Friday, May 14, 2010

UMOJA WA ULAYA WATUMA UJUMBE BURUNDI

Umoja wa Ulaya unapanga kutuma ujumbe wa watu 82 kusimamia chaguzi nchini Burundi.

Ujumbe huo utasimamia chaguzi za mabaraza ya miji tarehe 21 mwezi hu wa Mei,uchaguzi wa rais Juni 28 mwaka huu na chaguzi za bunge,baraza la Senet na mikoa kati ya Julai 23 na Septemba saba mwaka huu.

Ujumbe huo utakaoongozwa na bibi Renate Weber kutoka bunge la Ulaya utazifuatilia kampeni za uchaguzi na maandalizi ya uchaguzi katika mikoa yote 17 ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment