Friday, May 21, 2010

Kitendawili cha timu ipi itatwaa ubingwa katika wa Ligi Kuu Zanzibar msimu huu kinazidi kuwa kigumu hasa kutokana na matokeo ya mchezo wa juzi kati ya Miembeni na Duma.

Mchezo huo ulimalizika kwa Duma ya Pemba kuilaza Miembeni bao 1-0. Timu hizo zilianza mchezo kwa kasi, huku zikionekana kukamiana zaidi lakini umaliziaji kwa pande zote ulikuwa tatizo.

Miembeni kila inapocheza, imekuwa ikipata mashabiki wengi wakiwemo wanawake, jambo ambalo si nadra kuonekana zikicheza timu nyingine ilijikuta ikipoteza mwelekeo wa kuwemo katika kinyang'anyiro cha timu zinazogombea ubingwa msimu huu.

Mchezaji Ali Ahmed, aliyefanikiwa kuifungia Duma bao pekee na la ushindi katika mchezo huo, dakika ya 22 na kudumu hadi mapumziko.

Licha ya Miembeni kucheza kwa kasi zaidi kipindi cha pili, huku wachezaji wake Khamis Mcha " Viali" Said Kuzu na Othman Omar "Mani" kuhaha huku na kule kutaka kukomboa bao hilo, lakini ulinzi wa Duma ulikuwa mkali na kuhakikisha timu hiyo haiondoki na pointi kiwanjani hapo.

Ushindi huo wa Duma umeifanya timu hiyo kufikisha pointi 22 na kukamata nafasi ya tatu nyuma ya Zanzibar Ocean View yenye pointi 23 na KMKM inayoongoza ligi ikiwa na pointi 24.

No comments:

Post a Comment