Friday, May 28, 2010

TANGAZO LA MSAADA

NDUGU ZANGU
Assalamu 'alaykum

Kijana ambae picha yake imeambataniswa ni mgojwa wa kidonda ndugu. Tayari ameshakwenda hospitali nyingi hapa Zanzibar na Tanzania Bara lakini hali inazidi kuwa mbaya. Uchunguzi wa madaktari umegundua kwamba mishipa yake ya damu imeziba na ndio maana kidonda chake hakipoi (Angalia picha iliyoambatanishwa). Ameshauriwa kwenda India.

Tayari Shs 1,000,000/= zimeshakusanywa na kuna mtu amejitolea kutoa tiketi. Yupo mwengine ambae amejitolea kumpeleka. Fedha inayohitajika ni kama dola 4,000 hivi ambazo tumeona tuwaambie wenzetu ambao watapenda kutabaruk. Hizi si taarifa za kitapeli na naamini nyote mnanielewa. Na wala email yangu haijatekwa.

Kijana ni mzaliwa wa Tumbe (1987) lakini kwa sasa yupo Jang’ombe na anapatikana wakati wewote. Harakati na kumtafutia safari zimeshaanza. Hivyo tunakuomba na wewe utuunge mkono kwa chochote utakachojaaliwa. Unaweza kunipatia mimi 0777 420247 au mlezi wake Sheikh Omar ambaye husalisha sana sala ya Adhuhuri na hudarsisha msikiti wa Mtendeni karibu na tawi la chama cha wananchi makao makuu 0774 101166 au unaweza Kumuona ustaadh Maulid, anauza duka Malindi karibu na mkahawa wa Tausi.

Naomba tuwaarifu na wengine ambao watapenda kumsaidia huyu kijana na ambao hawamo katika orodha ya ujumbe huu.
Tafadhali pia watumie ujumbe huu ndugu zetu wengine ambao wanatunia mtandao.

Sote ni ndugu. Tumsaidie huyu kijana ili nasi Allah (SW) Atusaidie.

Shukran

Said Othman
Zanzibar AIDS Commission
P.0.BOX 2820
Shangani Kelele Square


No comments:

Post a Comment