Baada ya timu ya Taifa ya Uingereza kupatwa na msiba wa kumpoteza mchezaji wake Beckham baada ya kuumia mguu sasa kuna jinamizi jengine linainyemelea timu hio.
Hii ni kutokana na kuumia kwa mshambuliaji wake tegemeo Wyne Rooney jana katika mechi dhidi ya Mnchester United na Bayern.
Rooney aliumia mguu katika dakika za mwisho za mchezo wa jana na kitendo hichi kinaweza kumuweka juu kwa muda wa wiki sita au zaidi na hii itategemea na uchunguzi wa kitabibu ambao utafanyika leo hii.
Kutokana na maumivu aliyoyapata jana mshambuliaji huyu ambae pia ni tegemeo katika timu yake ya Manchester United kuna uwezekano mkubwa wa kuikosa mechi ya jumapili ambapo Manchester watakua na mechi muhimu sana watakapocheza dhidi Chelsea, lakini pia kuna uwezekano mdogo wa Rooney kucheza katika mechi ya marudiano dhidi ya Beyern jumatano ijayo
Nae kocha wa Manchester United Sir Alex Farguson alisema "Rooney ameumia ankle lakini ni mapema mno kuzungumza chochote hadi hapo kesho (leo).
Hii ni mara ya 12 kwa Rooney kuumia ankle katika maisha yake ya uchezaji, lakini mara hii kuumia kwake kumekuja katika wakati mgumu hasa kwa Mahsetani hawa wekundu kwani inawezekana pia wakamkosa mshambuliaji wao kwa mechi zote zilizobaki katika msimu huu wa ligi.
.
No comments:
Post a Comment