Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislam wa Somalia wamekishambulia kijiji kimoja kilichoko katika mpaka wa nchi hiyo na Kenya. Wakaazi saba wa kijiji hicho cha Dadajabula kilicho Kenya walijeruhiwa.
Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mashahriki huko Kenya. James Ole Serian, amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa wanahisi washambuliaji hao ni wapiganaji wa kundi la al Shaabab.
Wiki iliyopita msemaji wa al Shaabab, Ali Mohammed Rage, aliionya Kenya kutojiingiza katika mzozo wa Somalia. Serikali ya mpito nchini Somalia imekuwa katika mkakati wa kufanya mashambulio makubwa dhidi ya waasi hao wa al Shaabab ambao wanailaumu Kenya kwa kushiriki katika mkakati huo.
.
No comments:
Post a Comment