Wednesday, May 19, 2010

KENYA YAWA NCHI YA TANO KUTIA SAINI MAKUBALIANO

Kenya imetia saini leo mkataba mpya wa kugawana maji ya mto Nile baada ya nchi nne nyingine kufanya hivyo wiki iliyopita.

Ethiopia, Rwanda, Tanzania na Uganda zilitia saini mfumo huo wa ushirikiano katika bonde la mto Nile siku ya Ijumaa licha ya upinzani mkubwa kutoka kwa nchi za Misr na Sudan.

Waziri wa maji nchini Kenya Charity Ngilu amesema kuwa ni jukumu la Misr na Sudan sasa kuingia katika mkataba huo na kukubaliana na mataifa hayo kugawana maji ya mto Nile.

Makubaliano hayo mapya yanachukua nafasi ya mkataba uliotiwa saini mwaka 1959 kati ya Misr na Sudan ambao unatoa udhibiti kwao wa zaidi ya asilimia 90 ya maji ya mto huo.

mataifa ambayo mto huo unapitia yanataka kutekeleza miradi ya mabwawa ya umeme na umwagiliaji kwa kushauriana na Misr na Sudan, lakini bila ya Sudan kuwa na kura ya turufu iliyopewa na mkataba wa enzi za ukoloni na Uingereza mwaka 1929.

.

No comments:

Post a Comment