Wednesday, March 31, 2010

ICC YAAMUA GHASIA ZA KENYA ZICHUNGUZWE


Ni rasmi kwamba wahusika wakuu wa machafuko yaliyozuka nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 watachunguzwa na kufunguliwa mashtaka.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ilimpa idhini mwendesha mashtaka mkuu Luis Moreno-Ocampo kufanya uchunguzi na kuwafungulia mashtaka washukiwa wakuu 20.


Ghasia zilizuka baada ya vyama vikuu nchini humo, PNU na ODM, kutofautiana kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Watu zaidi ya 1,300 waliuawa na wengine zaidi wakapoteza makazi yao.


Majaji wawili kati ya watatu waliamua kwamba huenda uhalifu dhidi ya binadamu ulitendwa.
"Taarifa zilizopo zinatosha kudhihirisha kwamba uhalifu dhidi ya binadamu ulitendwa nchini Kenya," waliamua majaji hao.

Lakini jaji mmoja alitofautiana na wenzake kuhusu uamuzi huo.


Akiwasilisha ombi lake kwa majaji mwezi Novemba mwaka jana, Luis Moreno Ocampo alidai kwamba viongozi wa kisiasa walipanga na kufadhili machafuko hayo. Wakenya wengi wamepongeza uamuzi huo wakisema ni njia moja ya kumaliza mtindo wa kutenda uovu bila kujali.

.

No comments:

Post a Comment