Tuesday, May 18, 2010

NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA AFGHANISTAN ABIRIA WAHOFIWA KUFA

Balozi za Marekani na Uingereza mjini Kabul Afghanistan, zimethibitisha kuwa raia watatu wa Uingereza na mmoja wa Marekani, walikuwa katika ndege ya kiraia iliyoanguka nchini humo.

Haijafahamika iwapo kuna abiria wowote waliyonusurika katika ajali hiyo, ambapo hali mbaya ya hewa imekuwa kikwazo kwa waokoaji kufika katika eneo la ajali

Ndege hiyo ikiwa na abiria 44 sita wakiwa ni raia wa nje, ilianguka jana katika mameneo ya milimani kaskazini mwa Afghanistan.Ni ndege ya shirika binafsi la Afghanistan liitwalo Pamir Airways.

No comments:

Post a Comment