Monday, May 31, 2010

BINTI AFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA JIWE

Mtoto wa kike mwenye miaka 13, Tauhida Haji Abdul-rahman, amefariki dunia hapo hapo na mwenziwe Time Burhani Haji (12) amejeruhiwa baada ya kuangukiwa na jiwe wakati wakichimba mawe huko Mkwaju Mgoro, Micheweni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi, alisema Tauhida alifariki alipokuwa anachimba mawe na wenziwe kwa ajili ya kuvunja kokoto.

Alisema, katika harakati hiyo ya kuchimba mawe, jiwekubwa lilichomoka jiwe kubwa lililomuangukia na kupoteza uhai wake ambalo pia lilimjeruhi Time.

Kamanda Bugi alisema tukio hilo lilitokea Mkwaju Mgoro, Micheweni mnamo majira ya saa 7:00 mchana.

Kamanda alisema hali ya Time ambaye amejeruhiwa amelaza katika hospitali ya Micheweni anaendelea kupata matibabu huku hali yake ikielezwa kuwa siyo mbaya sana

Alisema mabinti hao walikuliwa wakichimba mawe kwa ajili ya kuvunjwa kokoto ili kuziuza

Kamanda alitoa wito kwa wachimbaji mawe kuwa na tahadhari katika kazi h yao hiyo hasa katika kipindi cha mvua kutokana na ardhi kushibwa maji hali ambayo inasababisha ardhi hiyo kuwa laini.

Daktari dhamana wa hospitali wa Wilaya ya Micheweni, Hamad Ali Hamad, alisemabinti aliyefariki aliumia kifua na mbavu huku aliyejeruhiwa aliumia mguu na mbavu.
.

No comments:

Post a Comment