Friday, May 14, 2010

ALIYENUSURIKA AJALI YA NDEGE APATA NAFUU

Mtoto aliyenusurika kimiujiza katika ajali ya ndege ya Libya iliyouawa watu 103 wakiwemo wazazi wake, inaarifiwa kuwa anaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kutoka hospitali.

Dokta Siddiq ben Dilla wa hospitali kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli amesema kuwa mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka minane anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji katika miguu yake kufuatia ajali hiyo ya Jumapili.Vyombo vya habari vya Uholanzi vimesema kuwa mtoto huyo anaitwa Ruben van Assouw

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi Ozlem Canel , ameliambia shirika la habari la AFP mjini The Hague kuwa mjomba na shangazi wa mtoto huyo wamewasili Tripoli kwa ndege maalum ya serikali.

Abiria 61 waliokuwemo ndani ya dege hiyo chapa A330-200 ambayo imekuwa ikifanya safari zake tangu mwezi Septemba mwaka uliopita, ni raia kutoka Uholanzi. Waziri Mkuu wa Uholanzi, Jan Peter Balkenende amesema ndege hiyo ilikuwa na abiria wengi wa Uholanzi. Nao maafisa wa Libya wamesema abiria wengine 22 walikuwa raia wa Libya, lakini hawajatoa taarifa zaidi kuhusu uraia wa abiria wengine.

Kwa mujibu wa shirika la utangazajai la Uholanzi, mtoto huyo aliweza kuwatambua jamaa zake hao wakati walipoingia hospitali.

No comments:

Post a Comment