Wednesday, May 12, 2010

NDEGE YA LIBYA YAANGUKA 104 WAUAWA

Watu 104 wameuwawa katika ajali ya ndege ya Shirika la Libya Al-Afriqiyah, leo karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, wakati ikijaribu kutuwa.

Msemaji wa uwanja wa ndege mjini Tripoli alisema ndege hiyo ilikuwa ikiwasili kutoka Afrika kusini.

Chanzo cha ajli bado hakijulikani. Jumuiya ya usafiri na uchukuzi ya Uholanzi imesema miongoni mwa abiria hao 104 waliofariki kiasi ya 61 ni raia wa Uholanzi.

Maafisa nchini Libya wamesema maiti 96 zimepatikana, kutoka katika mabaki ya ndege hiyo.

Kwa mujibu wa maafisa ni mtu mmoja tu aliyenusurika, akiwa ni mtoto wa kiholanzi mwenye umri wa miaka 9.

No comments:

Post a Comment