Friday, March 26, 2010

KENYA YAKATAA KUOKEA WASHUKIWA WA UHARAMIA

Kenya imekataa kuwapokea washukiwa watatu wa uharamia kutoka Somalia wanaoshikiliwa ndani ya meli moja wa wataliani pamoja na maiti ya mtu mmoja.

Polisi ya kenya imearifu kwamba jela pamoja na mahakama za nchi hiyo zimefurika.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kenya ambayo ni nchi pekee iliyoingia makubaliano na nchi za magharibi zilizopeleka wanajeshi wake katika mwambao wa Somalia kukabiliana na harakati za maharamia,kukataa kuwapokea watuhumiwa wa uharamia.

Mabaharia wa Meli ya Italia Scirocco,walipambana na washukiwa kadhaa wa uharamia katika pwani ya Somalia na baadae kuwazidi nguvu na kufanikiwa kuondoka na watuhumiwa watatu hadi katika bandari ya Kenya mjini Mombasa.

.

No comments:

Post a Comment