mekundu warejee kwenye mazungumzo.

Vikosi vya wanajeshi vimeshiriki katika makabiliano makali ya siku mbili na waandamanaji ambao walivurumisha mawe na mabomu ya petroli baada ya wanajeshi kuingia katika eneo la kibiashara la Rath-Chap-Rasong.

Wanajeshi hao waliingia katika enelo hilo kwa lengo la kuukomesha mvutano ambao sasa umeingia katika mwezi wa pili baina ya waandamanaji na serikali ya waziri mkuu, Abhisit Vejjajiva.

. Soma Zaidi ...

HAPO VIPI?????????

Soma Zaidi ...

FA Cup - FA Cup final: Facts and figures


FA Cup holders Chelsea are attempting to become the sixth club to perform the FA Cup and League double after clinching the Premier League title on Sunday.

- The Double has been achieved 10 times in the past with Manchester United (1993-94, 1995-96, 1989-99) and Arsenal (1970-71, 1997-98, 2001-02) winning it three times. The only other Doubles have been by Preston North End (1888-89), Aston Villa (1896-97), Tottenham Hotspur (1960-61) and Liverpool (1985-86).

- Chelsea are also attempting the rare feat of winning the FA Cup in successive seasons. Since the competition started in 1871-72, that has only been achieved by Wanderers (1871-72 and 1876-77-78), Blackburn Rovers (1884-85-86 and 1890-91), Newcastle United (1951-52), Tottenham Hotspur (1961-62 and 1981-82) and Arsenal (2002-03).

- Chelsea defender Ashley Cole will become the first player ever to collect six winners medals if the Blues' triumph.

- Arthur Kinnaird and Charles Wollaston both won five winners medals in the 19th century and no player matched them for 118 years until Cole won his fifth medal last season. He won the cup three times with Arsenal (2002, 2003 and 2005) and twice with Chelsea (2007 and 2009).

- An indication of Chelsea's emergence as a major force in recent years is that although this is their 10th FA Cup final appearance since their first losing final in 1915, it is their seventh since 1994 and their third in the last four seasons. They have won the cup five times.

- Portsmouth will be appearing in their fifth FA Cup final. After losing 2-0 to Bolton Wanderers in 1929 and 2-1 to Manchester City in 1934, they won the cup for the first time when they beat Wolverhampton Wanderers 4-1 in 1939. That was their last appearance until their 1-0 win over Cardiff City two years ago.

- Portsmouth are the fifth club to be relegated and appear in the final in the same season after Manchester City (1926), Leicester City (1969), Brighton (1983) and Middlesbrough (1997). All four relegated sides lost.

- Saturday's final is the first between the teams that finished top and bottom of the top flight.

- Chelsea's Stamford Bridge home staged the three finals immediatly before Wembley was built, in 1920, 1921 and 1922. -- Until Harry Redknapp's success with Portsmouth in 2008, no English manager had won the FA Cup since Joe Royle triumphed with Everton in 1995.

- Carlo Ancelotti will become the second Italian to manage an FA Cup winning team if Chelsea are successful, following Gianluca Vialli, who took the Blues to victory in 2000. Avram Grant would be the first Israeli to win the FA Cup, against the club he took to the Champions League final in 2008.

- Chelsea have had the most cosmopolitan collection of FA Cup winning managers of all. Following Englishman Dave Sexton's triumph in 1970, they have won the cup under Ruud Gullit (Netherlands) in 1997, Vialli (Italy) in 2000, Jose Mourinho (Portugal) in 2007 and Guus Hiddink (Netherlands) in 2009.

- Chelsea have an overwhelmingly superior record against Portsmouth over the last seven seasons when Portsmouth have been in the Premier League. Their 14 League matches have ended in 13 wins for Chelsea and one draw with a goal difference of 31-2. Chelsea also won a League Cup tie 4-0 against Portsmouth last season and beat them 5-0 at Fratton Park in their last meeting on March 24.

- The clubs have only played each other three times in FA Cup history with Portsmouth beating Chelsea 1-0 after a 1-1 draw en route to the 1929 final, and Chelsea beating Portsmouth 4-1 en route to winning the final in 1997.

- Only four of the Portsmouth players who started the 2008 final against Cardiff City are still at the club -- goalkeeper David James, defender Hermann Hreidarsson and forwards John Utaka and Nwanko Kanu, who scored the only goal.

- All of Chelsea's winning team from last season are still at Stamford Bridge, although Jose Bosingwa, Michael Essien and John Obi Mikel are out injured for Saturday.

- Chelsea's Peter Osgood in 1970 was the last player to score in every round of the FA Cup from the third round to the final.

- Didier Drogba has a remarkable scoring record for Chelsea at Wembley. He has scored one goal in all five competitive matches Chelsea have played there since the stadium re-opened in 2007.

- He scored the winner in their 1-0 FA Cup final victory over Manchester United in 2007; he scored Chelsea's only goal in their 2-1 defeat to Spurs in the 2008 League Cup final; he scored the winner in their 2-1 semi-final win over Arsenal in 2009; their equaliser in their 2-1 win over Everton in last season's FA Cup final and the opening goal in their 3-0 FA Cup semi-final win over Aston Villa last month.
Soma Zaidi ...

MAFURIKO NCHINI KENYA

Kenya imetoa tahadhari ya mafuriko huku ikitangaza kuwa mabwawa matatu katika mto mrefu kabisa nchini humo, huenda yakafurika katika siku chache zijazo, huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha.

Mabadiliko ya hali ya hewa,imelaumiwa kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi ambayo yameharibu majengo na kusababisha vifo nchini Kenya.

Mkuu wa kitengo cha kukabiliana na maafa nchini Kenya kanali Vicent Anami amesema kua, kumesalia nafasi kidogo tu, kabla ya bwawa la Masinga kuanza kufurika na baadae mabwawa ya Kiambere na Gitaru pia.

Hali hiyo itasababisha mafuriko makubwa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki na Mashariki mwa Kenya. Shirika la Msalaba Mwekundu limesema watu 81 wamepoteza maisha yao katika mafuriko na maporomoko ya ardhi, tangu mwanzo wa mwaka huu.

Msemaji wa shirika hilo, Nelly Muluka, amesema idadi ya watu walioathirika na mafuriko hayo inatarajiwa kuongezeka.

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo la Afrika Mashariki imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi siyo tu nchini Kenya lakini pia Tanzania na Uganda. Soma Zaidi ...

Friday, May 14, 2010

UMOJA WA ULAYA WATUMA UJUMBE BURUNDI

Umoja wa Ulaya unapanga kutuma ujumbe wa watu 82 kusimamia chaguzi nchini Burundi.

Ujumbe huo utasimamia chaguzi za mabaraza ya miji tarehe 21 mwezi hu wa Mei,uchaguzi wa rais Juni 28 mwaka huu na chaguzi za bunge,baraza la Senet na mikoa kati ya Julai 23 na Septemba saba mwaka huu.

Ujumbe huo utakaoongozwa na bibi Renate Weber kutoka bunge la Ulaya utazifuatilia kampeni za uchaguzi na maandalizi ya uchaguzi katika mikoa yote 17 ya nchi hiyo. Soma Zaidi ...

AMTERDAM MAMBO MSETO

Hii ndio hali ya Amtedam Centraal kwa sasa kufuatia mgomo wa wafanyakazi wa manispaa.







Soma Zaidi ...

ICI ANVERS

Jana tulibahatika kutembelea baadhi ya miji ndani ya belgium, na miongoni mwao ulikua ni mji wa Antwerpen a.k.a Anvers

Kituo cha mabasi ambacho kipo karibu na kituo kikuu cha treni Antwerpen
Barabara inayoelekea kwenye kituo kikuu cha treni cha Antwerpe, na barabara za Belgium hali yake ndio kama hii.




Soma Zaidi ...

ALIYENUSURIKA AJALI YA NDEGE APATA NAFUU

Mtoto aliyenusurika kimiujiza katika ajali ya ndege ya Libya iliyouawa watu 103 wakiwemo wazazi wake, inaarifiwa kuwa anaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kutoka hospitali.

Dokta Siddiq ben Dilla wa hospitali kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli amesema kuwa mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka minane anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji katika miguu yake kufuatia ajali hiyo ya Jumapili.Vyombo vya habari vya Uholanzi vimesema kuwa mtoto huyo anaitwa Ruben van Assouw

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi Ozlem Canel , ameliambia shirika la habari la AFP mjini The Hague kuwa mjomba na shangazi wa mtoto huyo wamewasili Tripoli kwa ndege maalum ya serikali.

Abiria 61 waliokuwemo ndani ya dege hiyo chapa A330-200 ambayo imekuwa ikifanya safari zake tangu mwezi Septemba mwaka uliopita, ni raia kutoka Uholanzi. Waziri Mkuu wa Uholanzi, Jan Peter Balkenende amesema ndege hiyo ilikuwa na abiria wengi wa Uholanzi. Nao maafisa wa Libya wamesema abiria wengine 22 walikuwa raia wa Libya, lakini hawajatoa taarifa zaidi kuhusu uraia wa abiria wengine.

Kwa mujibu wa shirika la utangazajai la Uholanzi, mtoto huyo aliweza kuwatambua jamaa zake hao wakati walipoingia hospitali. Soma Zaidi ...

Wednesday, May 12, 2010

NDEGE YA LIBYA YAANGUKA 104 WAUAWA

Watu 104 wameuwawa katika ajali ya ndege ya Shirika la Libya Al-Afriqiyah, leo karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, wakati ikijaribu kutuwa.

Msemaji wa uwanja wa ndege mjini Tripoli alisema ndege hiyo ilikuwa ikiwasili kutoka Afrika kusini.

Chanzo cha ajli bado hakijulikani. Jumuiya ya usafiri na uchukuzi ya Uholanzi imesema miongoni mwa abiria hao 104 waliofariki kiasi ya 61 ni raia wa Uholanzi.

Maafisa nchini Libya wamesema maiti 96 zimepatikana, kutoka katika mabaki ya ndege hiyo.

Kwa mujibu wa maafisa ni mtu mmoja tu aliyenusurika, akiwa ni mtoto wa kiholanzi mwenye umri wa miaka 9. Soma Zaidi ...

CAMERON KUONGOZA SERIKALI MPYA UINGEREZA


Nchini Uingereza,chama cha Conservatives, kimerejea madarakani baada ya miaka 13.Mwenyekiti wa chama hicho cha kihafidhina David Cameron ameteuliwa waziri mkuu baada ya kujiuzulu kwa kiongozi wa chama cha Labour,Gordon Brown.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 43,amesema,lengo lake ni kuunda serikali ya muungano uliokamilika,kati ya Conservatives na Liberal Democrats,kinachoongozwa na Nick Clegg.

Chama cha Consevatives, kilishinda kura na viti vingi, kuliko vyama vingine, katika uchaguzi mkuu uliofanywa Alkhamisi iliyopita,lakini kilishindwa kupata wingi wa kuweza kuunda serikali peke yake. Vyama vya Conservative na Labour, vilikuwa na majadiliano ya kuunda serikali pamoja na Liberal Democrats

Ripoti zinasema, George Osbourne atakuwa waziri mpya wa fedha na kiongozi wa zamani wa chama cha Conservative, William Hague,ataongoza wizara ya mambo ya nje. Nick Clegg atakuwa Naibu Waziri Mkuu na wanachama wenzake wanne watakuwemo katika baraza la mawaziri.

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza,David Cameron, amepongezwa na viongozi wa kimataifa, baada ya kiongozi huyo wa chama cha kihafidhina kupokea madaraka kutoka kwa Gordon Brown wa chama cha Labour.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa amemuambia Cameron ataendelea na uhusiano maalum ulioko kati ya nchi zao na amemualika kiongozi huyo mpya wa Uingereza, kwenda Washington wakati wa majira ya joto. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel vile vile amempongeza Cameron na amemualika kwenda Berlin upesi awezavyo. Taarifa kutoka ofisi ya Cameron imesema, viongozi hao kwa ufupi walijadili hali ya uchumi duniani na ajenda ya pamoja ya nchi za Ulaya.

. Soma Zaidi ...

Tuesday, May 11, 2010

OCAMPO AKUTANA NA WATU WALIOATHIRIKA NA GHASIA ZA UCHAGUZI NCHINI KENYA


Luis Moreno Ocampo amesema jana kuwa amefanya ziara katika eneo linalokumbwa mara kwa mara na uhalifu nchini Kenya la mtaa wa mabanda la Mathare ili kufahamu maoni ya baadhi ya watu walioathirika na ghasia za baada ya uchaguzi, ambazo zimesababisha watu zaidi ya 1,000 kuuwawa. Mtaa wa mabanda wa Mathare unafahamika kwa kiwango chake cha juu cha uhalifu na kusambaa kwa utengenezaji na matumizi ya pombe za kienyeji.

Mwendesha mashtaka amesema anaamini uhalifu dhidi ya ubinadamu umefanyika wakati wa ghasia hizo. Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita waliidhinisha mwezi uliopita kuwa Moreno Ocampo anaweza kuanza kufanya uchunguzi kuhusu suala hilo.

Serikali ya Kenya jana iliahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama hiyo kuhusiana na uchunguzi huo. Tamko hilo limetolewa katika mkutano mjini Geneva baina ya baraza la umoja wa mataifa la haki za binadamu na ujumbe wa serikali ya Kenya ukiongozwa na waziri wa sheria wa Kenya.

Katika muhtasari wa mkutano huo , Kenya imesema itatoa ushirikiano kamili kwa mahakama hiyo ya kimataifa na kutoa uhakikisho wa kuwalinda mashahidi dhidi ya vitisho vya kutaka kuwadhuru.

Ahadi ya kuwalinda mashahidi ambao huenda wakatoa ushahidi imekuja baada ya ombi la kufanya hivyo lililotolewa na Austria, Korea ya kusini, Ireland, Australia , Norway na Ureno. Kenya pia imekubali kuchukua hatua zaidi kuzuwia hali ya kuepuka kuchukuliwa hatua kwa wale waliohusika katika ghasia hizo za baada ya uchaguzi.

Luis Moreno-Ocampo , mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita , ICC, ambayo ni mahakama pekee ya kudumu ambayo ni huru duniani , amekwenda nchini Kenya wiki iliyopita kukutana na watu walioathirka na ghasia zilizosababisha kumwagika damu nchini Kenya.

Akizungumza mjini Nairobi , amesema kuwa ni muhimu kufanya uchunguzi wa uhalifu huu ili kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2012 nchini Kenya unakuwa wa amani. Ameongeza kusema kuwa uchunguzi huo unapaswa kuwa onyo kwa mataifa mengine ya Afrika ambayo yanakaribia kufanya chaguzi.

Ocampo amesema kuwa katika mwaka mmoja na nusu ujao , kutakuwa na karibu chaguzi 15 katika bara la Afrika na wao wanapaswa kuhakikisha kuwa chaguzi hizi zinakuwa za amani. Kenya itatoa ishara kwa nchi zote kwamba ukifanya uhalifu dhidi ya ubinadamu utapelekwa The Hague katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Ethiopia, Rwanda, Burundi, Tanzania na Uganda ni baadhi ya nchi za Afrika ambazo zinatarajia kufanya uchaguzi mnamo muda wa miaka miwili ijayo.

.
Soma Zaidi ...

HISA KATIKA MASOKO ZAPANDA

Hisa katika masoko duniani zimepanda baada ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF kuunda mfuko wa fedha wenye thamani ya Euro bilioni 750 ili kuzuia mzozo wa madeni nchini Ugiriki usisambae katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro.

Soko la hisa la DAX nchini Ujerumani limepata zaidi ya asilimia tano huku masoko ya hisa ya Ugiriki na Uhispania yakipata faida ya asilimia mbili.

Mfuko huo wa kuimarisha sarafu ya Euro umeanzishwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika Brussels usiku wa Jumapili na jana Jumatatu asubuhi. Mfuko huo utatoa msaada kwa kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro zitakazokumbwa na matatizo ya kiuchumi.

Lakini hatua hiyo haina utata kutokana na benki kuu za Ulaya kuanza kununua dhamana za serikali katika soko la wazi, suala ambalo Benki Kuu ya Ulaya-ECB hairuhusiwi kufanya hivyo. Hata hivyo, mkuu wa ECB, Jean-Claude Trichet amepinga ukosoaji kuwa benki hiyo imesalimu amri kutokana na shinikizo la kisiasa.

. Soma Zaidi ...

Monday, May 10, 2010

SARAFU YA EURO KUIMARISHWA

Umoja wa Ulaya pamoja na Shiriki la Fedha la Kimataifa-IMF, zimekubaliana kuanzisha mfuko wa dharura wa kiasi cha dola trilioni moja kwa ajili ya kuyaimarisha masoko ya fedha duniani na kuzuia mgogoro wa madeni wa Ugiriki usihatarishe sarafu ya Euro.

Makubaliano ya kuanzisha mfuko huo wa dharura yamefikiwa kati ya mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya, maafisa wa benki kuu na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, katika mazungumzo ya mwishoni mwa wiki mjini Brussels, Ubelgiji.

Kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno kuwahi kutengwa katika kipindi cha miaka miwili tangu kundi la mataifa 20 yaliyostawi kiviwanda-G20, lilipotoa fedha katika uchumi wa dunia kufuatia kufilisika kwa benki kubwa ya uwekezaji ya Marekani ya Lehman Brothers.
Kiasi hicho cha fedha kimewashangaza wachambuzi wa masuala ya kiuchumi na sarafu ya Euro imepanda karibu asilimia 2 huku masoko ya fedha ya Asia yakiwa thabiti.

Kufuatia tangazo hilo,Marekani na benki kuu za Japan, Ulaya, Uingereza, Canada na Uswisi zimesema zitaingilia kati kuhakikisha hakuna uhaba wa dola katika masoko ya fedha ya Ulaya. Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya fedha na uchumi, Olli Rehn, amewaambia waandishi habari kuwa Umoja wa Ulaya utailinda na kuitetea sarafu ya Euro kwa namna yoyote ile.

Hatua hizo za dharura zina thamani kubwa zaidi kuliko jitihada zozote za awali zilizowahi kuchukuliwa na nchi zote 27 za Umoja wa Ulaya au na kundi la nchi 16 zinazotumia sarafu ya Euro katika kuyatuliza masoko ya fedha.
Tayari Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zimepitisha msaada wa Euro bilioni 100 kwa ajili ya kuipiga jeki Ugiriki, ambayo nakisi ya bajeti yake ilipindukia pato lake la ndani kwa asilimia 13.6 mwaka uliopita.

Fedha hizo , dola trilioni moja zinajumuisha Euro bilioni 440 zitakazotolewa na mataifa ya Umoja wa Ulaya yanayotumia sarafu ya Euro na mkopo mwingine wa Euro 60 utatolewa na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya.
Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya wamesema kuwa Euro bilioni 250 zitatolewa na IMF, hivyo kufanya jumla ya fedha hizo kuwa Euro bilioni 750 ambazo ni sawa na karibu dola trilioni moja. Kufikiwa kwa makubaliano hayo kunatokana na simu zilizopigwa jana Jumapili kati ya Rais Barack Obama wa Marekani, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa.
Hata hivyo, mkurugenzi wa IMF, Dominique Strauss-Kahn hajaelezea mipango yoyote maalum, lakini amesema hatua zote za IMF zitafuata misingi ya nchi na nchi.
Soma Zaidi ...