Sunday, January 31, 2010

WASHIKA BUNDUKI WASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI KWAO DHIDI YA MASHETANI WEKUNDU

Timu ya soka ya Arsenal leo hii walishindwa kufurukuta mbele ya Man Utd katika uwanja wao wa Emirates Stadium kwa kuchukua kipigo cha magoli matatu kwa koja.

Man Utd waliandika bao la kwanza kupitia kwa winga wake wa kulia Nani baada ya kupiga krosi iliyomfanya mlinda mlango wa Arsenal Almunia kuukwamisha mpira nyavuni, bao la pili la Man Utd lilipachikwa nyavuniu na Rooney ambapo lile la tatu lilifungwa na Park.Goli la kufutia machozi kwa upande wa Arsenal limefungwa na Vermaelen.

Kwa matokeo hayo Man Utd bado wanaendelea kushikilia nafasi ya pili kwa kuwa na alama 53, na Arsenal wamebaki nafasi ya tatu kwa alama 49 huku usukani wa ligi hio bado unashikiliwa na Chelsea wakiwa na alama 54.

Kabla ya mechi hio kulikua na mechi kati ya Man City na Portmouth ambapo City walishinda 2-0

Kwa upande wa Kombe la mataifa Afrika limemalizika leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ghana na Egypt na Egypt kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli moja kwa zero na kuwafanya Egypt kuweza kutetea ubingwa wao. Soma Zaidi ...

NI BARAFU KWENDA MBELE

Hii barafu ya mara hii kwa kweli haitabiriki kwa sababu haishi
Soma Zaidi ...

MUHOGO - ZANZIBAR

Soma Zaidi ...

Saturday, January 30, 2010

MATOKEO YA BAADHI YA MECHI ZA LEO

Timu ya Chelsea imejiongezea alama zaidi kileleni mwa ligi kuu Uingereza baada ya kuwachapa Burnley magoli mawili kwa moja katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Turf Moor huko Burnley,kwa upande wa Chelsea magoli yalifungwa na Anelka goli la mwanzo na lile la pili liliwekwa nyavuni na nahodha Terry.

Chelsea wanashikilia usukani wa Premier League wakiwa na alama 54 kwa kucheza mechi 23 wakifuatiwa na Man Utd, nafasi ya pili kwa alama 50 huku wakiwa tayari wameshacheza mechi 23, na nafasi ya tatu wapo washika bunduki Arsenal wakiwa na alama 49 kwa kucheza mechi 23.

Msimamo huu wa ligi unaweza kubadilika kulingana na matokeo ya mchezo wa kesho kati ya Arsenal na Man Utd mechi ambayo itachezwa Emirates Stadium

Premier League
Burnley1 - 2Chelsea
Birmingham City1 - 1Tottenham Hotspur
Fulham0 - 2Aston Villa
Hull City2 - 2Wolverhampton Wanderers
Liverpool2 - 0Bolton Wanderers
West Ham United0 - 0Blackburn Rovers
Wigan Athletic0 - 1Everton

African Cup of Nations
Nigeria1 - 0Algeria

La Liga
RCD Espanyol1 - 0Athletic Bilbao

Serie A
Bari4 - 2Palermo

Bundesliga
Schalke 042 - 0Hoffenheim
Borussia Mönchengladbach4 - 3Werder Bremen
Eintracht Frankfurt1 - 21. FC Köln
Hertha BSC0 - 0VfL Bochum
Bayern München3 - 0FSV Mainz 05
Hannover 961 - 31. FC Nürnberg

Soma Zaidi ...

HONGERA ZANZIBAR NA WAZANZIBARI

MUWAZA (MUSTAKBALA WA ZANZIBAR) UNATOA PONGEZI ZA DHATI KWA :

RAIS AMAN ABEID KARUME NA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KWA UJASIRI NA USHUJAA WAO ULIOJITOKEZA KATIKA KULETA KUUNGANA KWA WAZANZIBARI, KUONDOSHA UHASAMA, CHUKI, MIFARAKANO ISIOKWISHA NA UADUI USIO NA MAANA.

TUNAWAPONGEZA KWA KUTULETEA ZANZIBAR ISHARA NJEMA INAYOLETA MATUMAINI YA SALAMA NA AMANI NA KULETA MATARAJIO YA SIASA ZA KIDEMOKRASIA NA KUJENGA MISINGI YA MAENDELEO

TUNAMPONGEZA MAKAMO WA RAIS WA MUUNGANO MH. ALI MUHAMMED SHEIN NA MH. MOHAMMED GHARIB BILAL KWA KUCHUKUA JUKUMU LA KUWAHAMASISHA WANA CCM KATIKA KIKAO MAALUUM CHA NEC ZANZIBAR

TUNAMPONGEZA KIONGOZI WA UPINZANI MH. ABUBAKAR KHAMIS BAKARI KWA MAPENDEKEZO YA KHERI ALIYOYAWAKILISHA KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI

VILE VILE TUNALIPONGEZA BARAZA LA WAWALIKILISHI ZIMA KWA DHAMANA, HAMASA NA HISIA ZA KIZANZIBARI KWA UPEO WAO WA KUYAKUBALI NA KUYASHINDIKIZA MABADILIKO YA KIHISTORIA YANAYOLINDA MUSTALBAL WA ZANZIBAR

TUNAWAPONGEZA WAZANZIBARI WOTE WALIOJITOKEZA HADHARANI NA WASIOJITOKEZA ULIMWENGUNI KOTE KWA KUWA NA IMANI NA VIONGOZI WAO PAMOJA NA KUWAOMBA WAONYESHE UZANZIBARI WAO WA DHATI KWA KUSAIDIA VIONGOZI WAO NA NCHI YAO YA ZANZIBAR KWA KUCHUKUA MAJUKUMU YA KILA AINA NDANI NA NJE YA ZANZIBAR KULETA MAENDELEO YA KUDUMU ZANZIBARI

TUNAWAOMBA VIONGOZI WAKIWEMO RAIS AMANI ABEID KARUME, MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD, WAWAKILISHI, WABUNGE WA KIZANZIBARI NA WAZANZIBARI WOTE KWA JUMLA WASIMAME KIDETE NA IMARA KULINDA MUSTAKBAL WA ZANZIBAR NA KUJILINDA NA FITINA NA MAFATANI WANAOTAKA KUIANGAMIZA ZANZIBAR

ZANZIBAR IMEWEKA HISTORIA YA KUIGWA AFRIKA NA ULIMWENGUNI KOTE NA KUWEKA MFANO WA VIPI MIZOZANO YA KISIASA INAWEZA KUTATULIWA KWA SALAMA NA AMANI – HAYA NI YAKUIGWA ULIMWENGUNI KOTE

YA RABBI MOLA WABARIKI MILELELE VIONGOZI WEMA WA ZANZIBAR, WAZANZIBARI NA NCHI YA ZANZIBAR

KWA NIABA MUWAZA

Dr. Yussuf S. Salim Soma Zaidi ...

SERENA WILLIAMS BINGWA TENA AUSTRALIAN OPEN

Mcheza tenis namba moja duniani Serena Williams(USA) leo hii ameweza kutetea ubingwa wake katika mashindano ya Australian open baada ya kumfunga Justine Henin ( BEL) kwa 6-4, 3-6, 6-2, katika mchezo uliodumu kwa masaa mawili na dakika saba.
Serena Williams anakua mchezaji wa kwanza kuweza kutetea ubingwa wake huko Melborne tangu pale Jennifer Capriati(USA) alipotwaa ubingwa mara mbili mfululizo mwaka 2001 na 2002, Capriati alimshinda Martina Hingis(SUI) mara zote mbili.

Hii itakua ni mara ya tano kwa Serena Williams kutwaa kombe la Australian Open Baada ya kuchukua 2003, 2005, 2007, 2009.
Soma Zaidi ...

HATUNA MUDA


Soma Zaidi ...

MWENYE WIVU AJINYONGE


Soma Zaidi ...

MECHI ZA LEO

Premier League
16:00 Birmingham City v Tottenham Hotspur
16:00 Fulham v Aston Villa
16:00 Hull City v Wolverhampton Wanderers
16:00 Liverpool v Bolton Wanderers
16:00 West Ham United v Blackburn Rovers
16:00 Wigan Athletic v Everton
18:30 Burnley v Chelsea

African Cup of Nations
17:00 Nigeria v Algeria

La Liga
18:00 RCD Espanyol v Athletic Bilbao
20:00 Sporting Gijón v FC Barcelona
22:00 Deportivo La Coruña v Real Madrid

Serie A
18:00 Bari v Palermo
20:45 Napoli v Genoa

Bundesliga
15:30 Borussia Mönchengladbach v Werder Bremen
15:30 Eintracht Frankfurt v 1. FC Köln
15:30 Hertha BSC v VfL Bochum
15:30 Bayern München v FSV Mainz 05
15:30 Hannover 96 v 1. FC Nürnberg
18:30 Schalke 04 v Hoffenheim

Dutch Eredivisie
18:45 NEC v Sparta Rotterdam
19:45 AZ Alkmaar v FC Groningen
19:45 NAC Breda v VVV-Venlo
20:45 ADO Den Haag v sc Heerenveen

NB: Ratiba hii ni kwa (CET)
Soma Zaidi ...

COCAINE YAMPANDISHA MAHAKANI MKE WA WAZIRI

Mke wa waziri wa masuala ya kijasusi wa Afrika Kusini amekamatwa kwa madai ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

Sheryl Cwele, mwenye umri wa miaka 50, mke wa Siyabonga Cwele, amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa jaribio la kuingiza cocaine nchini Afrika Kusini.

Bi Cwele ameshtakiwa kwa kumtumia mwanamke mmoja kuchukua dawa hizo Uturuki na kumwajiri mwanamke mwengine kuzichukua kutoka Brazil.

Amewekwa rumande mpaka dhamana yake itakaposikilizwa katika wiki moja ijayo.

Bi Cwele anakabiliwa na shutuma hizo pamoja na Frank Nabolis, raia wa Nigeria aliyekamatwa Afrika Kusini mwezi Desemba. Soma Zaidi ...

MELI ZANZIBAR ILIZAMA KWA UZEMBE

Hatimae ripoti ya kuzama kwa meli ya LCT Fatih, iliyosababisha vifo vya watu sita katika Bandari ya Malindi imetangazwa na serikali na kuelezwa ajali hiyo imetokana na uzembe wa nahodha wake Ussi.

Akisoma ripoti ya uchunguzi huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mawasilano na Uchukuzi, Machano Othman Said, alisema meli hiyo ilikuwa inaingiza maji kupitia mlango wa mbele na baadaye ilizama baada ya kuelemewa na kiwango kikubwa cha maji na tani 55 za mizigo zilizokuwamo ndani ya meli.

Akiwasilisha ripoti hiyo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi alisema sehemu ya chini ya meli hiyo pia iligundulika ilikuwa na matobo yaliyokuwa yakiingiza maji na kuwa chimbuko la kuzama kwa meli hiyo.

“Mheshimiwa Spika, meli ilikuwa haina mfumo wa kuingiza maji katika matangi yake kutokana na mabadiliko ya muundo yaliyofanywa huko nyuma nchini Madagascar,” alisema.

Waziri Machano alisema wakati meli ikiwa katika hatari ya kuzama Nahodha wa meli hiyo kapteni Ussi hakuchukua hatua yoyote ya kuomba msaaada kupitia mamlaka za uokozi.

“Nahodha achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kushitakiwa kwa kusababisha ajali na kupoteza maisha ya watu na mali zao,” alisema Waziri Machano.

Waziri Machano alisema kwamba ukaguzi wa meli hiyo pia unaonyesha kuwepo udanganyifu mkubwa kwa kampuni iliyopewa kazi ya kuikagua meli hiyo na itachukuliwa hatua ya kutozwa faini kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha, meli hiyo imegundulika ilikuwa ikifanya kazi huku ikiwa ina vyeti batili, vilivyotolewa na watendaji wa Ofisi ya Mrajisi wa Meli Zanzibar.

Bodi hiyo ya uchunguzi iliongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Omar Makungu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa. Wajumbe ni Kapteni Alhaji Sururu, Mwandisi Abdi Omar Maalim, Abdallah Kombo, Kapteni Mohammed Juma na Kapteni Wilium Mlesa. Soma Zaidi ...

Friday, January 29, 2010

SOKO LA ALHAMIS ALMELO

Soko kama hili nakumbuka tulikua nalo enzi za Rais Komandoo na lilikua ni la jumapili (Sunday Market) pale maeneo ya Msikiti Mabuluu na kwa kweli lilikua likisaidia wananchi kutokana na bidhaa zake kuuzwa rahisi, lakini sijui soko lile limekwendea wapi.
Soma Zaidi ...

Thursday, January 28, 2010

MATOKEO YA MECHI ZA LEO

Mafarao wafanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuwatundika Algeria magoli 4-0, katika mchezo huo wachezaji 3 wa timu ya Algeria wamepewa kadi nyekundu akiwemo mlinda mlango wao

Katika mechi ya mwazo Ghana walicheza dhidi ya Nigeria na Ghana walishinda kwa bao 1-0, mafarao watacheza Fainali dhidi ya Ghana siku ya jumapili wakati jumamosi Algeria wataminyana na Nigeria



Matokeo ya mechi nyengine za leo ni kama ifuatavyo:

Copa del Rey
Getafe CF 0 - 1 RCD Mallorca

Coppa Italia
Internazionale 2 - 1 Juventus
Soma Zaidi ...

UNAPO FATANA NA MPENZI WAKO PAMOJA RAFIKI FISI


Soma Zaidi ...

JE NA WAO WANATAMANI WAWE NA BARABARA KAMA ZETU?

Soma Zaidi ...

Wednesday, January 27, 2010

MAN UNITED WAPAA FAINALI CARLING CUP

Mashetani wekundu watinga fainali ya Carling Cup kwa kuwachabanga Manchester City katika mechi ya pili ya nusu fainali kwa mabao 3-1, mechi iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford.

Magoli ya mashetani wekundu yalifungwa na Paul Scholes la kwanza, Michael Carrick la pili, na lile la tatu limefungwa na Wayne Rooney na goli la kufutia machozi la City liliwekwa yavuni na Teves.

Man United watakutana na Aston Villa katika mechi ya fainali siku ya tarehe 28 Febuary katika uwanja wa Wembley.

Matokeo mengine ya mechi za leo ni kama ifuatavyo:

Premier League
Blackburn Rovers 2 - 1 Wigan Athletic
Everton 2 - 0 Sunderland
Aston Villa 0 - 0 Arsenal
Chelsea 3 - 0 Birmingham City

Coppa Italia
AC Milan 0 - 1 Udinese
Soma Zaidi ...

TAMKO LA MUWAZA KUHUSU MARIDHIANO NA MUSTAKBAL WA ZANZIBAR

MUWAZA inalaani vikali njama za viongozi wa Bara na vitimbakwiri vyake kutaka kuridisha uhasama baina ya Wazanzibari baada ya Wazanzibari kufikia hatua ya Maridhiano

MUWAZA inalaani kuingiliwa kati na Viongozi wa Bara katika maamuzi ya Wazanzibari

MUWAZA inalaani kudharau kwa Viongozi wa Bara maamuzi ya Rais na serikali ya Zanzibar na kufanya njama ya kutaka kuyaweka kando maamuzi ya Rais

MUWAZA inalaani kutaka kutayarisha mbinu za kuingilia kati maamuzi ya Baraza la Wawakilishi

MUWAZA inalaani njama za Bara kwa lengo la kuchelewesha kwa makusudi na kukwamisha kwa makusudi kutekelezwa kwa MUAFAKA wa tatu

MUWAZA inalaani kauli za Makamba, Msekwa na Chilingati za kuwaamulia Wazanzibari kuhusu Maridhiano yao na Mustakbal wao

MUWAZA inawalaani Vibaraka na Vitimbakwiri wanaotaka kuiangamiza Zanzibar kwa maslahi yao binafsi

MUWAZA inasisitiza tena kwamba Uchaguzi uahirishwe

MUWAZA unaunga mkono MAAMUZI YA BARAZA LA WAWAKILISHI yatoshe kuwa kama kura ya maoni ya Wazanzibari

MUWAZA inapendekeza kuundwe Serikali ya mpito kabla ya Uchaguzi ili kuyashughulikia maridhiano na kutengeneza misingi bora ya Uchaguzi

MUWAZA inalishauri Baraza la Wawakilishi lihakikishe kwamba Maslahi ya Zanzibar na Mustakbal wake wanayaweke mbele na :

1 Lirekibishe Katiba ili kuunda serikali ya mpito

2 Lirekibishe Katiba ili kulinda na kuendeleza mbinu za Maridhiano

3 Lirekibishe Katiba irekibishwe ili Katiba ya Muungano ipitiwe upya na hatimae ikibidi iundwe Katiba mpya ya Muungano

MUWAZA inawanasihi Wawakilishi wahakikishe kwamba:

I Mamlaka ya Zanzibar yanabaki katika mikono ya Zanzibar

II Wadhifa wa Waziri Kiongozi ubadilishwe na badala yake uwe wa Waziri Mkuu

III Rais wa Zanzibar awe moja kwa moja Makamu wa Rais wa Tanzania

IV Urais wa Tanzania uwe wa zamu baina ya Tanganyika na Zanzibar

V Baraza la Mawaziri la Zanzibar liwe sawa na Baraza la Mawaziri jengine lolote Ulimwenguni

VI Baraza la Wawakilishi liwe na nguvu sawa na Bunge lolote Ulimwnguni

VII Mungano uwe wa Serikali Tatu

MUWAZA inampogeza Rais Amani Abeid Karume kwa kuheshimu Katiba ya leo na kutotaka kuongeza muda wake wa Urais chini ya Katiba leo

MUWAZA inampongeza Maalim Seif Shariff Hamad kwa kutokuwa na uroho wa Madaraka na kuwa tayari kumuachia Rais Amani kundelea madarakani ikibidi.

Mungu Ibariki Zanzibar – Amiin !!! Soma Zaidi ...

KICK BOXING BADO NI MARUFUKU ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza msimamo wake wa kutoruhusu mchezo wa ngumi za mateke (kick boxing) katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Naibu Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Mahmoud Thabit Kombo amewambia wajumbe wa Baraaza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar kwamba Serikali haijaruhusu mchezo huo hapa nchini .

Mwakilishi wa Jimbo la Chambani (CUF) Abass Juma Muhunzi alisema kwa kuwa vijana wa Zanzibar sasa wanashiriki katika mashindano ya judo na ngumi za mateke ( kick boxing ) ambayo hayana tafauti sana na mchezo wa ngumi za kawaida (boxing ) ni kusema sasa mchezo wa ngumi unaruhusiwa kuchezwa Zanzibar.

Waziri Kombo alisema ipo tafauti kubwa kati ya mchezo wa judo na mchezo wa ngumi kwa kuwa katika mchezo wa judo wachezaji hawapigani ngumi wala mateke isipokuwa wanaoneshana nguvu na mbinu katika kukamatana na kuangushana kwenye kiwanja kilichowekwa maalum matandiko malum ya kuangukia

Mwakilishi wa nafasi za Wawanawake (CUF) Zakia Omar Juma alisema kwa kuwa mchezo wa ngumi za mateke ulipigwa marufuku na mzee Karume ili kulinda wananchi wasipigane kwa wakati huo kwa nini hivi sasa bado suala hilo linaekewa pingamizi na serikali hali ya kuwa baadhi ya Wazanzibar wanashiriki mchezo huo nje ya nchi na kushinda

Naibu Waziri huyo alisema suala la kukatazwa ngumi za mateke lilipingwa marufuku na muasisi wa kwanza wa Taifa la Zanzibar ambaye ni rais wa kwanza wa visiwa hivi marehemu mzee Abeid Amani Karume hivyo marufuku hiyo kwa sasa haiwezi kuondolewa hadi hapo ionekane kuna haja hiyo

Kombo alisema Wazanzibari wanaokwenda kushiriki mchezo huo nje ya nchi hawakatazwi wala hawawezi kuingiliwa uhuruwao huo lakini Serikali haiwasindikizi wanapokwenda katika mashindano wala kuwapokea rasmi kwa kuwa mchezo huo bado ni marufuku kwa Zanzibar.

Hata hivyo alisema iwapo wananchi watataka kuondosha marufuku hiyo ni suala la wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuleta mswada Barazani juu ya suala hilo na wajumbe kwa mamlaka waliyopewa wanaweza wakachangia na wakitaka sheria kufanyiwa marekebisho na haja ya kuuondosha kama itawezekana kufanyika hivyo. Soma Zaidi ...

Tuesday, January 26, 2010

MAREHEMU SWETU FUNDIKIRA AMEZIKWA MAKABURI YA KISUTU

Umati mkubwa wa watu walihudhuria maziko katika makaburi ya kisutu leo jioni.
Watu waliohudhuria mazishi katika makaburi ya kisutu wakipepea kitambaa juu ya kaburi alilolazwa marehemu Swetu.
Sehemu ya wanaume ndugu na jamaa waliohudhuria maziko wakipata chakula nyumbani kwa mzee Fundikira

Sehemu ya wanawake ndugu na jamaa waliohudhuria katika msiba wa marehemu Swetu fundikira aliefariki dunia kwa kupigwa na wanajeshi, marehemu amezikwa leo jioni mnamo majira ya saa 10 jioni kwa saa za Arfika Mashariki.
Soma Zaidi ...

KARUME ALIPOTEMBELEA BANDARI YA MALINDI

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi mh. Amani Abeid Karume akipata maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe wakati alipofika bandarini hapo ili kukagua maendeleo ya ujenzi unaoendelea bandarini hapo.
Rais wa Zanzibr na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi akizungumza na mafundi wanaoshuhulikia ujenzi wa sehemu ya kuwekea makontena katika bandari ya Malindi iliopo mjini Unguja, ujenzi huo unesimamiwa na shirika la bandari la Zanzibar.
Soma Zaidi ...

HABARI NDO HIO

Soma Zaidi ...

BANDARI KUU YA MALINDI


Soma Zaidi ...

KUIJENGA UPYA HAITI


Itachukua muongo mmoja kukarabati nchi ya Haiti ambapo kulitokea uharibifu mkubwa uliosababishwa na tetemeko la ardhi.
Hiyo ni kauli ya waziri mkuu wa Canada Stephen Herper wakati kongamano la siku moja la wafadhili wa kimataifa mjini Montreal kujadili mustakabhali wa kisiwa hicho.

Akizungumza baada ya kongamano hilo kumalizika waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema wafadhili hawapaswi kuwaachia wananchi wa Haiti jukumu la kuijenga upya nchi yao.

Naye waziri mkuu wa Haiti Jean Max Belerieve amewakumbusha wafadhili kuhusu mahitaji muhimu ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na vitanda laki mbili na huduma za afya na matibabu kwa takriban watu laki nne.

Mkasa wa tetemeko la ardhi lenye kipimo cha saba kwenye vipimo vya Richer ulisababisha vifo vya takriban watu laki mbili na kuiacha Haiti mojawapo wa nchi masikini kabisa duniani ikikabiliana na uharibifu wa kiwango cha juu.

Kongamano kuu la wafadhili litafanyika mwezi Machi nchini Marekani ili kujadili zaidi mstakabhali wa Haiti. Soma Zaidi ...

Monday, January 25, 2010

NIGERIA WATINGA NUSU FAINALI KWA NJIA YA MATUTA

Timu ya taifa ya Ngeria imeingia nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuitoa timu ya Zambia kwa njia ya matuta baada ya kumaliza kwa dakika 120 bila ya timu hizo kufungana, katika mapigo hayo ya matuta timu ya Zambia walikosa moja na wanaigeria walipata zote.

Kabla ya mtanange huo kulikua na mechi kati ya Cameroon na Egypt ambapo Cameroon walibugizwa mabao 3-1 na kutolewa.


Soma Zaidi ...

MCHEMBA UMEMALIZIKA

Dogo inabidi aisaidie polisi kwa kukisukuma kisakina mara baada ya kumazikiwa na mafuta Soma Zaidi ...

NDEGE YA ETHIOPIA YAANGUKA BAHARINI


Ndege moja ya abiria ya kampuni ya Ethipia Airline imeanguka katika bahari ya Mediterenian muda mfupi baada ya kuruka ikitokea Beirut.

Ndege hio ilipoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kuruka mapema asubuhi ya leo, walioishuhudia ajali hio walisema kua moto mkubwa umeonekana katika eneo la bahari pahali ambapo ndege hio imeangukia.Wakuu wa kikosi cha uokoaji cha Lebanon wamesema kua wamefanikiwa kuwaokoa watu saba.

Ndege hio aina ya Boeing 737 iliyoruka katika uwanja wa ndege wa Beirut Lebanon 2:10 am na kutarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Adis Ababa Ethiopia saa 7:50 am (local time), ilikua imbeba abiria zaidi 83 pamoja na wafanyakazi 7.

Wakuu wa Lebanon wameanzhisha zoezi la uokoaji katika ajali hio lakini zoezi hilo limekua likifanyika kwa tabu kutokana na kuwepo kwa upepo mkali pamoja na mvua kubwa.

Abiria waliokuwemo ndani ya ndege hio ni pamoja na walebanon 54 waethiopia 22 pamoja na raia kutoka mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Iraq
Soma Zaidi ...

HOUSE BOY - BAKARI

Bakari is a house boy who every day drinks the wine of his Boss and puts water in the bottle to replace what he drank. But the Boss having suspicions as for the quality of the wine, he decides to buy pastis (a French wine that changes color if you add water).

Bakari as usual, takes a mouthful and add water to replace what he drank. However, soon after he added water the pastis became milky.

When the Boss came back and noticed it, he was sure he had managed to nail Bakari as thief!!! At that same moment Bakari realized he was in trouble and decided to go into the kitchen.

The Boss told his wife that 'Mary, you will see today, he will be obliged to acknowledge'. So he calls Bakari.

He shouted: “Bakari”

Bakari answered” “Yes Boss”

Boss” ‘Who drank my pastis?’

No answer.

Then the Boss went to fetch Bakari from the kitchen and says to him: You insane or what? Why when I call you, you say yes Boss but when I ask you a question you don’t answer me?

Bakari retorted that ‘it is that boss, when you are in the kitchen there, you don’t hear anything at all, except the name.

Then to prove that Bakari lies, the Boss says to him: ‘You stay beside Madam here, me I go in the kitchen, and you ask me a question’. Bakari accepted and the Boss went in the kitchen

Bakari shouted: Boss’.

He answered; ‘Yes Bakari’.

Bakari continued; ‘Who goes in the maid bedroom when the madam is not here?’

No answer

Bakari shouted again: ‘Boss, I say who made the maid pregnant?’

No answer

Bakari shouted again (third time); ‘Boss, I say who made the maid pregnant?’

The Boss returns from the kitchen running and says, Bakari, it is true, you are right. When one is in the kitchen, does not hear anything, only the name! Soma Zaidi ...

Sunday, January 24, 2010

UONEVU HUU MPAKA LINI?

Kwa muda mrefu sasa tumekua tukishuhudia mateso na dhuluma zinazofanywa na vyombo vya usalama kama vile Jeshi la polisi, JWTZ na wengine.

Ninavyojua mimi ni kuwa hivi vyombo vya dola vipo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi pamoja na mali zao lakini hali hii imekua ni kinyume, walinzi wetu hawa wamekua wakijipandia magari ya abiria bure,wamekua wakiwavua na kuwanyang'anya watu nguo zao, wanawapiga watu wasio na hatia na wengine kuwasababishia vifo na ulemavu wa maisha.


Swetu Fundikira aliezaliwa tarehe 28/06/1962 ni mmoja wa watu waliokutwa na mikasa ya kupigwa na wanajeshi wa JWTZ siku ya ijumaa usiku katika maeneo ya kinondoni na kupelekea kulazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na hatimae kuaga dunia leo asubuhi kutokana na majeraha aliyoyapata.

Marehemu kaacha mke, watoto wawili na mjukuu mmoja, Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema.......................Ameen.

Kwa kweli hii hali imekua inatisha na haionekani kama kuna mtu ambae anaweza kuizuia kwa kuwachukulia hatua hawa wanajeshi, maana kama wangelikua wanachukuliwa hatua za kisheria na wakuu wao wa kazi na Serikali kwa ujumla pindi wanapofanya makosa basi wasingekua wakifanya mambo hayo kwa hayo kila siku, lakini hapa unaeza kusikia wahusikawamehamishwa sehemu zao za kazi na kupelekwa mkoa mwengine.

Lakini ifahamike kua kuna siku watu watachoka na kuanza kujichukulia hatua mikononi mwao kwa kupambana na vyombo vya dola iwapo tu Serikali haikulifanyia ufumbuzi hili tatizo
Soma Zaidi ...

MATOKEO YA MECHI ZA LEO

Vijana machachari wa Mourinho Inter milan wamewafunga wapinzani wao AC Milan mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa San Siro.

Matokeo ya mechi nyengine ni kama ifuatavyo:

FA Cup
Scunthorpe United 2 - 4 Manchester City
Stoke City 3 - 1 Arsenal

African Cup of Nations
Ivory Coast 2 - 3 Algeria
Angola 0 - 1 Ghana

La Liga
Real Madrid 2 - 0 Málaga CF
Getafe CF 1 - 0 Atlético Madrid
CD Tenerife 0 - 0 Valencia CF
Villarreal CF 4 - 2 Real Zaragoza
Xerez CD 1 - 2 Osasuna
RCD Espanyol 1 - 1 RCD Mallorca
Sporting Gijón 0 - 1 Racing Santander

Serie A
Internazionale 2 - 0 AC Milan
Genoa 2 - 0 Atalanta
Udinese 2 - 3 Sampdoria
Siena 1 - 1 Cagliari
Lazio 1 - 1 Chievo
Palermo 3 - 0 Fiorentina
Bologna 2 - 1 Bari
Livorno 0 - 2 Napoli

Bundesliga
Hoffenheim 0 - 3 Bayer Leverkusen
VfL Wolfsburg 2 - 3 1. FC Köln

Dutch Eredivisie
VVV-Venlo 1 - 1 Feyenoord
FC Groningen 0 - 0 FC Twente
Sparta Rotterdam 0 - 0 ADO Den Haag
Ajax 1 - 0 AZ Alkmaar Soma Zaidi ...

MNAKUMBUKA HAYA MAMBO?

Mambo haya nayakumbuka yalikua yakipatikana sehemu mbali mbali ambazo ni maarufu licha ya kuwepo sehemu nyingi ambazo sio maarufu, sehemu maarufu kama vile kwa Adnan, kwa kijiko, kwa bi Tumai na kuna yule wa pale mlandege kwa Satar karibu na msikiti wa baruan yeye nimemsahau jina. Soma Zaidi ...

BARAFU BADO INAANGUKA

Barafu imeanguka tena usiku wa kuamkia leo huku mjini kwetu na kufanya kibaridi kupepea kwa nguvu, siku kadhaa zimepita tangu ilipoyayuka ile barafu iliyoanguka katika mwezi wa Disemba Soma Zaidi ...

MATOKEO YA MECHI ZA JANA

Mashetani wekundu jana walijilia pweza kizani katika mechi ya ligi kuu Uingereza kwa kuibugiza Hull City magoli 4-0 katika mechi iliyochezwa Old Trafford, magoli yote katika mechi hio yalifungwa na Rooney,matokeo ya mechi nyengine ni kama ifuatavyo.

Kombe la FA
Tottenham Hotspur 2 - 2 Leeds United
Southampton 2 - 1 Ipswich Town
Derby County 1 - 0 Doncaster Rovers
Cardiff City 4 - 2 Leicester City
Notts County 2 - 2 Wigan Athletic
Everton 1 - 2 Birmingham City
Accrington Stanley 1 - 3 Fulham
Bolton Wanderers 2 - 0 Sheffield United
Portsmouth 2 - 1 Sunderland
Aston Villa 3 - 2 Brighton & Hove Albion
Wolverhampton Wanderers 2 - 2 Crystal Palace
West Bromwich Albion 4 - 2 Newcastle United
Preston North End 0 - 2 Chelsea
Reading 1 - 0 Burnley

La Liga
Deportivo La Coruña 3 - 1 Athletic Bilbao
Real Valladolid 0 - 3 FC Barcelona
Sevilla FC 1 - 0 UD Almería

Serie A
Juventus 1 - 2 AS Roma
Catania 3 - 0 Parma

Bundesliga
Borussia Dortmund 1 - 0 Hamburger SV
VfL Bochum 2 - 2 Schalke 04
Hertha BSC 0 - 0 Borussia Mönchengladbach
1. FC Nürnberg 1 - 1 Eintracht Frankfurt
FSV Mainz 05 1 - 0 Hannover 96
Werder Bremen 2 - 3 Bayern München

Serie A
Juventus 1 - 2 AS Roma
Catania 3 - 0 Parma

Dutch Eredivisie
RKC Waalwijk 0 - 1 NAC Breda
Roda JC 2 - 0 FC Utrecht
sc Heerenveen 4 - 2 Willem II
Heracles Almelo 1 - 2 Vitesse

Na raiba ya mechi za leo ni kama ifuatavyo:

FA Cup
14:30 Stoke City v Arsenal

African Cup of Nations
17:00 Angola v Ghana
20:30 Ivory Coast v Algeria

La Liga
17:00 CD Tenerife v Valencia CF
17:00 Villarreal CF v Real Zaragoza
17:00 Xerez CD v Osasuna
17:00 RCD Espanyol v RCD Mallorca
17:00 Sporting Gijón v Racing Santander
19:00 Getafe CF v Atlético Madrid
21:00 Real Madrid v Málaga CF

Serie A
15:00 Genoa v Atalanta
15:00 Udinese v Sampdoria
15:00 Siena v Cagliari
15:00 Lazio v Chievo
15:00 Palermo v Fiorentina
15:00 Bologna v Bari
15:00 Livorno v Napoli
20:45 Internazionale v AC Milan

Bundesliga
15:30 VfL Wolfsburg v 1. FC Köln
17:30 Hoffenheim v Bayer Leverkusen

Dutch Eredivisie
12:30 Ajax v AZ Alkmaar
14:30 VVV-Venlo v Feyenoord
14:30 FC Groningen v FC Twente
14:30 Sparta Rotterdam v ADO Den Haag

NB: mechi zote ni kwa (CET) Soma Zaidi ...

Saturday, January 23, 2010

UMASIKINI HUU UTAKISHWA LINI?

Soma Zaidi ...

FEDERER ATINGA MZUNGUKO WA NNE AUSTRALIAN OPEN

Mcheza tenis namba moja duniani Rogger Federer atinga katika mzunguko wa nne kwenye mashindano ya Australian Open baada ya kumbamiza bila ya huruma kwa seti tatu bila 6-3, 6-4, 6-4 mspain mweny kushikilia nafasi ya 23 duniani Albert Montanes.Federer atakutana na Lleyton Hewitt katika mzunguko huo wa nne. Soma Zaidi ...

AKUTWA UFUKWEI AKIWA AMEKUFA

Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Samson Kivinge aliyekua mfanyakazi wa ubalozi wa Denmak, maerehemu alikutwa akiwa amekufa katika ufukwe wa karibu na hospitali ya Aga Khan leo asubuhi Soma Zaidi ...

MAMBO YA CHIPSI KUKU




Soma Zaidi ...

AKATWA MKONO BAADA YA KUIBA SIMU SOMALIA


Kijana mmoja nchini Somalia anaejuilikana kwa jina la Yussuf Sheikh Ahmed amekatwa mkono baada ya kuhukumiwa kwa sheria za kiislam na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab baada ya kukamatwa akiiba simu.

Yussuf ambae ana umri wa miaka 30 mkaazi wa Merka alikatwa mkono wake wa kulia baada ya kukiri kutenda kosa hilo mahakamani na baadae aliwahishwa hositali kwa matibabu baada ya kupewa adhabu hio.

"Adhabu hii ni mojawapo ya juhudi zetu za kutokomeza uhalifu kwa sheria za kiislamu, mtu yoyote atakayeiba atakatwa mkono wake", alisema Sheikh Isa Mohamed, ambaye ni mmoja wa maafisa wa Al Shabab.

Kundi la Al Shabab linaihikilia baadhi ya miji nchini somalia na kuendesha hukumu chini ya sheria za kiislamu kwa wale wote wanaokamatwa na makosa kama ya wizi, uzinifu, ulevi n.k .
Soma Zaidi ...

Thursday, January 21, 2010

RAHA KAA NINIIIIIIII !!!!!!!!!!!


Soma Zaidi ...

HII NDIO BONGO BWANA!!!

Bongo wewe pale unapoandikiwa hakuna njia basi wewe pita hapo hapo ndio mambo yatakwenda
Soma Zaidi ...

SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI


Soma Zaidi ...

LAZIMA UJAE LEO


Soma Zaidi ...