Saturday, May 29, 2010

50 CENT ALIVYOJIANDAA NA "THINGS FALL APART"

50 Cent amepoteza uzito kwa ajili ya filamu yake mpya ijulikanayo kama, "Things Fall Apart". Katika filamu hiyo, 50 Cent anaigiza sehemu kama mcheza mpira ambaye anagundulika kuwa na saratani.

Alipungua uzito toka paundi 214 hadi 160 kwa kula lishe maalumu ya vimiminika pekee (liquid diet) na kufanya mazoezi ya -treadmill- kwa saa tatu kila siku kwa muda wa wiki nane.

"Nilifunga kula." Kwa sasa amerejea katika ziara zake na anasema, "Nimeanza kula. Nitarudia hali yangu kiafya muda si mrefu!"

No comments:

Post a Comment