Monday, May 24, 2010

BURUNDI WAPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

Wananchi wa Burundi leo wamejitokeza kwa wingi kupiga katika uchaguzi wa serikali za mitaa, ambayo ni awamu ya kwanza kabla ya chaguzi nyingine, ubunge na urais June na Julai mwaka huu.

Uchaguzi huo uliahirishwa mara mbili hapo siku ya Ijumaa kutokana na matatizo ya kutokuwepo kadi na maboxi ya kuhifadhia kura. Hali hiyo, hali hiyo ilisababisha kuongezeka wasi wasi iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki. Hata hivyo, tume ya uchaguzi nchini Burundi imewahakikishia wananchi kwamba uchaguzi huo hakutakuwa na tatizo lolote.

Renate Weber, ambaye ni kiongozi wa waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya, alithibitisha kuwa idadi ya watu waliojitokeza ilikuwa kubwa.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema leo asubuhi, ambapo kiasi cha watu millioni 3.5 wenye haki ya kupiga kura wanatarajiwa kuwachagua madiwani wa serikali za mitaa. Uchaguzi huo ni kipimo muhimu kwa uchaguzi wa wabunge na ule wa rais.


No comments:

Post a Comment