Baraza la biashara Zanzibar limesema suala ya wafanyabiashara wa Zanziar kutozwa kodi mara mbili Tanzania bara linaweza kuathiri shughuli zao mara baada ya kuanza kwa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika mashariki Julai mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari katibu mtendaji wa baraza hilo Ali Vuai amesema licha baraza hilo kuyapatia ufumbuzi zaidi ya matatizo 60 yanayowakwamisha wafanyabiashara wa Zanzibar, lakini suala hilo haliko mikonini kwa Zanzibar.
Hata hivyo amesema suala hilo linaendelea kujadiliwa katika vikao vya kero za muungano vinavyohusisha mawaziri wa pande mbili za muungano chini ya mwenyekiti wake makamo wa rais wa Tanzania.
Aidha Vuai amesema katika kuwatayarisha wafanya biashara wa Zanziar kuingia katika soko la pamoja la jumuiya ya Afrika mashariki Jumanne ijayo litaendesha mkutano utakao wajumuisha zaidi ya wajumbe 300 kutoka ndani na nje ya Zanzibar.
Amesema lengo la mkutano huo ni kuwaemisha wafanyabiashara wa Zanzibar juu ya umuhimu wa kulitumia soko hilo pamoja na kuyapatia ufumbuzi matatizo yao watakayokabiliana nayo katika soko hilo.
Nae mkurugenzi wa Idara ya biashara Zanzibar Rashid Ali akizungumzia suala la misamaha katika soko hilo amesema misamaha ya bidhaa haitaombewa kwa mtu mmoa bali itaombewa kwa wafanyabiashara wote watakaoingiza bidha zinazoombewa msamaha.
No comments:
Post a Comment