Sunday, March 28, 2010

BERBATOV A.K.A BERBATOP AIWEKA MANU TOP


Dimitar Berbatov airejesha tena Manchester United kileleni mwa ligi ya Uingereza kwa kudhihirisha kwamba maisha yanaendelea hata bila ya mshambuliaji machachari Wyne Rooney.

Berbatov alitoa zawadi kwa Ferguson baada ya ile kamari aliyocheza ya kumueka nje ya kikosi Wyne Rooney

Kizaa zaa kilianza pale mchezaji wa Bolton Jlloyd Samuel alipouzamisha nyavuni mpira wa krosi uliopigwa na Giggs na kuandika goli la kwanza kwa upande wa Mashetani wekundu.

Baadae ilikua ni zamu ya Berbatov alipopachika bao la pili na la tatu, lakini mambo hayakuishia hapo mabadiliko aliyoyafanya Sir Alex yalizaa matunda pale alipomtoa nje Giggs na kumuingiza Gibson ambae aliweza kupachika bao la nne katika dakika ya 82 baada ya kupokea pasi mwanana kutona kwa winga wa kushoto Nani.

Kabla ya mechi hio ya Mashetani wekundu kulikua na mechi kati ya Chelsea na Aston Villa ambapo Chelsea walitoa kichapo cha paka mwizi kwa Villa kwa kuwatandika mabao 7 - 1 licha ya kumkosa mshambuliaji wao matata Drogba.

Kwa matokeo hayo ya jana ManU wanarejea kileleni mwa ligi hio wakiwa na alama 72 huku Chelsea wakiwa kwenye nafasi ya pili kwa alama 71 huku wote wakiwa na michezo sawa.


.


No comments:

Post a Comment