Thursday, March 25, 2010

BIN LADEN AONYA KUUWA WAMAREKANI

Kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida, Osama bin Laden, ameonya kuwa mtandao huo utawaua Wamarekani, iwapo kiongozi wa maandilizi ya mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, Khaled Sheikh Mohammed, atanyongwa.

Katika ujumbe alioutoa kupitia mkanda wa video, na kurushwa na kituo cha televisheni cha Al Jazeera, Osama bin Laden pia amemuonya Rais wa Marekani,
Barack Obama kuwa anafuata nyayo za mtangulizi wake George W Bush kwa kuendelea na vita nchini Afghanistan.
Kitengo cha kupambana na ugaidi nchini Marekani kimesema mkanda huo unaonekana kuwa halisi.

Marekani katika wiki chache zijazo itafikia uamuzi iwapo mtuhumiwa huyo na washirika wake wanne, washtakiwe katika mahakama ya kiraia au kijeshi.

Utawala wa Rais Obama umetangaza kuwa kesi yao itasikilizwa katika mahakama ya mjini New York Marekani iliyoko mita chache tu kutoka mahali palipokuwa jengo la kituo cha kimataifa cha biashara ambalo lilibomolewa na mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001.
.

No comments:

Post a Comment