Friday, March 26, 2010

SOKA WIKI HII

Kura imepigwa kwa duru ya pili ya duru ya kwanza ya Kombe la Afrika la Mataifa ambao Tanzania ina miadi na Somalia n a simba wa nyika- Kameroun wakiwasubiri simba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Nako katika ligi ya Ujerumani kocha wa Bayern Munich, mdachi Louis van Gaal baada ya kuitimua juzi Schalke kwa bao 1:0 katika robo-finali ya Kombe la Ujerumani , adai sasa anataka mataji yote 3 msimu huu:Kombe la ulaya la chamüpions League,taji la Bundesliga na kombe hilo la Ujerumani.

"Nataka kushinda mataji 3", alisema mdachi huyo kabla Bayern Munich, haikuteremka jioni hii uwanjani kupambana na majirani zao wa kusini-Stuttgart.Munich kwahivyo, inabidi kutamba mbele ya Stuttgart, ili salamu zao kwa Manu ,adui yake ijumaane hii azitie maanani.Munich inacheza na Manchester katika robo-finali ya Champions League.Jumamosi iliopita lakini, Munich ilikiona kilichomtoa kanga manyoya ilipozabwa mabao 2:1 Frankfurt. haitataka kurudia makosa hayo leo.

Changamoto nyengine uwanjani jioni hii ni kati ya mainz na mabingwa wolfsburg,Hertha berlin na Borussia Dortmund wakati Hannover inaikaribisha nyumbani FC Cologne.Bremen inacheza na Nüremberg kabla ya kesho Hoffenheim kukumbana na Freiburg na Borussia Mönchengladbach kukamilisha kalenda ya Bundesliga mwishoni mwa wiki hii na Hamburg.

Ama katika Premier League, Muivory Coast ,Didier Drogba anaamini kwamba Chelsea bila kutamba kesho mbele ya Aston Villa itajikuta mashakani.
Kikosi hiki cha kocha Carlo Ancelotti kilipata nguvu mpya na ari mpya kati ya wiki hii kilipoicharaza Portsmouth mabao 5:0.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ana yakini kuwa ,Arsenal mwishoe,itasahau jiinamizi walilolion huko Birmingham City miaka 2 iliopita na kutamba mwishoni mwa wiki hii.Birmingham inalenga kubakia kati ya safu ya ngazi ya premier League.Arswenal pamoja na Chelea zinaifukuzia Manchester united kileleni mwa Premier League.



Nako kwenye Kombe la Dunia duru ya pili katika mzunguko waa kwanza wa kinyan'ganyiro cha kombe lijalo la Afrka la mataifa kwa wachezaji wanaocheza ligi za Afrika tu imerudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii:

Nigeria,ina kibarua kigumu mwishoni mwa wiki hii kufuta madhambi yao ya mabao 2:0 waliopigwa na jirani zao Niger katika duru ya kwanza ya kinyan'ganyiro hiki.
Hivyo, itabidi kupania kwani timu kadhaa za Afrika zinawania tiketi zao za kwenda Sudan,
ambako ndio kituo cha Kombe lijalo kwa timu za wachezaji wa ndani ya Afrika. Nigeria, imemsajili kwa Kombe hili,mtiaji wao mabao mengi katika ligi ya nyumbani: Ahmed Musa.Kwani, ni mizinga yake inayotarajiwa na mashabiki wa Nigeria duru hii ya pili kufuta mabao 2 ya Niger ya duru ya kwanza.

Mabingwa watetezi ni simba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na wameapa kuridi nalo Kombe Kinshasa.

Kongo ilitoa salamu zake na mapema katika duru ya kwanza ilipoikomea Gabon mabao 2:1.Gabon itajitutumua isimezwe tena na simba -mabingwa.Tanzania-kilimanjaro Stars, wana miadi na Somalia wakati jirani zao Malawi , wanaumana na Msumbiji .

Tembo wa Ivory Coast ambao wanatazamia mwishoni mwa wiki hii kumtangaza kocha wao mpya, wana miadi na Togo.Zimbabwe, inacheza na jirani zao Swaziland wakati Bafana Bafana au -Afrika kusini , inapambana na Botswana.Namibia inaikaribisha Seyschelles.

Majirani wengine uwanjani ni Uganda na Rwanda.Angola, iliokuwa mwenyeji wa Kombe lililopita la Afrika la Mataifa tofauti kabisa na hili, mapema mwaka huu,iko nyumbani ikiwakaribisha Wabuki- Madagaskar.Black Stars (Ghana), nyota yao nyeusi inan'gara mjini Accra, mbele ya Burkina faso.Siera leone inaumana na Senegal wakati Guinea, inacheza na Mali.Libya inaikaribisha nyumbani Algeria, mojawapo ya timu 6 za kombe lijalo la dunia ,kanda ya Afrika:

Tugeukie sasa Kombe lijalo la dunia nchini Afrika kusini litakalofunguliwa rasmi kwa mpambano kati ya wenyeji Bafana bafana na Mexico Juni 11.Kocha wa Ujerumani,
mojawapo ya timu zinazopigiwa upatu kutoroka na taji,Joachim Loew , ametangaza kwamba atataja kikosi chake kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika afrika kusini hapo mwanzoni mwa mwezi Mei.Amesema ameamua kutangaza kikosi chake wiki moja kabla msimu huu wa Bundesliga kumalizika hapo Mei 8.

.

No comments:

Post a Comment