Tuesday, May 18, 2010

BOATENG AOMBA RADHI KWA KUMUUMIZA BALLACK

Kevin Boateng ameomba radhi kutokana na kumchezea rafu mbaya nahodha wa Ujerumani Michael Ballack katika mechi ya fainali ya kombe la chama cha soka cha Uingereza FA kati ya timu ya Portsmouth na Chelsea.Rafu hiyo imemfanya Ballack kuzikosa fainali zijazo za kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

Boateng ambaye anatoka Ghana lakini mzaliwa wa Ujerumani,ameliambia Gazeti la michezo la hapa Ujerumani Sport-Bild kuwa hakudhamiria kumchezea rahi hiyo Ballack.

Kocha wa Ujerumani Joachim Löw ametangaza kuwa sasa kiungo wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger ndiye atakayebeba jukumu la kusimamia kiungo katika kikosi cha Ujerumani.

Wakati huo huo, mahakama ya kimataifa ya michezo iliyoko uswis imetupilia mbali rufaa ya timu ya Bayen Munich kutaka kuondolewa kwa adhabu ya kutocheza mechi tatu inayomkabili kiungo wao Frank Ribery.Kufuatia hukumu Ribery hatoweza kuwemo katika kikosi cha timu kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya Jumamosi ijayo dhidi ya Inter Milan ya Italia

No comments:

Post a Comment