Monday, May 24, 2010

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA BRITISH AIRWAYS WAGOMA

Mgomo wa siku tano wa shirika la ndege la Uingereza, British Airways umeanza leo baada ya viongozi wa shirika hilo na vyama vya wafanyakazi kushindwa kufikia makubaliano.

Kiongozi wa chama cha wafanyakazi cha Unite, Tony Woodley, aliwaambia waandishi habari jana Jumapili kwamba mgomo huo ungeweza kusimamishwa tu kama shirika la ndege la British Airways lingerudisha marupurupu ya usafiri kwa wafanyakazi wake.

Mkuu wa shirika hilo, Willie Walsh, ameapa kutekeleza mpango wa shirika hilo wa kubana matumizi.

Shirika la British Airways linapanga kupunguza matumizi kwa kiasi cha zaidi ya euro milioni 72 baada ya kupata hasara kubwa Ijumaa iliyopita, tangu lilipobinafsishwa mnamo mwaka 1987.

.

No comments:

Post a Comment