Thursday, May 20, 2010

MKUTANO WA MSUKOSUKO WA FEDHA ULIMWENGUNI BERLIN

Berlin , mji mkuu wa Ujerumani,wiki hii , ni shina la harakati za kuutatua msukosuko wa fedha ulimwenguni:Bunge la Ujerumani-Bundestag, likijadiliana juu ya mikopo kwa nchi za Umoja wa Ulaya, zilizokumbwa na shida za madeni.Wakati huo huo, wabunge wanavutana kuhusu fedha zitoke wapi za kupambana na msukosuko kama huu ukizuka tena . Isitoshe, inazungumzwa vipi , masoko ya fedha nayo yachangie kukabiliana na gharama za msukosuko huo.Hapo, kuna maafikiano lakini, tofauti zinazuka ni kwa aina gani ?

Nia ya kuyawekea vikwazo vikali vya kisheria masoko ya hisa, aliitangaza Rais Barck Obama wa Marekani, hapo Septemba, mwaka uliopita wakati wa mkutano wa kilele wa kundi la mataifa tajiri 20-(G-20) huko Pittsburgh,Marekani.Lakini, maneno yake hayakufuatia vitendo.Kwani, kuna masilhai tofauti kati ya nchi za kiviwanda na zinazoinukia na hivyo,jinsi ya kupitisha sheria hizo kuna misimamo tofauti.Miongoni mwa wale ambao hawataki tena kutumbua macho tu hali hii ikiendelea, ni waziri wa fedha wa Ujerumani Bw. Wolfgang Schäuble.Alisema katika Bunge la Ujerumani :

"Nime fadhahishwa mno na jinsi Jumuiya ya ya Kimataifa, inavyokabiliana na msukosuko huu wa fedha na wa mabenki.Ndio, kuna baadhi ya mambo yamepatiwa ufumbuzi tena haraka mno kuliko ilivyotazamiwa,lakini, bado hatahivyo, mambo yanakwenda pole pole mno.Kuna wakati mtu anahisi kuwa kasi imepungua."

Mapema Februari, mwaka huu, Bw.Schäuble,alisema juhuidi za kutunga sheria bora za kuyadhibiti masoko ya fedha, zisiache kutiliwa kasi hata ikiwa athari mbaya za msukosuko huu wa uchumi zimedhibitiwa.Akawaambia mawaziri wenzake wa fedha kutoka nchi 7 tajiri za kiviwanda (G-7) kuwa anapanga kandoni mwa mkutano wa kilele wa nchi tajiri-20,mwezi ujao wa Juni, nchini Kanada, kuitisha kikao cha maandalio kitakacho wajumuisha Viongozi wa Benki -Kuu,Idaraza za usimamizi wa shughuli za mabenki , Taasisi za fedha za Kimataifa na wataalamu wa sayansi za kiuchumi.

Ni mkutano ambao sasa unachukua sura nyengine kabisa .Msukosuko wa Mabenki na kuzorota kwa uchumi, umefuatiwa sasa na msukosuko wa madeni ya serikali.Ugiriki imefilisika kope si zake na nchi nyengine zanachama wa UU, zinaweza kufuata mkondo huo wa Ugiriki.Thamani ya sarafu ya Euro inaanguka.

Waziri wa fedha wa Ujerumani, anasema kwahivyo, yawapasa kuilinda sarafu yao ya pamoja ya Euro.Hivi sasa imezuka hali ya kuiingiliwa sarafu hiyo na hali katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa kadiri ambayo wakati wa kuasisiwa kwa Umoja wa sarafu ya ulaya (Euro) hakuna alietazamia...

Kutokana na shinikizo la kuzidi kwa msukosuko wa sarafu ya Euro, yabainika mengi ghafula sasa yanawezekana .Kwa mshangao wa wengi, juzi Jumaane, hatua ambazo hazikupata wingi wa kura kuzipitisha na serikali ya muungano wa vyama-tawala vya CDU-CSU na FDP, zilipitishwa.

Nae Kanzela Angela Merkel akasema: "Katika sekta ambayo Ujerumani kwa kujiamulia mambo pekee hakutailetea dhara, tutajiamulia wenyewe ; na tulioyapituisha, yatabakia kufanya kazi hadi sheria kwa Umoja wa Ulaya nzima , zimepitishwa."
.

No comments:

Post a Comment