Thursday, March 25, 2010

10 WAFA PAPO HAPO KWENYE AJALI TANZANIA


Watu 10 wamekufa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea nje kidogo ya mji wa Daresalaam, alfajiri ya kuamkia leo.
Ajali hiyo ilihusisha basi dogo la abiria na Lori la mafuta.

Walioshuhudia wanasema gari hizo ziligongana uso kwa uso na baadaye Lori kupinduka na kuliangukia basi hilo dogo.

Ajali hiyo ilitokea saa kumi za alfajiri katika eneo la Kibamba kilomita 20 nje ya jiji la Dar es salaam.

Kamanda mkuu wa kikosi cha barabarani Muhamed Mpinga amesema ilikua vigumu kutoa miili ya waliokufa kutokana na jinsi basi hilo dogo lilivyopondwapondwa.

Miili tisa ilitolewa baada ya kunyanyuliwa kwa lori hilo.

Kamanda huyo anasema inaelekea dereva wa lory hilo alishindwa kulidhibiti.

Inasadikiwa Abiria wengi waliokuwa wanasafiri katika basi dogo walikuwa ni wafanyibiashara wadogo wadogo waliokuwa wakiwahi kuchukua bidhaa katika soko la Kariakor.

Kutokana na ajali hiyo, barabara zilifungwa na safari kutoka Dar es salaam kwenda mikoani zikasimamishwa kwa muda, hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari.
.

No comments:

Post a Comment