Wednesday, March 31, 2010

ICC YAAMUA GHASIA ZA KENYA ZICHUNGUZWE


Ni rasmi kwamba wahusika wakuu wa machafuko yaliyozuka nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 watachunguzwa na kufunguliwa mashtaka.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ilimpa idhini mwendesha mashtaka mkuu Luis Moreno-Ocampo kufanya uchunguzi na kuwafungulia mashtaka washukiwa wakuu 20.


Ghasia zilizuka baada ya vyama vikuu nchini humo, PNU na ODM, kutofautiana kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Watu zaidi ya 1,300 waliuawa na wengine zaidi wakapoteza makazi yao.


Majaji wawili kati ya watatu waliamua kwamba huenda uhalifu dhidi ya binadamu ulitendwa.
"Taarifa zilizopo zinatosha kudhihirisha kwamba uhalifu dhidi ya binadamu ulitendwa nchini Kenya," waliamua majaji hao.

Lakini jaji mmoja alitofautiana na wenzake kuhusu uamuzi huo.


Akiwasilisha ombi lake kwa majaji mwezi Novemba mwaka jana, Luis Moreno Ocampo alidai kwamba viongozi wa kisiasa walipanga na kufadhili machafuko hayo. Wakenya wengi wamepongeza uamuzi huo wakisema ni njia moja ya kumaliza mtindo wa kutenda uovu bila kujali.

.
Soma Zaidi ...

MKENYA MWENGINE AUAWA SAUDIA

Soma Zaidi ...

HAPO VIPI?

Kina dada wakipata kumbukumbu muhimu, lakini ni kweli siku zijazo watakuja kujuana nani ni nani katika picha hii?
Dogo anaandikiwa baada ya kuvunja sheria za barabarani na hii inadhihirisha wazi kwamba sheria haichagui mkubwa wala mdogo.


. Soma Zaidi ...

MANCHESTER, UINGEREZA PRESHA INAPANDA PRESHA INASHUKA


Baada ya timu ya Taifa ya Uingereza kupatwa na msiba wa kumpoteza mchezaji wake Beckham baada ya kuumia mguu sasa kuna jinamizi jengine linainyemelea timu hio.

Hii ni kutokana na kuumia kwa mshambuliaji wake tegemeo Wyne Rooney jana katika mechi dhidi ya Mnchester United na Bayern.

Rooney aliumia mguu katika dakika za mwisho za mchezo wa jana na kitendo hichi kinaweza kumuweka juu kwa muda wa wiki sita au zaidi na hii itategemea na uchunguzi wa kitabibu ambao utafanyika leo hii.

Kutokana na maumivu aliyoyapata jana mshambuliaji huyu ambae pia ni tegemeo katika timu yake ya Manchester United kuna uwezekano mkubwa wa kuikosa mechi ya jumapili ambapo Manchester watakua na mechi muhimu sana watakapocheza dhidi Chelsea, lakini pia kuna uwezekano mdogo wa Rooney kucheza katika mechi ya marudiano dhidi ya Beyern jumatano ijayo

Nae kocha wa Manchester United Sir Alex Farguson alisema "Rooney ameumia ankle lakini ni mapema mno kuzungumza chochote hadi hapo kesho (leo).

Hii ni mara ya 12 kwa Rooney kuumia ankle katika maisha yake ya uchezaji, lakini mara hii kuumia kwake kumekuja katika wakati mgumu hasa kwa Mahsetani hawa wekundu kwani inawezekana pia wakamkosa mshambuliaji wao kwa mechi zote zilizobaki katika msimu huu wa ligi.

.
Soma Zaidi ...

RUFAA YAKATALIWA KUUSHITAKI UM

Wakati huo huo , mahakama ya rufaa nchini Uholanzi imekubali hukumu iliyotolewa hapo kabla kuwa ndugu wa wahanga wa mauaji ya mjini Srebrenica hawataweza kuushtaki umoja wa mataifa kutokana na mauaji hayo.

Watu karibu 6,000 walionusurika na mauaji hayo pamoja na jamaa zao wamo katika kundi linalojulikana kama akina mama wa Srebrenica na wanasema kuwa umoja wa mataifa unahusika na mauaji hayo kutokana na kushindwa kuyazuwia.

Mawakili wanaowakilisha kundi hilo la watu walionusurika wanasema kuwa watakata rufaa katika mahakama kuu ya Uholanzi ili kulipeleka suala hilo katika mahakama kuu ya umoja wa Ulaya.



.
Soma Zaidi ...

Tuesday, March 30, 2010

Champions League - Bayern Munich v Manchester United: Key battles


We take a look at the key battles ahead of the Champions League quarter-final first-leg clash between Bayern Munich and Manchester United.

Franck Ribery v Gary Neville

With Arjen Robben set to miss out, the German side will look to Ribery to provide a threat from wide areas. While the Frenchman has been the subject of much speculation as to where he will be playing next season, for the meantime he is very much Bayern's star man, and they need a star performance from him. Veteran defender Neville's legs are ageing and while he may pose a threat going forward with his crosses, he could be seriously tested by Ribery's pace and trickery at the other end of the pitch.

Holger Badstuber v Wayne Rooney

Forget about the best player in the world debate for a moment, Rooney doesn't need that particular label to give Badstuber the runaround at the Allianz Arena. The Germany U21 international, a product of Bayern's youth system, looked shaky in the defeat to Stuttgart at the weekend and lacks the experience to contain a player in Rooney's current form. Indeed, Rooney will be hoping Bayern coach Louis van Gaal keeps Badstuber in his starting line-up.

Ivica Olic v Nemanja Vidic

Olic may be dropped for the visit of United after criticising Van Gaal, but the experienced coach knows the Croat striker probably represents his side's best chance of unsettling United's centre-backs. Strong, powerful and deceptively quick, Olic's workrate is second to none and Vidic, who has committed several high profile errors this season, will have his hands full.

Philipp Lahm v Nani

Nani has been resurgent of late but his influence will be checked by Germany international Lahm, who was one of few Bayern players to emerge with credit from last weekend's defeat. Lahm may only be 26 but he is vastly experienced and considering he is equally adept at going forward as defending, Nani will have to be diligent and willing to track back if he is not to be found out on Tuesday.

Marc van Bommel v Darren Fletcher

With Nani and Antonio Valencia likely to fill the wide positions, Fletcher is set to move back inside after a couple of brilliant performances on the flanks against Milan. Then, his influence on the result was enormous, as it can be in Germany if he can stamp his authority on the midfield. But vying for control of the middle of the park will be combative Bayern skipper Van Bommel, who has never been averse to sticking the boot in for his team and could prove to be a real thorn in United's side.

***Eurosport Soma Zaidi ...

TANGANYIKA KILA SIKU NI UNYAMA TU




****Kwa hisani ya Bustani ya Waswahili.


. Soma Zaidi ...

MAMA SALMA KIKWETE ANUSURIKA AJALINI

Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, amenusurika kupata ajali baada ya msafara wake kugongwa na lori linalodaiwa kuwa lilikuwa limebeba bidhaa za magendo.

Lori hilo linadaiwa kuuvamia msafara huo na kusababisha baadhi ya magari yaliyokuwapo kugongana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Tanzania Daima, hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo zaidi ya magari yaliyokuwa katika msafara huo kuharibika.

Taarifa hizo zilibainisha kuwa ajali hiyo ilitokea jana asubuhi muda mfupi wakati msafara huo ukitokea Wilaya ya Tarime, mkoani Mara ukielekea Rorya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ajali hiyo ilitokea baada ya lori ambalo namba zake za usajili hazijafahamika mara moja likiendeshwa kwa mwendo wa kasi, kukaidi amri ya askari wa kikosi cha usalama barabarani kulitaka lisimame kwa ajili ya kupisha msafara wa mke wa rais.

“Lori ambalo namba zake hazijafahakamika mara moja liliingia kwenye msafara wa Mama Salma Kikwete, kutokana na kukaidi amri ya askari wa usalama barabarani kumtaka dereva kuupisha msafara huo,” kilisema chanzo cha habari.

Kiliongeza kwamba, baada ya kukaidi amri ya askari wa kikosi cha usalama barabarani, likiwa kwenye mwendo wa kasi liliingilia masafara wa Mama Salma Kikwete na kuligonga gari mojawapo na kwenda pembeni mwa barabara.

Imedaiwa kugongwa kwa gari hiyo ya tatu kutoka kwa mke wa kiongozi wa nchi, ilisababisha magari mengine yaliyokuwa nyuma ya msafara huo kugongana yenyewe kwa yenyewe.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, waliiambia Tanzania Daima kwamba, lori hilo lilishindwa kusimama kama lilivyoamriwa kutokana na kubeba bidhaa za magendo.

Mashuhuda hao waliongeza kwamba dereva wa lori hilo alikuwa akikimbia askari wa usalama kwa kuhofia kukamatwa akiwa na bidhaa za magendo.

“Lori lilishindwa kusimama kama lilivyoamriwa kutokana na kubeba bidhaa za magendo, dereva wa lori hilo alikuwa akikimbia askari wa usalama kwa kuhofia kukamatwa akiwa na bidhaa za magendo,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.

Tanzania Daima ilijaribu kuwasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime, Costatine Massawe kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini jitihada hizo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kupokewa na msaidizi wake na kudai yuko kwenye mkutano.

“Kamanda yupo kwenye kikao labda mpigie kuanzia saa moja usiku, mimi siwezi kuzungumza juu ya ajali unayoiulizia,” alisema msaidizi huyo.

Aidha Msemaji wa Jeshi Polisi nchini, Abdallah Msika aliithibitishia Tanzania Daima kutokea kwa ajili hiyo, lakini alishindwa kutoa maelezo zaidi kwa madai hajapata taarifa za kina.

Kamanda Msika alisema alikuwa nje ya ofisi na aliporudi alijaribu kuwasiliana na makamanda wa mikoa ya kipolisi ya Tarime na Rorya bila mafanikio kutokana na kuwepo kwenye mikutano.

Alibainisha kuwa baada ya kushindwa kuwapata makamanda hao, aliwasiliana na maofisa kadhaa ambao walimthibitishia kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ndugu yangu mke wa mheshimiwa rais amepata ajali, lakini hakuna aliyefariki na pia sikuweza kupata taarifa za kina zaidi,” alisema Msika.

Aliliahidi Tanzania Daima kuwa, atafuatilia kwa karibu suala hilo, lakini mpaka tunakwenda mitamboni alishindwa kufanya hivyo kutokana na kutopatiwa taarifa na wahusika waliokuwapo eneo la tukio.

***Tz Daima

Soma Zaidi ...

Monday, March 29, 2010

IDADI YA WALIOUAWA KATIKA MIRIPUKO YA MOSCOW YAFIKIA 38


Miripuko ya leo asubuhi mjini Moscow yametajwa kama mbaya zaidi kutokea katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Wizara inayoshughulikia mambo ya dharura imethibitisha kwamba watu 38 waliuawa.

Katika mripuko wa kwanza watu 24 waliuawa na 20 kujeruhiwa katika kituo cha Lubyanka na wengine 14 walipoteza maisha yao na 15 kujeruhiwa katika mripuko wa pili karibu na bustani la utamaduni.

Maafisa wa idara ya ujasusi ya Urusi, FSB wamesema waripuaji hao wawili wanawake waliojitoa mhanga walikuwa na mabomu ya uzito wa kilo moja na nusu na kilo tatu .

Mamia ya waokoaji walifika katika maeneo ya mikasa yanayotajwa kama mbaya zaidi tangu mwaka wa 2004 wakati mwanamgambo wa Kichechen aliporipua bomu katika kituo cha treni na kuwauwa watu 41 na kuwajeruhi wengine 250.

Picha za televisheni nchini Urusi zilionyesha vituo vya treni chini ya ardhi zikifuka moshi na waathiriwa walitiririkwa na damu. Kufikia sasa hakuna kundi lolote lililojitokeza kupanga miripuko hiyo lakini wachunguzi wanawatuhumu wanachama wa kundi la wanamgambo wa kaskazini wenye msimamo mkali wa Kiislamu. Meya wa mji wa Moscow, Juri Luschkov alikiri kwamba miripuko hiyo ilikuwa imepangwa.

Kituo cha Lubyanka kiko karibu na makao makuu ya shirika la ujasusi la FSB lililochukua nafasi ya lile la KGB.

Mwendesha mashtaka mjini Moscow alisema waripuaji hao wa kujitoa mhanga walikuwa wamebeba mambomu hayo lakini bado hawajadhibitisha kama yaliripuriwa kwa kutumia mbinu ya kisasa inayohusisha simu ya kiganjani.

Shirika la habari la Novosti limeripoti kwamba wachunguzi walipata bomu lingine ambalo halikuwa limeripuka karibu na eneo la mikasa.

Rais wa Urusi, Dmitry Medvedev aliyeongoza dakika moja ya ukimya kuwakumbuka waliowawa, awali alitoa hotuba kwa taifa na aliapa kupiga vita ugaidi.

Waziri mkuu wa Urusi, Vladmir Putin alikatiza ziara yake ya Siberia na alitoa wito kwa mashirika ya ujasisi nchini humo kufanya kazi kwa pamoja kukabiliana na ugaidi.

Kati ya viongozi waliotuma risala zao za rambirambi ni Rais Barack Obama wa Marekani, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Mawaziri wakuu Gordon Brown wa Uingereza na Manmohan Singh wa India , viongozi wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya kujihami ya NATO.


.
Soma Zaidi ...

JK AKIENDESHA KIKAO CHA CCM IKULU JANA

Hivi ni kweli kuvaa au kutovaa hizi sare za Chama ((green) kunaashiria mapenzi ya Chama? nauliza hivi kwa sababu Rais Karume ameku akionekana mara nyingi kutovaa sare za chama chake hasa kwenye vikao vikubwa kama hivi.


. Soma Zaidi ...















***Maathir Muhanad,

Dar-es-Salaam.

. Soma Zaidi ...

MADEREVA WA DALA DALA KUGOMA

Madereva na makondakta wa daladala jijini Dar es Salaam wametangaza mgomo wa chinichini kuanzia leo.
Taarifa za mgomo huo wa siku mbili zilisambazwa jana na baadhi ya madereva kwa kutumia ujumbe wa maandishi ulioandikwa katika vikaratasi.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mgomo huo utahusisha njia zote za mkoa wa Dar es Salaam, huku madereva hao wakidai mgomo huo una baraka zote za Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA).

Maderava hao wanadai sababu ya mgomo huo ni maslahi duni, kero za barabarani zinazosababishwa na Kampuni ya Majembe na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, (Trafiki) ambao wamekuwa kikwazo kikubwa.

Madai mengine ni kutopatiwa dhamana, kutaka mazingira bora ya kazi pamoja na mishahara na makato ya mishara kupelekwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na marupurupu mbalimbali.

Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya madereva wakipeana vikaratasi hivyo katika maeneo ya Posta, Gongo la Mboto, Buguruni na Ilala huku kukiripotiwa kuonekana hali kama hiyo maeneo ya Mwenge.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa masharti ya kutotajwa majina, madereva hao walisema wameamua kufanya mgomo huo kutokana na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa Majembe na trafiki pamoja na kudai maslahi yao.

“Tunafanya kazi katika mazingira magumu, huku tukisumbuliwa na Majembe na trafiki na mwisho wa siku hakuna tunachokipata kwani mwajiri naye amekupangia hesabu yake. Kwa kifupi hatuna uhakika na maisha yetu,” alisema dereva mmoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa DARCOBOA, Sabri Mabruki, alipoulizwa kuhusiana na habari za kuwepo kwa mgomo huo, alisema hana taarifa.

“Mimi sina taarifa ya mgomo huo, ndiyo kwanza nazisikia kwako, hakuna mgomo sisi hawajatuletea taarifa zozote,” alisisitiza Mabruki.

Mabruki aliendelea kusema kuwa madai yao hayo ya kutaka kugoma hayana msingi wowote kwao kwani mikataba ya madereva hao iko wazi na kila siku wanaambiwa kufuata mikataba yao lakini hawajitokezi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mpaka sasa madereva 2500 baadhi yao wana mikataba huku wengineo wakiombwa kuchukua mikataba yao lakini hawataki kufanya hivyo.

“Sisi kama DARCOBOA, tunasema mgomo huo si halali na wala hatuujui,” alisema Mabruki.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Mabasi ya Abiria Dar es Salaam (UWAMADAR), Shukuru Mlawa, hakuweza kupatikana kuzungumzia ngomo huo.


.
Soma Zaidi ...

MIAKA MIWILI BAADA YA MAKUBALIANO MAGEUZI BADO NI NDOTO KENYA

Mwezi Machi 2008, wanasiasa mahasimu nchini Kenya walikuwa wakipiga zumari la mabadiliko ya kisiasa na Jumuiya ya kimataifa ikipongeza mafanikio ya kupatikana suluhisho la mgogoro uliozuka baada ya uchaguzi mwishoni mwa 2007, jambo ambalo ni nadra barani Afrika.

Lakini pamoja na hayo miaka miwili baadae hali halisi iliopo ni tofauti kabisa .
Mwana harakati mmoja anasema ilikuwa ni lazima zifanyike jitihada za kuinusuru Kenya baada ya machafuko na mauaji yaliotokana na uchaguzi mkuu wa Desemba 2007.

Makubaliano yaliosainiwa Februari 28 2008 na kuanza kufanya kazi mwezi Machi mwaka huo, juu ya kugawana madaraka, yalikua na ahadi ya kufanyika marekebisho.

Lakini kuna wanaodai kwamba sambamba na baraza la mawaziri kufanywa kuwa kubwa ili kuzihusisha pande zote zilizohusika katika mgogoro huo, hayo sasa yanaonekana kuandamana pia na kuzidi kwa rushwa serikalini. Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, aliyekua mpatanishi miaka miwili iliopita pamoja na dola zenye nguvu za magharibi zilizosaidia kupatikana makubaliano, wanaendelea kuikumbusha Kenya juu ya ahadi zake na kuonya juu ya ulipizaji kisasi na hofu ya kuzuka upya mivutano ya kikabila.

Mnamo takriban ziara yake ya tano nchini Kenya wiki iliopita, Bw Annan alizungumzia kuvunjwa moyo na pia hali ya wasi wasi. Pamoja na kugawana madaraka, lakini utendaji wa serikali ya muungano nchini humo hauridhishi kwa sababu ya mivutano isiyokwisha na mtu anaweza kusema imeshindwa kuwajibika kama Wakenya walivyotarajia.

Mgogoro wa hivi karibuni tu ni ule uliozuka baada ya waziri mkuu Raila Odinga kutangaza anawasimamisha mawaziri wawili waliotajwa katika kashfa tofauti hadi uchunguzi umekamilika. Hao walikua ni waziri wa kilimo William Ruto na wa elimu Profesa Sam Ongeri.

Lakini hatua hiyo ikapingwa na Rais Kibaki akisema Odinga hana mamlaka hayo na wala hakumshauri. Kibaki akawataka mawaziri hao waendelee na kazi zao. Baadhi ya wadadisi wanasema mivutano katika serikali ya Kenya sio tu jambo linalomvunja moyo.

Bw Annan kama mtu aliyekua mpatanishi , lakini pia mabalozi wa nchi za magharibi waliokua wakisaidia suluhisho lipatikane. Sasa wanaonekana kama nao wameshindwa na sasa wanazungumzia athari zake, pindi wanasiasa wa Kenya hawatakuwa makini.
Afisa mmoja wa kibalozi aliyetaka asitajwe jina amesema kwa mtazamo wa migogoro mengine barani Afrika, tangu ulipozuka ule wa Kenya, kuna umuhimu wa kuzingatia ujumbe uliotolewa kwa watawala katika mgogoro wa kisiasa Zimbabwe au nchini Madagascar.

Anasema la sivyo mtindo wa watawala kufanya mizengwe ukiwemo wizi wa kura wakati wa uchaguzi ili wabakie madarakani utaendelea.

Mwanaharakati Mwalimu Mati anasema Kwa Kenya, inaonekana hata miaka miwili baada kutiwa saini makubaliano ya kugawana madaraka, mivutano iliopo haina dalili ya kumalizika.

Anasema Rais Kibaki hataki kuona yaliokubaliwa yanatekelezwa kwa sababu yatamaliza madaraka makubwa aliyonayo kama rais na Odinga hatoregeza kamba kwa sababu akiwa kama Waziri mkuu anataka atambuliwe kuwa ni mkuu wa serikali nao mawaziri hawatotaka kuona mivutano inamalizika na wanawajibika kwa sababu wanataka waendelee katika nyadhifa zao na kuwepo nafasi zaidi ya uporaji mali ya umma. Mwanaharakati huyo anamaliza kwa kusema hali hii ni sawa na " njama iliopangwa barabara dhidi ya umma wa Kenya."

.
Soma Zaidi ...

Sunday, March 28, 2010

UJERUMANI KUANZA MAZUNGUMZO KUHUSU WAFUNGWA WA GUANTANAMO

Wizara ya ndani ya Ujerumani imethibitisha imeanza tena mazungumzo na Marekani kuhusu uwezekano wa kuwakubali wafungwa wa zamani wa gereza la Guantanamo.

Karibu mwaka mmoja sasa,Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa akijaribu kulifunga gereza hilo lililoko katika eneo la Cuba lililo kwenye mamlaka ya Marekani lakini amekumbana na matatizo ya kupata nchi zitakazowakubali wafungwa walioachiliwa.

Kiongozi wa ngazi ya juu wa masuala ya usalama nchini Ujerumani amelipinga hatua yá kuwakubali wafungwa wa Guantanamo akionya kwamba linaweza kusababisha wasi wasi mkubwa wa usalama.





. Soma Zaidi ...

MAMBO YA DEN HAAG a.k.a THE HEGUE

Hapa ni Station kwa nje
Hii ni Station ya Tram ya nje

Station ya Treni kwa ndani na kwa sehemu ya juu kuna Station ya Tram pia

Sehemu ya kuingilia Station na zile ngazi ndio za kuendea juu kwenye Tram

. Soma Zaidi ...

BERBATOV A.K.A BERBATOP AIWEKA MANU TOP


Dimitar Berbatov airejesha tena Manchester United kileleni mwa ligi ya Uingereza kwa kudhihirisha kwamba maisha yanaendelea hata bila ya mshambuliaji machachari Wyne Rooney.

Berbatov alitoa zawadi kwa Ferguson baada ya ile kamari aliyocheza ya kumueka nje ya kikosi Wyne Rooney

Kizaa zaa kilianza pale mchezaji wa Bolton Jlloyd Samuel alipouzamisha nyavuni mpira wa krosi uliopigwa na Giggs na kuandika goli la kwanza kwa upande wa Mashetani wekundu.

Baadae ilikua ni zamu ya Berbatov alipopachika bao la pili na la tatu, lakini mambo hayakuishia hapo mabadiliko aliyoyafanya Sir Alex yalizaa matunda pale alipomtoa nje Giggs na kumuingiza Gibson ambae aliweza kupachika bao la nne katika dakika ya 82 baada ya kupokea pasi mwanana kutona kwa winga wa kushoto Nani.

Kabla ya mechi hio ya Mashetani wekundu kulikua na mechi kati ya Chelsea na Aston Villa ambapo Chelsea walitoa kichapo cha paka mwizi kwa Villa kwa kuwatandika mabao 7 - 1 licha ya kumkosa mshambuliaji wao matata Drogba.

Kwa matokeo hayo ya jana ManU wanarejea kileleni mwa ligi hio wakiwa na alama 72 huku Chelsea wakiwa kwenye nafasi ya pili kwa alama 71 huku wote wakiwa na michezo sawa.


.


Soma Zaidi ...

Saturday, March 27, 2010

SABABU ZA KUHARIBIKA NDOA NYINGI ULAYA

kwa ujumla ni nyingi zikiwemo kama hizi:


Katika sababu zenye kumhusu mume ni kama hizi:

1. Mwanamume kutokuwa na tabia nzuri.
2. Mwanamume kumdhulumu mwanamke na kutomtendea haki kwa kutomtimizia anayotakiwa amtimizie wa visingizio kama vile unafanya kazi kama ninavyofanya hivyo akawa hampi fedha wala hamnunulii mahitaji yake na kadhalika.
3. Mwanamume kushindwa kumtimizia mkewe haki yake kwa kujituma kupita kiasi na kila anapodaiwa haki akawa hawezi kwa uchovu au vyenginevyo.
4. Kupatikana kwa uasi kwa mmoja wao au kwa wote wawili jambo ambalo hupelekea kuharibika uhusiano baina yao kwa uasi huo mpaka ikafikia kupelekea kuachana.
5. Mwanamume kutokufan ya kazi na kutegemea kipato cha mwanamke anachosaidiwa na serikali kwa udanganyifu n.k.
6. Mwanamume kuwa mvivu na kutegemea serikali kumsaidia yeye kwa kudanganya serikali na pia kuwa na tabia za udanganyifu kwa kupata kipato cha haramu.
7. Mwanamume kupoteza masaa mengi kwenye internet au tv kutazama mipira na upuuzi mwengine na kutothamini kutumia wakati wake na mkewe.
8. Mwanamume kuwa na mahusiano na wanawake wengine nje ya ndoa.
9. Mwanamume kutumia masaa mengi kazini na kufanya overtime nyingi hata akirudi nyumbani yu hoi na hana nafasi na mkewe.
10. Mwanamume alioa kwa lengo la kudandia nyumba ya mke anayolipiwa na serikali ili abane matumizi na fedha zake atume makontena Afrika na kuanzisha miradi.
11. Tabiya chafu za wanaume kama kuvuta sigara, kula mirungi na mengine yenye kumkirihisha mke na kumkosesha subira za kukaa na mume.
12. Mwanamume kuoa mke mwengine.
13. Mwanamume kupenda maovu kama kutaama picha za ngono na sinema zisizo na maadili.
14. Mwanamume kutokuswali au kutokufanya ‘Ibaadah nyinginezo au kutoshikamana na Diyn kwa ujumla.

Na sababu zinazomuhusu mwanamke ni hizi:

1- kusagana
2-umalaya
3-kupenda hongo kwa wanaume
4-jeuri na wajuba
5-wambeya na mafisadi
6-wachoyo na wasengenyaji
7-wanapenda ushirikina
8- wanapenda vya watu
9-walaghai kwa mapenzi ya watu
10-wizi wa waume za watu
11-wanaeneza ukimwi kirahisi
12-waasi na kutowatii waume
13-kumfilisi mume kwa matakwa sio ya lazima
14-kusikiliza wazee na kumdharau mume
15-tamaa ya waume za watu na vitu
16- hawapendi kuzaa na kulea
17-wajinga sio wenye elimu


Mengine ambayo yanawahusu wote wawili ni haya yafuatayo:

1. Mahusiano mabaya baina ya mke na wazee wa mumewe au mahusiano ya mume na wazee wa mke.
2. Wazazi kuingilia kati ya ndoa ya watoto wao.
3. Kutokuwa na Imani na Taqwa inayohitajika.
4. Kutoijua Dini inavyohitajiwa kwa kila Muislamu.
5. Watu kuingia katika ndoa bila ya kujua haki na majukumu yake.
6. Ukabila na utaifa.
7. Watu kuwa na ada za siri (kujichua na kujisugua).
8. Watu kuwa na marafiki kabla ya kuoa au nje ya ndoa.

. Soma Zaidi ...

WALIMU ZANZIBAR WAPIGWA MARUFUKU KUVAA MABAIBUI

Na Salim Said

Wizara ya Elimu ya Zanzibar, imewataka walimu wa shule za serikali wanaovaa baibui kujieleza kwa maandishi sababu za kuvaa nguo hizo wawapo kazini.


Waziri wa Elimu wa Zanzibar, Haroun Ally Suleiman aliliambia gazeti hili jana kuwa wizara ina mwongozo wa mavazi kwa walimu na wanafunzi wanapokuwa shuleni hivyo hawaruhusiwi kuvaa baibui.


Alisema mwongozo huo wa mwaka 1988, ndio unaowaelekeza walimu na wanafunzi aina ya mavazi wanayopaswa kuvaa wawapo shuleni.


"Zanzibar tuna mwongozo wa mavazi kwa walimu na hata wanafunzi, ulitungwa tangu mwaka 1988," alisema Haroun. Alisema kwa mujibu wa mwongozo huo, walimu wanazuiwa kuvaa baadhi ya baibui hasa zile ambazo zinazovaliwa nyakati za jioni visiwani.


â€Å“Hatutaki mavazi ambayo yatamsumbua mwalimu wakati wa kufundisha, hatutaki mavazi yanayofunika uso au baibui ya jioni, haya haturuhusu kabisa,â€‌ alisema Waziri Haroun.


Kauli ya waziri huyo imekuja baada ya gazeti hili kumtaka atoe ufafanuzi wa malalamiko ya baadhi ya walimu wa Kisiwa cha Pemba kwamba Mratibu wa Elimu ya Msingi Faki Suleyum Faki amewataka wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kuvaa baibui kazini.


Walimu hao walisema mratibu huyo amekuwa akiwataka wasivae nguo hizo kwa muda wote wawapo kazini jambo ambalo walisema kuwa hawajui msingi wake.


â€Å“Sisi hatuoni sababu ya mwalimu kukatazwa kuvaa baibui, hili ndilo vazi letu la stara, sasa serikali inapotuambia tusivae je inataka tutembee uchi,â€‌ alihoji mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ya Minungwini ambaye hakutaka kutajwa gazetini.


Walimu hao walidai kuwa mratibu huyo amewataka wajieleze kwa kuvaa baibui baada ya kuwakuta wameyavaa wakati wa kazi alipokuwa akitembelea baadhi ya shule za serikali visiwani humo juzi.


"Kwa kweli sisi wengine kazi hii itatushinda kwa sababu, inatupelekea kumwogopa kiumbe mwenzetu badala ya Mwenyezi Mungu, leo akija mkaguzi kutoka wizarani walimu wanajificha, akiondoka ndio wanarudi," alisema mwalimu mwingine.


Mwalimu huyo alisema utaratibu huo, umewaathiri sana walimu wa kike katika shule nyingi Kisiwani Pemba kwani unawalazimisha waache vazi lao la asili na linaloendana na imani ya dini yao.


"Hivi sasa walimu wengi hatuvai baibui, kwa sababu ukikutwa tu na mkaguzi kutoka wizarani hiyo itakuwa kesi kwako, kwa hiyo wengine huamua tu kuacha kuvaa," alisema mwalimu mwingine.


Jitihada za gazeti kumpata Mratibu huyo wa Elimu zilishindikana baada ya kukosa mawasiliano yake ya simu ya mkononi. Hata hivyo, moja ya utamaduni wa muda mrefu wa visiwa vya Zanzibar ni vazi la baibui ambalo hutofautiana mitindo, ambalo huchukuliwa kama sehemu ya dini ya Kiislaam kwa wanawake kusitiri miili yao.


Katika siku za hivi karibuni vazi hilo la baibui limeshika kasi baada ya kuibuka kwa mitindo mbalimbali ya nguo hiyo maarufu visiwani Zanzibar na hivyo hata baadhi ya wageni kulipenda vazi hilo.

. Soma Zaidi ...

BREAKING NEWS

Kuna taarifa ya kwamba MV Pemba imezama wakati ikitokea Dar kwenda Unguja na watu wamewahi kuokolewa ila mizigo imezama na Meli. taarifa kamili tutawaletea mara tu baada ya kuzipata.









.
Soma Zaidi ...

Friday, March 26, 2010

SOKA WIKI HII

Kura imepigwa kwa duru ya pili ya duru ya kwanza ya Kombe la Afrika la Mataifa ambao Tanzania ina miadi na Somalia n a simba wa nyika- Kameroun wakiwasubiri simba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Nako katika ligi ya Ujerumani kocha wa Bayern Munich, mdachi Louis van Gaal baada ya kuitimua juzi Schalke kwa bao 1:0 katika robo-finali ya Kombe la Ujerumani , adai sasa anataka mataji yote 3 msimu huu:Kombe la ulaya la chamüpions League,taji la Bundesliga na kombe hilo la Ujerumani.

"Nataka kushinda mataji 3", alisema mdachi huyo kabla Bayern Munich, haikuteremka jioni hii uwanjani kupambana na majirani zao wa kusini-Stuttgart.Munich kwahivyo, inabidi kutamba mbele ya Stuttgart, ili salamu zao kwa Manu ,adui yake ijumaane hii azitie maanani.Munich inacheza na Manchester katika robo-finali ya Champions League.Jumamosi iliopita lakini, Munich ilikiona kilichomtoa kanga manyoya ilipozabwa mabao 2:1 Frankfurt. haitataka kurudia makosa hayo leo.

Changamoto nyengine uwanjani jioni hii ni kati ya mainz na mabingwa wolfsburg,Hertha berlin na Borussia Dortmund wakati Hannover inaikaribisha nyumbani FC Cologne.Bremen inacheza na Nüremberg kabla ya kesho Hoffenheim kukumbana na Freiburg na Borussia Mönchengladbach kukamilisha kalenda ya Bundesliga mwishoni mwa wiki hii na Hamburg.

Ama katika Premier League, Muivory Coast ,Didier Drogba anaamini kwamba Chelsea bila kutamba kesho mbele ya Aston Villa itajikuta mashakani.
Kikosi hiki cha kocha Carlo Ancelotti kilipata nguvu mpya na ari mpya kati ya wiki hii kilipoicharaza Portsmouth mabao 5:0.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ana yakini kuwa ,Arsenal mwishoe,itasahau jiinamizi walilolion huko Birmingham City miaka 2 iliopita na kutamba mwishoni mwa wiki hii.Birmingham inalenga kubakia kati ya safu ya ngazi ya premier League.Arswenal pamoja na Chelea zinaifukuzia Manchester united kileleni mwa Premier League.



Nako kwenye Kombe la Dunia duru ya pili katika mzunguko waa kwanza wa kinyan'ganyiro cha kombe lijalo la Afrka la mataifa kwa wachezaji wanaocheza ligi za Afrika tu imerudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii:

Nigeria,ina kibarua kigumu mwishoni mwa wiki hii kufuta madhambi yao ya mabao 2:0 waliopigwa na jirani zao Niger katika duru ya kwanza ya kinyan'ganyiro hiki.
Hivyo, itabidi kupania kwani timu kadhaa za Afrika zinawania tiketi zao za kwenda Sudan,
ambako ndio kituo cha Kombe lijalo kwa timu za wachezaji wa ndani ya Afrika. Nigeria, imemsajili kwa Kombe hili,mtiaji wao mabao mengi katika ligi ya nyumbani: Ahmed Musa.Kwani, ni mizinga yake inayotarajiwa na mashabiki wa Nigeria duru hii ya pili kufuta mabao 2 ya Niger ya duru ya kwanza.

Mabingwa watetezi ni simba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na wameapa kuridi nalo Kombe Kinshasa.

Kongo ilitoa salamu zake na mapema katika duru ya kwanza ilipoikomea Gabon mabao 2:1.Gabon itajitutumua isimezwe tena na simba -mabingwa.Tanzania-kilimanjaro Stars, wana miadi na Somalia wakati jirani zao Malawi , wanaumana na Msumbiji .

Tembo wa Ivory Coast ambao wanatazamia mwishoni mwa wiki hii kumtangaza kocha wao mpya, wana miadi na Togo.Zimbabwe, inacheza na jirani zao Swaziland wakati Bafana Bafana au -Afrika kusini , inapambana na Botswana.Namibia inaikaribisha Seyschelles.

Majirani wengine uwanjani ni Uganda na Rwanda.Angola, iliokuwa mwenyeji wa Kombe lililopita la Afrika la Mataifa tofauti kabisa na hili, mapema mwaka huu,iko nyumbani ikiwakaribisha Wabuki- Madagaskar.Black Stars (Ghana), nyota yao nyeusi inan'gara mjini Accra, mbele ya Burkina faso.Siera leone inaumana na Senegal wakati Guinea, inacheza na Mali.Libya inaikaribisha nyumbani Algeria, mojawapo ya timu 6 za kombe lijalo la dunia ,kanda ya Afrika:

Tugeukie sasa Kombe lijalo la dunia nchini Afrika kusini litakalofunguliwa rasmi kwa mpambano kati ya wenyeji Bafana bafana na Mexico Juni 11.Kocha wa Ujerumani,
mojawapo ya timu zinazopigiwa upatu kutoroka na taji,Joachim Loew , ametangaza kwamba atataja kikosi chake kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika afrika kusini hapo mwanzoni mwa mwezi Mei.Amesema ameamua kutangaza kikosi chake wiki moja kabla msimu huu wa Bundesliga kumalizika hapo Mei 8.

.
Soma Zaidi ...

KENYA YAKATAA KUOKEA WASHUKIWA WA UHARAMIA

Kenya imekataa kuwapokea washukiwa watatu wa uharamia kutoka Somalia wanaoshikiliwa ndani ya meli moja wa wataliani pamoja na maiti ya mtu mmoja.

Polisi ya kenya imearifu kwamba jela pamoja na mahakama za nchi hiyo zimefurika.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kenya ambayo ni nchi pekee iliyoingia makubaliano na nchi za magharibi zilizopeleka wanajeshi wake katika mwambao wa Somalia kukabiliana na harakati za maharamia,kukataa kuwapokea watuhumiwa wa uharamia.

Mabaharia wa Meli ya Italia Scirocco,walipambana na washukiwa kadhaa wa uharamia katika pwani ya Somalia na baadae kuwazidi nguvu na kufanikiwa kuondoka na watuhumiwa watatu hadi katika bandari ya Kenya mjini Mombasa.

.
Soma Zaidi ...

UJUMBE MAALUM WA LEO


Assalaam alaikum Ommykiss, huu ujumbe nimeupenda sana.

IJuMaa KaReeM,

Maathir Hanad,

Dar-es-Salaam.

. Soma Zaidi ...

JK NA RONALDO, MKAPA NA WAANDISHI WA NJE


Na Johnson Mbwambo.

Nilijizuia mno nisiandike chochote kuhusu tukio la Jumanne ya wiki iliyopita ambapo Rais wetu, Jakaya Kikwete, ‘alizawadiwa’ jezi ya Ronaldo na Rais wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania, Florentino Perez.

Ilielezwa wakati wa hafla hiyo ya Ikulu kwamba bwana mkubwa huyo wa Real Madrid ameamua ‘kumzawadia’ Kikwete jezi hiyo ikiwa ni ‘kuthamini’ mchango wake katika kuinua kandanda (sijui ni kuinua Taifa Stars au Real Madrid!).

Picha za Kikwete akipokea jezi hiyo Na. 9 ya Ronaldo zilipamba kurasa nyingi za michezo za magazeti yetu nchini, Jumatano ya Machi 17. Naomba Mungu ili Kikwete asije, siku moja, kuivaa jezi hiyo; maana tumewahi kumwona Pinda akiwa amevaa fulana ya Vodacom!

Nasema nilijizuia sana nisiandike chochote kuhusu tukio hilo; japo nilipokea e-mail nyingi za wasomaji wangu wa Ughaibuni (wasomaji wa hapa nchini labda waliona ni tukio la kawaida) zilizoonyesha kukerwa kwao na tukio na picha hiyo.

Sababu za kujizuia nisiandike chochote kuhusu tukio hilo ni nyingi, lakini kubwa ni malalamiko kutoka kwa baadhi ya wana CCM kwamba namwandama mno Rais Kikwete katika safu yangu kwa mambo madogo madogo! Wanasahau kuwa katika maisha ni mambo madogo madogo ambayo mwisho wa yote hujenga picha kubwa ya hulka ya mtu.

Hata hivyo, uvumilivu huo uliniishia jioni ya Alhamisi iliyopita, Machi 18, nilipomsikia Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akihojiwa mjini Nairobi na BBC na kulalamika kwamba tatizo kubwa linaloikabili Tanzania ni ukosefu wa uzalendo!

Mkapa, ambaye alikuwa Kenya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Kampuni ya Nation Media Group, alitumia fursa hiyo kuwaponda sana waandishi wa habari wa Tanzania, na kujisifu kwamba yeye wakati wa urais wake alikuwa akipenda zaidi kuzungumza na waandishi wa habari wa nje!

Akizungumza kwenye ukumbi uliofurika wageni mbalimbali, wakiwemo Rais Kibaki na Rais Kagame, Bw. Mkapa aliwaponda waandishi wa Tanzania kwamba hawana uelewa wa kutosha wa masuala mbalimbali.

Hata hivyo, hiyo si mara ya kwanza kwa Mkapa kuwaponda waandishi wa habari wa Tanzania; japo safari hii amewaponda akiwa mbele ya marais wengine wawili (Kagame na Kibaki) ambao wao walisema katika mkutano huo kuwa wana kawaida ya kuzungumza na waandishi wa nchi zao!

Baadaye jioni, Bw. Mkapa alihojiwa na BBC kuhusu mahusiano ya waandishi wa habari na marais; hususan wa Afrika Mashariki, na ndipo aliposema kwamba mahusiano hayo ni muhimu lakini akasisitiza kuwa tatizo kubwa linaloyakwaza, ni ‘ukosefu wa uzalendo’. Karibu mara mbili tatu hivi wakati wa mahojiano hayo, Bw. Mkapa alirudia suala hilo la ‘ukosefu wa uzalendo’.

Ni kwa muktadha huo nashawishika leo kuyalinganisha matukio hayo mawili ya Nairobi na Dar es Salaam ya Bw. Mkapa na Rais Kikwete, kwa sababu, kwa mtazamo wangu, yafananafanana.

Wakati Mkapa anajisifu, mjini Nairobi, kwamba anapenda kuzungumza na waandishi wa habari wa nje na si wa Tanzania; huku hapo hapo akibainisha kwamba tatizo kuu linaloikabili nchi yetu ni ‘ukosefu wa uzalendo’; mjini Dar es Salaam nako Rais wetu Kikwete alikuwa akihudhuria, Ikulu, hafla ya kukabidhiwa ‘zawadi’ ya jezi ya mchezaji wa klabu ya Hispania – Ronaldo!

Kama ‘uzalendo’ ndiyo kigezo chetu kikuu cha kutathmini matukio hayo mawili ya Nairobi na Dar es Salaam; nashawishika kuuliza: Ni nani kati ya Kikwete na Mkapa tunayeweza kusema alionyesha uzalendo katika matukio hayo mawili tofauti?

Je, ni Kikwete anayekubali kukaribisha, Ikulu, hafla ya kukabidhiwa jezi ya mwanasoka wa Hispania (Ronaldo) au ni Mkapa anayejisifu ugenini kwamba yeye hupendelea kuzungumza na waandishi wa habari wa Ughaibuni tu (Ulaya na Marekani)?

Ndugu zangu; ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba, ni kweli tuna tatizo la ukosefu wa uzalendo; lakini wachangiaji wakubwa wa ukosefu huo wa uzalendo nchini mwetu, ni watawala wetu wenyewe.

Unapokuwa na rais wa nchi ambaye anakubali, katika hafla rasmi ya Ikulu, ‘kuzawadiwa’ jezi ya Ronaldo maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba anatuma ujumbe kwa vijana wetu wadogo mashuleni na hata kwa sisi wazee wazima, kwamba, hata kwenye michezo, nyota wa nje ndiyo wa kuwathamini na wa kuwapapatikia.

Kwa mtazamo wangu, ujumbe ulio dhahiri alioutuma ni ule wa kuthamini vya nje (vya wazungu), na si vya kwetu. Sasa kama hali ni hiyo, ni vipi tunaweza kujenga uzalendo kama hata viongozi wetu wenyewe wanawapapatikia na kuwatukuza wanamichezo wa nje, na si wa kwetu hapa nyumbani?

Naomba nieleweke vyema. Kikwete kama mtu binafsi ana uhuru wa kumshabikia Ronaldo na Real Madrid au mwanamichezo yoyote yule, lakini kama rais; si vyema kufanya hivyo hadharani, na tena katika hafla rasmi za Ikulu.

Kwa maana hiyo, ningemuelewa vyema Kikwete kama angekuwa anamshabikia Ronaldo kimya kimya sebuleni kwake.

Ningemuelewa kama angeipokea jezi hiyo kimya kimya sebuleni, na pengine kuigawa hapo hapo. Lakini kwa kulifanya tukio hilo kuwa ni rasmi; kiasi hata cha kuita wapiga picha; maana yake ni kwamba analithamini, analirasimisha na analipa kipaumbele!

Kinachogomba hapa ni pale anapoitumia Ikulu na urais kumshabikia mwanasoka wa nje - Ronaldo. Usisahau kwamba huyu ni rais wa nchi, na kila alifanyalo katika hafla rasmi inayofanyika Ikulu, anakuwa ni kioo cha Taifa – kioo cha uzalendo wetu sote ndani na nje ya nchi.

Inapotokea Rais mwenyewe anamshabikia Ronaldo hadi kwenye hafla rasmi ya Ikulu, ni dhahiri wajibu huo wa kuwa kioo cha uzalendo wetu sote ndani na nje ya nchi unadhoofika.

Labda ni kwa sababu ya hulka hizo za watawala wetu za kupapatikia vya nje, hatupaswi kushangaa kuiona televisheni yetu ya taifa (TBC) ikionyesha ‘live’ mechi za Ligi Kuu ya Uingereza, lakini haifanyi hivyo kwa mechi za Ligi Kuu yetu ya hapa nyumbani. Kuna uzalendo gani tunaweza kuujenga kwa kuonyesha ‘live’ ligi ya nje badala ya ligi ya nchi yetu wenyewe?

Aidha, kwa kitendo kile cha Kikwete cha kupigwa picha Ikulu akipokea jezi Na. 9 ya Ronaldo, na picha hiyo kuchapishwa na magazeti na kuingizwa kwenye tovuti mbalimbali duniani, Rais Kikwete ametumika kutangaza, kote duniani, biashara ya Real Madrid ya kuuza jezi Na. 9 ya Ronaldo! Kwa maneno mengine, ni endorsement ya bure kabisa ya kibiashara ya Rais wetu kwa jezi namba 9 ya Ronaldo!

Sasa hapo ni uzalendo gani aliouonyesha Kikwete kwa Watanzania kwa kukubali ‘zawadi’ ya jezi ya mwanasoka huyo wa kigeni? Hata kama amefanya hivyo ili eti kuishawishi Real Madrid ije nchini, sote tunajua kwamba timu hiyo haina “udugu” na nchi yoyote duniani, na kwamba inachojali ni kutengeneza mapesa tu. Itakuja nchini kama italipwa mapesa inayotaka, na itakwenda hata Bermuda kama ikilipwa mapesa inayotaka.

Kwa mtazamo wangu, hali ingekuwa ni tofauti kama jezi aliyoipokea Kikwete, Ikulu, ingekuwa ni ya yule Mtanzania mwenzetu anayeng’ara nchini Marekani katika ligi ya mpira wa kikapu ya NBA, Hasheem Thabeet. Hapo, uzalendo ungekuwepo, na hata uhalali wa kuvaa T.Shirt yake ungekuwepo.

Ni kwa msingi huo naelewa ni kwa nini Watanzania wengi wanaoishi Uingereza ndiyo walionitumia e-mails za kuonyesha kukerwa na suala hilo la Kikwete na jezi ya Ronaldo. Walikiona kitendo hicho kuwa hakichochei Watanzania kujenga utaifa na uzalendo kwa taifa lao, kwa sababu hakitangazi u-Tanzania.

Nawafahamu baadhi ya Watanzania hao. Baadhi yao ni wale wanaodiriki kusafiri kilomita nyingi, jijini London, mwishoni mwa wiki, kufuata baa ya Mhindi mmoja inayouza bia aina ya Serengeti. Watanzania wale hujisikia raha mno wanapokunywa bia ya nyumbani Tanzania katika baa ya London iliyojaa Wazungu - bia yenye chupa iliyoandikwa “brewed in Tanzania”!

Naamini ni uzalendo tu ndiyo unaowatuma kufanya hivyo ugenini, na kama ndivyo, basi, lazima uielewe hasira yao wanapoona picha ya rais wao akikabidhiwa jezi za mchezaji wa kizungu wa Ulaya, na si jezi ya Mtanzania mwenzao, Hasheem Thabeet! Si ilisemwa ya kwamba: Mcheza kwao hutuzwa?

Tukirejea kwa ya Mkapa; ya kwake hayana hata mjadala mkubwa. Huwezi kuwathamini waandishi wa nje na kuwapuuza wa nchini mwako, na kisha ukajitia wewe ni mzalendo.

Huwezi kukaa Ikulu, kwa miaka 10, kama rais wa nchi na usifanye lolote kujenga uzalendo, na kisha unapotoka Ikulu ndipo ulalame kwamba tatizo letu kubwa ni kukosa uzalendo! Alifanya nini kujenga uzalendo alipokuwa rais?

Huwezi kukaa Ikulu kwa miaka 10 na kuongoza serikali iliyogubikwa na ufisadi wa kila aina (EPA, Meremeta, Deep Green nk); huku mwenyewe ukituhumiwa kununua kampuni ya umma (Kiwira) kwa bei ya kutupa, na kisha ukitoka Ikulu ulalame kwamba hakuna ‘uzalendo’ nchini! Ni uzalendo gani anaomaanisha Mkapa?

Kama hata waandishi wenyewe wa Tanzania hawapendi, na anaowapenda ni wa Ughaibuni, angewezaje kuujenga huo uzalendo kwa Watanzania wakati wa kipindi chake cha urais?

Isitoshe, hivi Mkapa hajui kwamba ni vigumu mno kujenga uzalendo katika nchi ambayo imegawanyika katika matabaka mawili makuu ya walichonacho na wasichonacho?

Hivi katika mazingira yetu hapa Tanzania; mtoto wa mkulima masikini na mtoto wa mfanyabiashara tajiri wanaweza kweli wakachangia maana ile ile ya uzalendo? Nina shaka.

Hivi Mkapa hajui kwamba tafsiri ya neno ‘mzalendo’ inazidi kupoteza maana yake hapa Tanzania; kiasi tunavyojenga jamii isiyo na haki, jamii ambayo wachache hufaidika vilivyo na keki ya taifa; huku walio wengi wakiogelea katika lindi la umasikini?

Hivi Kalimanzira na Patel Khulibhai wanaweza kweli kuchangia tafsiri moja na maana ile ile ya neno ‘mzalendo’? Nina shaka.

Ndugu zangu, ni kweli tuna tatizo la ukosefu wa uzalendo, lakini viongozi wetu hawa wa zama hizi hawawezi kukwepa lawama za kuhusika na kuongezeka kwa tatizo hilo. Viongozi wanapotumia nafasi zao za uongozi kujitajirisha, kamwe hawawezi kuwa na utashi wa kuujenga uzalendo.

Nihitimishe kwa kusisitiza kwamba uzalendo hushamiri tu kwenye nchi yenye misingi ya haki na inayotoa fursa sawa kwa wote. Kwa maana hiyo, uzalendo utazidi kuota mbawa nchini; kiasi tunavyozidi kupanua wigo wa walichonacho na wasichonacho, na kiasi watawala wetu wanavyozidi kuwapendelea wale walichonacho na kuwatelekeza wanyonge.

. Soma Zaidi ...

YAHYA HUSSEIN AJA NA "UZUSHI" MPA

Mtabiri maarufu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein ameibuka na utabiri mpya kuwa mwaka huu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani hautafanyika kama ilivyopangwa.

Sheikh Yahya alitoa utabiri huo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Hata hivyo, alipotakiwa na waandishi kutoa maelezo zaidi kuhusu utabiri huo alisema kwamba anapotoa utabiri hatakiwi kutolea majibu.

Aidha alisema baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo tofauti na utabiri wake huku wengi wakidhani anatumiwa na viongozi wa kisiasa.

“Kwanza napenda kuwafahamisha kwamba mimi ninapotoa utabiri wangu huwa simlengi mtu wala simtabirii mtu, natoa utabiri kwa manufaa ya jamii. Kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu aidha kukubali au kukataa haya ambayo ninayasema,” alisema Sheikh Yahya.

Alisema kwa upande wa Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume ataendelea kuongezewa muda wa kutawala tofauti na wengi wanavyofikiria.

Kuhusu Bunge, mtabiri huyo alisema bunge lijalo litakuwa na sura nyingi mpya huku wanawake wakiongezeka kwa idadi kubwa wakati robo tatu ya wabunge wa zamani watapoteza nafasi zao.

Sheikh Yahya, alisema kinyota watu watakaokuwa na bahati ni wale wanaoanzia na herufi za majina ya ‘S’.

Kutokana na hali hiyo, alisema nyota ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta itaendelea kung’ara na kwamba hakuna mtu atakayemchezea katika masuala ya siasa.

Alisema kitendo cha kupatwa kwa jua Januari 15, 2010, kunaashiria kuwepo kwa vurugu, umwagikaji wa damu, harakati za kijeshi na kashfa za kipolisi, mabadiliko ya uongozi katika ngazi mbalimbali, uasi wa ghafla katika serikali za nchi ambazo zilipitiwa na kupatwa kwa jua.

“Nchi za Chad, Somalia, Tanzania, Kisiwa cha Zanzibar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kenya, India, Sri Lanka, Bangladesh na Mayanmar ndizo zilizopitiwa na kupatwa kwa jua vile vile kutokea vurugu za uchaguzi katika nchi hizo, watu kufanya maasi na matukio ya kigaidi,” alisema Sheikh Yahya.

Akizungumzia kuibuka kwa Chama Cha Jamii (CCJ), alisema kitakuwa kimedhamiria kukimaliza Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini jamii inatakiwa kufahamu kuwa CCM itaweza kuvunjwa na wanachama wenyewe na si chama chochote cha siasa.

“CCJ ilitakiwa kutafuta ushauri wa kinyota. Iwapo CCJ ingejiita CCN hapo kungekuwa na uwezekano wa kuishinda CCM, lakini kutokana na kukosea kuchagua herufi basi chama hicho hakikiwezi kabisa chama tawala hata wakitumia jina la Baba wa Taifa Julius Nyerere,” alisema.

Sheikh Yahya ameibuka na utabiri huo baada ya hivi karibuni kutabiri kuwa kama kuna mwanachama au mwanasiasa atayakayejitokeza ndani ya CCM kumpinga Rais Jakaya Kikwete katika mbio za urais mwaka huu, atakufa ghafla.


.
Soma Zaidi ...

Thursday, March 25, 2010

10 WAFA PAPO HAPO KWENYE AJALI TANZANIA


Watu 10 wamekufa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea nje kidogo ya mji wa Daresalaam, alfajiri ya kuamkia leo.
Ajali hiyo ilihusisha basi dogo la abiria na Lori la mafuta.

Walioshuhudia wanasema gari hizo ziligongana uso kwa uso na baadaye Lori kupinduka na kuliangukia basi hilo dogo.

Ajali hiyo ilitokea saa kumi za alfajiri katika eneo la Kibamba kilomita 20 nje ya jiji la Dar es salaam.

Kamanda mkuu wa kikosi cha barabarani Muhamed Mpinga amesema ilikua vigumu kutoa miili ya waliokufa kutokana na jinsi basi hilo dogo lilivyopondwapondwa.

Miili tisa ilitolewa baada ya kunyanyuliwa kwa lori hilo.

Kamanda huyo anasema inaelekea dereva wa lory hilo alishindwa kulidhibiti.

Inasadikiwa Abiria wengi waliokuwa wanasafiri katika basi dogo walikuwa ni wafanyibiashara wadogo wadogo waliokuwa wakiwahi kuchukua bidhaa katika soko la Kariakor.

Kutokana na ajali hiyo, barabara zilifungwa na safari kutoka Dar es salaam kwenda mikoani zikasimamishwa kwa muda, hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari.
.
Soma Zaidi ...

SERA YA MAKAAZI YA ISRAEL YAZIDI KUPINGWA

Mpango wa kutafuta amani mashariki ya kati sasa umewekwa njia panda kutokana na tangazo la Israel la kupanua makazi ya walowezi katika eneo la Mashariki ya Jerusalem, huku viongozi wa magharibi wakitakiwa kuchukua hatua.

Akionya juu ya hatua hiyo ya Israel Mfalme wa Jordan Abdullah wa pili ametahadharisha kuwa mpango huo wa kutafuta amani uko njia panda kwa sababu watu wamechoshwa na mchakato usiokwisha katika kupatikana kwa amani katika eneo hilo, hali ambayo haipelekei matokeo yoyote

Katika mahojiano yake na Wahariri wa vyombo vya habari mjini Amman, Mfalme Abdullah amesema anafikiri kuwa dunia nzima inakabiliwa na ukweli kwamba,
tunapigania hatua za kweli, hatua wazi na za haraka kuutatua mzozo huu kwa ufumbuzi wa mataifa mawili, ama kuingia katika mzozo mpya na machafuko ambayo yataathiri ulimwengu mzima.

Kwa upande wake msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran Ramin Mehmanparast amesisitizia umuhimu wa nchi za magharibi kuichukulia hatua Israel na kuongeza kuwa hatua itakazochukua zisiwe tena za maneno bali ziwe za vitendo.

Ameyakosoa vikali pia matamshi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba matakwa ya kutaka ujenzi huo wa makaazi usitishwe hayana msingi na kwamba Jerusalem siyo makaazi ila ni mji mkuu wao.

Viongozi mbalimbali wa nchi za magharibi ikiwemo Ujerumani tayari wametoa kauli kuhusiana na tangazo lake hilo la kupanua makaazi.


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hillary Clinton alisema kuendelea kwa ujenzi huo kunahatarisha kupatikana kwa amani katika eneo hilo

Amesema ujenzi mpya katika Jerusalem ama ukingo wa magharibi unahujumu hali ya kuaminiana ya pande mbili na kuhatarisha mazungumzo yaliyokaribu ambayo ni hatua ya kwanza kuelekea mapatano kamili ambayo pande zote mbili zinasema zinayataka na kuyahitaji.

Kwa upande mwingine, Msemaji wa Mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Ghassan Khatib
akielezea kitendo hicho cha Israel kutetea ujenzi huo, amesema ni uvunjaji wa sheria za kimataifa na kwamba matamshi ya hivi karibuni ya waziri Mkuu
Netanyahu ambayo yanaahidi kuendelea na ujenzi haramu wa makaazi ya walowezi katikia Jerusalem ya mashariki ni ya kusikitisha.

Serikali ya Israel jana ilitoa ruhusa ya ujenzi wa nyumba mpya 20 mashariki mwa Jerusalem.

Tangazo hilo limekuja katika siku ambayo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa amekutana na Rais Barack Obama wa Marekani mjini Washngton, ikiwa uhusiano wa nchi hizo mbili umetikiswa vibaya na sera hiyo ya makaazi ya Israel.
.
Soma Zaidi ...

BIN LADEN AONYA KUUWA WAMAREKANI

Kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida, Osama bin Laden, ameonya kuwa mtandao huo utawaua Wamarekani, iwapo kiongozi wa maandilizi ya mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, Khaled Sheikh Mohammed, atanyongwa.

Katika ujumbe alioutoa kupitia mkanda wa video, na kurushwa na kituo cha televisheni cha Al Jazeera, Osama bin Laden pia amemuonya Rais wa Marekani,
Barack Obama kuwa anafuata nyayo za mtangulizi wake George W Bush kwa kuendelea na vita nchini Afghanistan.
Kitengo cha kupambana na ugaidi nchini Marekani kimesema mkanda huo unaonekana kuwa halisi.

Marekani katika wiki chache zijazo itafikia uamuzi iwapo mtuhumiwa huyo na washirika wake wanne, washtakiwe katika mahakama ya kiraia au kijeshi.

Utawala wa Rais Obama umetangaza kuwa kesi yao itasikilizwa katika mahakama ya mjini New York Marekani iliyoko mita chache tu kutoka mahali palipokuwa jengo la kituo cha kimataifa cha biashara ambalo lilibomolewa na mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001.
.
Soma Zaidi ...

APRILFOOL, 2010

Wazee wetu, Ndugu zetu,

Assalaam Alaaykum

UMOJA, UHURU, UADILIFU

Wazanzibari Tushikamane Tugombea Wattani Wetu

Aprilfool, April 1964

Wazanzibari tulifanyiwa Aprilfool siku ile ya April 24, 1964 pale Nyerere kwa mbinu zake ovu alipomlaghai Mzee Karume na kuleta zile Articles of Union, 1964; akaimeza na kuifutisha Dola Huru ya Zanzibar kwa huu wenyekuitwa muungano.

“Articles of Union, 1964”,

a. The Constitution and Government of the United Republic;

Katiba na Sirikali ya Jamhuri ya Muungano

b. External Affairs;

Mambo ya Nje

c. Defence;

Jeshi


d. Police;

Polisi


e. Emergency Powers;

Uwezo wa kutangaza hali ya khatari


f. Citizenship;

Uraia


g. Immigration;

Uhamiaji


h. External trade and borrowing;

Biashara za nje na mikop0


i. The Public service of the United Republic;

Utumishi wa Sirikali ya Jamhuri ya Muungano


j. Income tax, corporation tax, customs and excise;

Mapato, kodi, kastamu


k. Harbours, civil aviation, posts and telegraphs;

Bandari, huduma za anga, posta na telegram


Vifungu Kumi na Moja hivi ni Utiwamgongo wa Nchi

Hapana shaka sote tunatambuwa kwamba mambo kumi na moja haya ndio utiwamgongo wa Dola yoyote ile, bila ya haya haiwi Dola. Vifungu hivi vimekuwa vikiongezwa na Tanganyika mara baada ya mara bila ya hata kushauriwa, licha ya kuwafiqiwa na Zanzibar. Muhimu mno katika vifungu vilivyo ongezwa ni “Ilimu ya Juu, “Higher Education”. Mafuta, gesi na mali asili hapana shaka ni katika mambo muhimu, ni uchumi wa Nchi. Kuongezwa huku huwa ni kwa kutolewa katika Sirikali ya Zanzibar na kutiwa katika Sirikali ya Tanganyika.

Wazalendo wa Kizanzibari Hawataridhia

Tangu sikumosi ya khiyana hii kuu Nyerere aliotufanyia Wazanzibari, Wazalendo wa Kizanzibari wamekanya vikali uovu huu. Wazalendo wa Kizanzibari wataendelea kukanya uovu huu na kufanya kila waliwezalo kuhakikisha kwamba Dola Huru Kaamili ya Zanzibar inarejea kama ilivyokuwa siku ile ya December 10, 1963 ilipopata Uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Wazalendo Unajidhatiti

Kwa kukaribia siku hii, siku ya giza, siku Zanzibar ilipofanyiwa Aprilfool, Umoja wa Wazalendo unajidhatiti kuendeleza harakati za kuikataa dhulma hii na kuwania kurejea Dola Huru ya Zanzibar. Umoja wa Wazalendo unawanadia Wazanzibari tushikamane na kwa umoja wetu tuendeleze harakati za ukombozi wa Nchi yetu, Zanzibar kutokana na ukoloni wa mvamizi mkoloni Tanganyika.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala atujaalie kila kheri na atuepushe na kila shari na atujaalie ufunguzi wa karibu, Aamyn.

Wa Billahi Tawfiiq

Umoja wa Wazalendo

Zanzibar, March 25, 2010

.
Soma Zaidi ...

KWA WANYE WATOTO WADOGO

Kutokana na ugumu wa maisha wachina wamevumbua hii njia mbadala ya matumizi ya Pampers kwa watoto. Soma Zaidi ...

MWANAMKE MWENYE LENGO LA KUA MNENE KULIKO WANAWAKE WOTE DUNIANI


Donna akiwa na mwanawe wa kike Jacquline akimsaidia kufanya Shopping kwenye Supper Market moja huko New Jersey
Aanaitwa Donna Sampson ana umri wa miaka 42 mkaazi wa New Jersey huko Marekani, kwa sasa ana uzito wa kilo 273 huku matumaini yake ni kuwa mara mbili ya unene alionao hivi sasa ili awe mwanamke mnene zaidi ya wote duniani.Dona ambae uwezo wake wa kutembea kwa miguu hauwezi kupindukia zaidi ya 20ft huwa anatumia kigari kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake, licha ya unene alionao lakini aaonekana ni mwenye afa njema. Soma Zaidi ...

Wednesday, March 24, 2010

TANGU LINI UWELEWANO UKAPIGIWA KURA YA MAONI?



• Wengi wakikataa, ina maana uhasama uanze upya?
• Wenye uchu wa madaraka wamejaa Zanzibar na dunia nzima

Na Walusanga Ndaki

JE -- kwa msomaji wa makala hii – uliwahi kuona wapi watu wanaoamua kuheshimiana na kuelewana wakalazimishwa kupiga kura ya maoni?
Vilevile – jambo muhimu zaidi – iwapo kura ya maoni itaonyesha kwamba watu wengi hawataki maelewano kwa kupitia serikali ya mseto nchini Zanzibar, je huo ndiyo uwe mwisho wa maelewano baina ya watu wa visiwa hivyo?
Je, baada ya kura maoni kukataa maelewano, wanasiasa wa Zanzibar ambao hivi sasa wanakazania sharti ifanyike kura ya maoni, watafanya nini?...

Wataanza kuwaambia wananchi kwamba kwa vile kura ya maoni kuanzisha serikali ya mseto imekataa jambo hilo, kwa hiyo waendelee na uhasama wao kama ilivyokuwa huko nyuma?
Kama si hivyo, nia yao hasa ni nini ya kuwauliza watu kwa kura kuhusu jambo lenye kuleta heri kwa wote?
Je, kuna watu wanaogopa kukosa vyeo katika Zanzibar mpya ambapo “ulaji” wa kupitia siasa utabidi kugawanywa katika mikono mingi zaidi?
Kama si hivyo, nia ya kura ya maoni ni ya nini?

Je, wakati wa kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika, au wakati wa kuuganisha vyama vya Afro-Shiraz na TANU, wananchi wa Zanzibar – na wa Bara – waliulizwa kuhusu mambo hayo ambayo yalikuwa muhimu zaidi ya hili la kuleta uelewano na kuunda serikali ya mseto?
Hawa wanasiasa wanaong’ang’ania kura ya maoni leo hii – wengi wao wakiwa watu wazima wakati hayo yanafanyika -- hawakuwepo wakati huo na wakaitoa hoja kama hiyo ya kura ya maoni? Mbona walikaa kimya wakati huo? Au hivi sasa siasa zimekuwa za “mteremko mno?”

Maswali au kauli kama hizi zimetawala kuhusu Muswada wa Kura ya Maoni Zanzibar ambayo wanasiasa wanafiki wamekuwa waking’ang’ania ifanyike katika visiwa hivyo kabla ya kuundwa kwa serikali ya mseto!
Wananchi wengi nchini Tanzania, wenye nia njema kwa Wazanzibar na wengine kokote waliko duniani, wamesema wazi kupiga kura ya maoni kwa watu ambao maelewano yatawaletea neema na faida nyingi, ni jambo la kupoteza muda na fedha.

Hii ni kwa kutia maanani kwamba kura kama hiyo – kwa mategemeo ya wanasiasa wajuvi -- inaweza ikapigwa kwa misingi ya ushindani wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) na kuzaa matokeo ambayo siku zote yamechochea kuleta uhasama visiwani humo.
Kwa faida tu ya wasomaji, Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar leo.
Kwa ufahamisho wa wasomaji wa tovuti hii, hii ni mara ya pili kwa mwandishi wa makala hii, kupinga kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu kuanzishwa kwa serikali ya mseto nchini Zanzibar kwani ni jambo la unafiki wa kisiasa na ni la kupoteza muda.

Kwa kweli – kwa watu wanaowaheshimu wananchi wenzao na kuwachukulia kwamba nao pia wana busara – kura hiyo ya maoni ambayo wanasiasa kadhaa wameng’ang’ania ifanyike -- ni jambo la kipuuzi!
Halina faida yoyote kwa mwenye nia njema na hali ya Zanzibar. Kinyume chake, wale wanaotaka kukwepesha serikali ya mseto -- hasa wanasiasa wa Tanzania Bara na “washikaji” zao wa Zanzibar – watakuja kujuta na kuona aibu kwa kung’ang’ania kitu ambacho hata watoto wa shule za msingi wanakiona ni kichekesho!

Jambo hili halihitaji maelezo marefu hasa kwa Wazanzibar kujua kilicho bora na kilicho kibaya kwao.
Makala hii inasisitiza tena kwamba matatizo ya Zanzibar yataisha tu pale Wazanzibar watakapong’amua kuwa kitu kimoja na kuanza kuamua kile kilicho muhimu kwao kwanza badala ya kuwafurahisha watu walio nje ya visiwa hivyo, watu ambao uchungu wa uhasama visiwani humo hawaujui!

Wazanzibar wanaoendekeza ushabiki wa kisiasa kwa kuwasikiliza wanasiasa wanaoishi nje ya visiwa hivyo, hususani wale wa bara, ni dhahiri watakuja kujilaumu siku moja, kwani moto wa kweli wa uhasama ukiibuka visiwani humo ni wao na familia na marafiki zao ambao watapiga magoti kuomba amani ambayo leo wanaikwepa.

Wenye uchu wa madaraka wamejaa Zanzibar, Tanzania Bara na dunia nzima – wote wakiwa ni wanasiasa wanaotegemea kuishi kwa kuwalaghai binadamu wenzao!
Wazanzibar wajifunze kuamua kilicho muhimu kwao kwanza –- wasikubali kuwafurahisha wanasiasa wa Tanzania Bara au kwengineko duniani!
Wasipofanya hivyo leo, wajue watakuja kujuta kwani watakuwa wamechelewa kufanya jambo lolote lenye heri kwao kwa kupoteza muda wao wakiwasikiliza wapiti njia!

.
Soma Zaidi ...

MPOKI: ZANZIBAR SIO TANZANIA

Soma Zaidi ...

NETANYAHU AKUTANA NA OBAMA

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewasili katika Ikulu ya Marekani ya Whitehouse atakakokutatana na Rais Barack Obama.

Rais Obama na bwana Netanyahu wanakutana kwa mara ya kwanza tangu serikali za Marekani na ile ya Israeli kutofautiana hadharani hivi karibuni, kuhusu mpango wa Israeli wa ujenzi wa makazi mapya ya wayahudi mashariki mwa Jerusalem.

Mkutano huo unafanyika baada ya Waziri Mkuu Netanyahu kulihutubia bunge la
Marekani alikosisitiza kuwa mchakato mzima wa kutafuta amani ya Mashariki ya Kati ya kudumu huenda ukakwama kwa mwaka mmoja mwengine ikiwa Wapalestina hawatolitupilia mbali dai lao la kusimamishwa kabisa ujenzi wa makazi ya walowezi.

Wakati wa ziara yake nchini Marekani Bwana Netanyahu amerejelea kile alichosema ni haki ya Israeli ya kujenga mjini Jerusalem.

''Jerusalem ni mji mkuu wa Israeli na si makazi'', alieleza Bwana Netanyahu.


Awali, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo wa nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa jumla zinaamini kuwa sera ya Israel ya kuendelea kuyaongeza makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika eneo la Jerusalem Mashariki inazirudisha nyuma hatua zozote zile za kufikia amani ya Mashariki ya Kati.

.
Soma Zaidi ...

CHELSEA CLOSE ON £10M VAN


Boss Carlo Ancelotti has been tracking Real Madrid's £10m Dutch playmaker for several months.

Talks with the representatives of the player have already begun about a move to Stamford Bridge this summer.

Ancelotti is keen to play Van der Vaart, 27, in his diamond midfield behind the two strikers.

The Dutch ace is widely regarded as one of the most creative players in Europe but has been frozen out at Real.

Chelsea are keen to finalise a deal before the World Cup finals as they fear Van der Vaart's price will rocket if he does well.

With Deco destined to go home to Brazil next season, Ancelotti wants a reliable ball player to supply his strikers.


.
Soma Zaidi ...

Tuesday, March 23, 2010

ISRAEL NA MPANGO WAKE WA KUJENGA MAKAAZI ZAIDI MASHARIKI MWA JERUSALEM


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema mpango wa serikali ya Israel wa kujenga makaazi zaidi ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa Jerusalem utayahujumu mazungumzo na wapalestina.

Lakini waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kuwa nchi yake ina haki ya kujenga katika mji huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema hali iliyopo sasa kati ya Israel na Wapalestina haiwezi kudumishwa katika upande wowote kwa sababu hali hiyo inatishia kusababisha umwagikaji damu zaidi na kuzuia shabaha zinazolengwa.

Akizungumza mjini Washington kwenye mkutano wa jumuiya inayoyapigia debe maslahi ya Israel nchini Marekani bibi Clinton aliiambia Israel kuwa ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi mashariki mwa mji wa Jerusalem unaihujumu hadhi ya Marekani kama msuluhishi wa kuaminika anaepaswa kuwa tayari kupongeza, na ikibidi kulaani vitendo vya kila upande katika mashariki ya kati.

Waziri Clinton aliwaambia wajumbe kwenye mkutano huo kwamba Marekani illipaswa kulaani ujenzi wa makaazi mapya mashariki mwa Jerusalem na kwenye Ukingo wa Magharibi ili kulinda uaminifu wake na kuhakikisha mazungumzo baina ya Israel na wapalestina yanasonga mbele.

Lakini amewaambia waisraeli na wapalestina kuwa hali iliypo sasa haiwezi Waziri wa mambo ya nje Bibi Hillary Clinton asema hali ya Israel na Palestina inatishia umwagikaji wa damu

Bibi Hillary Clinton asema hali ya Israel na Palestina inatishia umwagikaji wa damukudumishwa.

Amesema hali hiyo inatishia kusababisha umwagikaji wa damu na hadaa ya malengo yasiyoweza kufikiwa. Hata hivyo waziri Clinton amesema ipo njia nyingine.

Lakini ipo njia nyingine inayoongoza kwenye amani na neema, kwa Israel, wapalestina na watu wote wa eneo la mashariki ya kati.

Hata hivyo pande zote ikiwa pamoja na Israel zinapaswa kufanya maamuzi magumu lakini ni ya lazima.

Lakini akizungmza kwenye mkutano wa kila mwaka wa jumuiya inayoyapigia debe maslahi ya Israel nchini Marekani, AIPAC, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema kuwa Jerusalem siyo sehemu ya kulowea bali ni mji mju mkuu wa Israel.

Netanyahu ameeleza kuwa wayahudi walikuwa tayari wanaujenga mji huo miaka alfu 3 iliyopita na kwamba wanaendelea kuujenga leo.

Waziri mkuu huyo ameeleza kuwa anafuata sera za serikali zote za Israel tokea mwaka 1967 baada ya Israel kushinda vita dhidi ya jirani zake wa kiarabu na kuiteka sehemu ya mashariki y a mji wa Jerusalem.

Ujenzi wa makaazi zaidi mashariki mwa Jerusalem na kwenye Ukingo wa Magharibi unaivuruga hali ya kuaminiana na unayatia mashakani mazungumzo-japo siyo ya ana kwa ana.

Bibi Clinton amesema mazungumzo hayo ndiyo msingi wa kuelekea kwenye mazungumzo kamili ambayo kila upande unayataka. Clinton amesema ujenzi wa makaazi mapya pia unahujumu fursa pekee ya Marekani ya kutoa mchango muhimu katika juhudi za kuleta amani.

.
Soma Zaidi ...

MUSWADA KURA ZA MAONI ZANZIBAR WAPINGWA

Wakati muswada wa Sheria wa kuanzishwa kwa Serikali ya Mseto visiwani hapa, ukitarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi unaotarajiwa kuanza kesho, maoni dhidi ya muswada huo yameongezeka.

Idadi kubwa ya wakazi wa hapa wakiwamo wanachama wa CCM, wasomi na wanasheria kama vile Awadh Ali Saidi, wameendelea kusisitiza kuwa kuupigia kura za maoni muswada huo, ni kupoteza fedha na muda kwa kuwa tayari Baraza la Wawakilishi lilishatoa uamuzi kwa niaba ya Wanzibari, kuwa na
Serikali hiyo iundwe baada ya uchaguzi mkuu.

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Abdallah Omar na Profesa Issa Shivji, pia waliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari wakihoji umuhimu wa kupiga kura ya maoni.

Wazo la kupiga kura hiyo lilitolewa Januari mwaka huu na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakari Khamis Bakari na kupitishwa na Baraza ili kuwapa nafasi Wanzibari kuamua kuwa na Serikali ya mseto au la.

Muswada huo wa Sheria ya Kura za Maoni wa mwaka 2010 unatarajiwa kuwasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi,
Hamza Hassan Juma, ili wajumbe wa Baraza waujadili na ikiwezekana upitishwe na kuanza kutumika mara Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, atakapousaini.

Aidha, Muswada huo utaipa uwezo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kusimamia upigaji kura hizo ikiwa ni pamoja na kupanga tarehe na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki.

Kwa mujibu wa muswada huo, ni Wanzibari waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura tu, ndio watakaopiga kura ya kuulizwa ana kujibu ndio au hapana na gharama za shughuli hiyo zitabebwa na Wizara ya Fedha.

“ZEC ndio watakaotangaza matokeo na kama kutatokea shaka katika matokeo hayo, haitatiliwa maanani na kama ikitokea matokeo hayo yakafungana,
Tume itatangaza tarehe nyingine katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya matokeo hayo, kwa ajili ya upigaji kura mwingine,” Muswada huo unaeleza.

Hata hivyo, Mzanzibari aliyepiga kura anaruhusiwa kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar. “Uamuzi wa mahakama hiyo ndio utakuwa wa mwisho na hakuna rufani itakayokubaliwa katika Mahakama ya Rufani,”

Lakini kabla ya mtu kukata rufaa dhidi ya matokeo ya upigaji kura huo, atatakiwa kwanza kuwa na wapiga kura 10 kutoka kila mkoa visiwani hapa, wanaomuunga mkono na kulipa Sh milioni tano kwa ajili ya kufungulia kesi siku 30 baada ya matokeo kutangazwa.

Muswada huo ambao unasubiriwa kwa hamu pia unaeleza kuwa itakuwa ni kosa kwa mtu au taasisi kutangaza matokeo ya kura hizo kabla ya ZEC na unapendekeza faini ya kati ya Sh milioni moja hadi 10 au kifungo cha miaka mitatu jela au adhabu zote kwa pamoja.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee, alisema jana kuwa katika mkutano huo, kutawasilishwa pia miswada mingine minne ukiwamo wa Haki na Wajibu wa Mwanasheria Mkuu na Wanasheria wote wa Serikali ambao unatarajiwa kujadiliwa kwa siku mbili.

Pia alisema jumla ya maswali 104 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa katika kikao hicho. Miswada mingine ni pamoja na wa Sheria ya Uvuvi, wa Sheria ya kuanzisha Baraza la Taifa la Michezo na wa Kuanzisha Mamlaka ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe.

***Habari Leo


.
Soma Zaidi ...

BAO HAPO NJIA MBILI

Wazee wetu, Ndugu zetu

Assalaam Alaykum

UMOJA, UHURU, UADILIFU

Nini Makusudio ya Bao Hili

Ukifika njia mbili, meli kumi ukielekea Mkokotoni kutoka mjini Zanzibar; kuna saruji (bao) limeandikwa, “Coral Cave and Slave Chambers”. Maneno haya tunaweza kuyatarjimu kama hivi, “Pango la Pwani na vyumba vya watumwa”. Hivi ni kueleza kwamba huko Mangapwani kuna pango ambalo wakiwekwa watumwa. Hivi pia ndivyo wanavyoeleza wale wanaofuatana na watalii kufika kwenye hilo pango. Inasikitisha sana kuona uwongo huu mpaka hii leo bado inatiwa kwenye vichwa vya wageni, bali zaidi wananchi wenyekuishi na kupita njiani hapa kila siku. Zanzibar yamejaa ya uwongo kama haya. Suala ni nini makusudio ya yote haya? Tujaalie haya yenye kuelezwa ni kweli, jee ni sisi kutafakhari kwa haya. Hapana shaka hili si lakutafakhari nalo na kufika kuweka bao njiani kueleza hili, bali ni kuona haya na aibu.


Kujenga Chuki Baina ya Binaadamu

Bao hili, hapana shaka halina isipokuwa kupandikiza chuki baina ya binaadamu kwa uwongo usiokuwa na msingi. Ziada ya uwongo uliojengwa na kupaliliwa kila siku, hili bao ni kuzidisha chuki hizi. Vipi tunapiga makelele kwa kusema “Umoja na Mshikamano”, haya ni maneno, lakini vitendo ni hili bao, bao linajenga chuki, maneno yanasema tuwe wamoja. Hapana shaka vitendo vinanguvu kuliko maneno.


Tunaomba Sirikali Iliondoe Bao Hili

Ili tujiepushe na aibu hii, aibu ya kutilia nguvu uwongo usiokuwa na misingi, na aibu ya kujenga chuki ambazo zinavunja umoja baina ya binaadamu, tunaiomba Sirikali ya Zanzibar ichukuwe khatuwa za haraka kuliondoa bao hili.


Wa Billahi Tawfiiq


Farouk

March 22, 2010

.
Soma Zaidi ...

CHELSEA MANCHESTER CITY WAMTOLEA MACHO DAVID VILLA



Timu ya Valencia wanaweza wakajitilia kibindoni kiasi cha Peund za Kienereza 60m kwa kuwauza wachezaji wake wawili ikiwa ni pamoja na mshambuali wake hatari David Villa na kiungo Silva.

Kiungo huyo mshambuliaji Silva yuko kwenye biashara ya Pound 20m na tayari Mnchester United wameshaonesha nia yao ya kumchukua kwa msimu ujao wa ligi.

Kwa upande wake Villa timu ya Chelsea pamoja na Machester City wameonesha nia yao ya kumtaka na timu yake Valencia wametangaza dau la Pound 50m kwa atakae kua tayari kumnunua.

Kwa upande wao Chelsea wamemtolea macho David Villa ili kuchukua nafasi ya Anelka ambae anamaliza mkataba wake wa mwaka mmoja huku Villa akiwa ndio chaguo namba moja kwa mashabiki wa Chelsea.

Licha ya kuwa timu za Hispani nazo zimeonesha nia ya kumchukua Villa, kama vile Barcelona na Real Madrid, lakini yeye mwenyewe amesema kwamba anapendelea zaidi akacheze kwenye Premier League huku akionesha mapenzi yake yako zaidi kwa timu ya Chelsea.

David Villa amekua ni mshambuaji hatari ambae anategemewa katika timu yake ya Valencia pamoja na taifa lake la Hispania katika mashindano ya kombe la
Dunia kwa sasa ameshaweka nyavuni magoli 121, katika mechi 223 kwenye timu yake ya Valencia, na pia ameshapachika magoli 37 kwenye mechi 55 alizocheza kwenye timu ya Taifa.

Villa ambae kwa sasa ana umri wa miaka 28, amesema anaangalia zaidi kufanya vizuri katika timu yake ya Valencia na pia kwenye mashindano ya kombe la Dunia huko Afrika Kusini,
na yatakapo malizika mashindano hayo ndipo atakapojua ni wapi ataelekea na uamuzi wake hauaelemea kwenye pesa zaidi bali utajali mapenzi.


.

Soma Zaidi ...

Monday, March 22, 2010

SIKU YA MAJI DUNIANI


Watu zaidi ya bilioni moja duniani wanakosa maji safi ya kunywa, sehemu kubwa ya ardhi ya dunia imezungukwa na maji.Kwa hali hiyo inaweza kuonekana kwamba kuna kiasi cha kutosha cha maji katika dunia.

Asilimia 97,5 ni maji ya bahari na mito pamoja na maziwa, kiwango kilichosalia cha asilimia 2,5 ni maji maji safi.Takriban theluthi moja ya watu wote duniani hawana maji safi ya kunywa.Na idadi nyingine inagawanya kiasi cha maji kilichosalia.

Hii leo karibu watu billioni 1.1 duniani hawana maji safi ya kunywa na wengine wapatao billioni 2,6 ambao ni kiasi cha thuluthi moja ya watu wa dunia nzima hawapati maji ya kutosha kukidhi huduma zao za siku kwa jumla.

Katika malengo ya Millenium ya Umoja wa mataifa imezungumzwa kwamba, maji ni mojawapo ya bidhaa muhimu inayotakiwa kuwafikia watu wote wa dunia kufikia mwaka 2015.

Data za shirika la maji nchini Ujerumani za mwaka 2008 zinaonyesha kwamba matumizi ya maji kwa siku yalifikia lita 122.

Nchini Italia kiwango hicho ni lita 800 kwa kila mtu.
Kwa mantiki hiyo imeonyesha kwamba matumizi jumla ya maji yanazidi kuongezeka kila uchao.Maji yanatumika sio tu kwa matumizi ya kila siku ya majumbani bali hata kwenye mashamba kwa mfano ya mchele kahawa au pamba.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la linaloshughulikia mazingira la World wide Fund for Nature WWF unaonyesha kwamba kila mkaazi nchini Ujerumani anahitaji kiwango cha zaidi ya lita 5000 kwa matumizi yake jumla kwa siku.

Ingawaje maji ni bidhaa muhimu katika maisha ya mwanadamu lakini bado imesalia kuwa bidhaa ghali kabisa na ambayo haipatikani kiurahisi na kila mtu na pia ubora wake unatofautiana.
Matatizo hayo ya maji sio tu yanashuhudiwa katika ulimwengu wa tatu bali ni tatizo la ulimwengu mzima kwa jumla.

Kuna maeneo machache duniani ambayo yana matatizo sugu ya ukosefu wa maji nayo ni pamoja na eneo la Sahel mashariki ya kati na baadhi ya maeneo ya Asia.Nchi nyingi zinazoendelea hilo ni tatizo la kila siku.

.
Soma Zaidi ...

KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO PEMBA

Soma Zaidi ...

ANCELOTTI: MAN UNITED ARE NOW THE FAVOURITES TO WIN THE TITLE


Carlo Ancelotti admits Manchester United are now the favourites to win the title after Chelsea slipped up again.

Days after being knocked out of the Champions League to Inter Milan, Ancelotti's Blues saw their Premier League hopes dented by Sam Allardyce's plucky Blackburn.

El-Hadji Diouf headed Rovers level in the second half after the visitors had failed to build on the early lead given them by Didier Drogba's 28th goal of the season.

And it means Chelsea are outside the top two for the first time since August and lie four points behind United - although they still have a game in hand.

Ancelotti admits his team have made it much more difficult for themselves and knows only a win will be enough when they travel to Portsmouth on Wednesday night.

The Italian was asked whether he felt United now had the advantage.

And he said: "They are top of the league now, so yes. We know we have to do better than this.

"We now have less probability of winning the title. We have made it more difficult for ourselves now - although it is not impossible. I still think we can do it.

"We still have the ability to win this title but we have to be at our best. What we have to do now is stay as close to Manchester United as possible so that's why our game at Portsmouth on Wednesday is so important."

Ancelotti admitted this was his worst week since taking charge at Stamford Bridge - but admitted his players are struggling to recover from their humbling by Manchester City last month.

They were particularly disappointing in the second half after looking likely to breeze past Rovers in a dominant first-half show.

The Stamford Bridge boss said: "Yes, it's been a hard week but we have to start preparing for the next games which we need to win.

"The difficult moment started against Manchester City. It's a difficult moment in our season.

"We don't have to lose our confidence but we are behind now. The pressure was that we needed to win this game and we didn't do it. It's more difficult now.

"We have to win games now - that's the only solution to go forward.

"We need to work together and stay compact. We need to prepare well for the next game.

"I don't know how many points we will need to win the title.

"All I know is that we have to win on Wednesday. We have to prepare well for every game and look forward."

One consolation for Ancelotti is that both title rivals United and Arsenal still have to come to Ewood Park to face a Blackburn side who are tough to beat on their own patch. He said: "This is a very difficult place to come. At home they are a very strong team.

"Every team will find it difficult to come here.

"The second half was more difficult for us. We lost a bit of composure and conceded a goal.

"After that we came back but it was too late.

"I'm disappointed because we lost two important points.

"I don't know if there was a hangover from Wednesday against Inter but we prepared very well.

"We tried to win this game to cancel out the game against Inter.

"For an hour we did well but it's not an easy moment for us."

Ancelotti hopes to have both Petr Cech and Michael Ballack available for the trip to Fratton Park - but he faces an anxious wait on Branislav Ivanovic.

The Serbian defender suffered a knee injury following a challenge from Diouf and is likely to need a scan on the problem to determine the extent today.

Ancelotti said: "Ivanovic has a knee injury and we will see on Monday.

"Then we'll have a clearer idea of his injury. You have to be worried but you have to recover quickly.

"Hopefully Petr will be ready for Wednesday. Ballack had a problem with his tendon so should be ready as well.

"We have the quality to push up and look forward to the next game with confidence."

Rovers boss Allardyce tipped Chelsea to do the Double on the eve of the game and does not necessarily think this is the end of their chances.

And he handed Ancelotti a boost by promising to give United and Arsenal just as tough a test when they visit Ewood before the end of the campaign.

He said: "We've only lost twice here all season and we're very proud of that.

"We want to keep that going over the rest of the season.

"Hopefully we can have a big effect on the title by taking points off some more of the big boys between now and the end of the season."

One more bright point for Ancelotti was the fact this was the first time Chelsea have worn their navy away kit in a competitive fixture - and not lost.

SunSport revealed in December how the hooped shirts were cursed after four defeats out of four - to Aston Villa, Wigan, Blackburn in the Carling Cup and Manchester City.

Yesterday was the first time they have dared to don the hoodoo strip since. Maybe a point was not so bad after all.


***The Sun

. Soma Zaidi ...