Tuesday, May 11, 2010

HISA KATIKA MASOKO ZAPANDA

Hisa katika masoko duniani zimepanda baada ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF kuunda mfuko wa fedha wenye thamani ya Euro bilioni 750 ili kuzuia mzozo wa madeni nchini Ugiriki usisambae katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro.

Soko la hisa la DAX nchini Ujerumani limepata zaidi ya asilimia tano huku masoko ya hisa ya Ugiriki na Uhispania yakipata faida ya asilimia mbili.

Mfuko huo wa kuimarisha sarafu ya Euro umeanzishwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika Brussels usiku wa Jumapili na jana Jumatatu asubuhi. Mfuko huo utatoa msaada kwa kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro zitakazokumbwa na matatizo ya kiuchumi.

Lakini hatua hiyo haina utata kutokana na benki kuu za Ulaya kuanza kununua dhamana za serikali katika soko la wazi, suala ambalo Benki Kuu ya Ulaya-ECB hairuhusiwi kufanya hivyo. Hata hivyo, mkuu wa ECB, Jean-Claude Trichet amepinga ukosoaji kuwa benki hiyo imesalimu amri kutokana na shinikizo la kisiasa.

.

No comments:

Post a Comment