Monday, May 24, 2010

MASAUNI MASHAKANI

Jeshi la polisi nchini limesema linafanya uchunguzi wa nyaraka na vielelezo kuhusu umri wa mwenyekiti wa zamani wa jumuiya ya vijana ya chama cha mapinduzi UV-CCM, Hamad Masauni.

Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja baada ya Masauni kudaiwa kuhushi umri wake wakati wa kugombea wadhifa huo mwaka 2008.

Naibu kamishna wa jeshi la polisi anaekaimu ukurugenzi wa makosa ya jinai Piter Kibuyo amesema taarifa za vielelezo vya uchunguzi vitatolewa baada ya uchunguzi huo kukamilika.

Amesema katiba ya nchi inaeleza hakuna mtu alieko juu ya sheria hivyo iwapo Masauni ataonekana amehushi umri wake sheria itachukua mkondo wake

Masauni alitarajiwa kupokelewa leo kwa mapokezi ya aina yake, lakini umoja wa vijana wa UV-CCM, Zanzibar umesema hauhusiki na mapokezi hayo.

Uchunguzi uliofanywa na ndani ya Zanzibar umegundua kua mapokezi hayo yaliandaliwa na baadhi ya vijana wa CCM kutoka jimbo la uchaguzi analoishi Masauni.
.

No comments:

Post a Comment