Tuesday, March 23, 2010

CHELSEA MANCHESTER CITY WAMTOLEA MACHO DAVID VILLA



Timu ya Valencia wanaweza wakajitilia kibindoni kiasi cha Peund za Kienereza 60m kwa kuwauza wachezaji wake wawili ikiwa ni pamoja na mshambuali wake hatari David Villa na kiungo Silva.

Kiungo huyo mshambuliaji Silva yuko kwenye biashara ya Pound 20m na tayari Mnchester United wameshaonesha nia yao ya kumchukua kwa msimu ujao wa ligi.

Kwa upande wake Villa timu ya Chelsea pamoja na Machester City wameonesha nia yao ya kumtaka na timu yake Valencia wametangaza dau la Pound 50m kwa atakae kua tayari kumnunua.

Kwa upande wao Chelsea wamemtolea macho David Villa ili kuchukua nafasi ya Anelka ambae anamaliza mkataba wake wa mwaka mmoja huku Villa akiwa ndio chaguo namba moja kwa mashabiki wa Chelsea.

Licha ya kuwa timu za Hispani nazo zimeonesha nia ya kumchukua Villa, kama vile Barcelona na Real Madrid, lakini yeye mwenyewe amesema kwamba anapendelea zaidi akacheze kwenye Premier League huku akionesha mapenzi yake yako zaidi kwa timu ya Chelsea.

David Villa amekua ni mshambuaji hatari ambae anategemewa katika timu yake ya Valencia pamoja na taifa lake la Hispania katika mashindano ya kombe la
Dunia kwa sasa ameshaweka nyavuni magoli 121, katika mechi 223 kwenye timu yake ya Valencia, na pia ameshapachika magoli 37 kwenye mechi 55 alizocheza kwenye timu ya Taifa.

Villa ambae kwa sasa ana umri wa miaka 28, amesema anaangalia zaidi kufanya vizuri katika timu yake ya Valencia na pia kwenye mashindano ya kombe la Dunia huko Afrika Kusini,
na yatakapo malizika mashindano hayo ndipo atakapojua ni wapi ataelekea na uamuzi wake hauaelemea kwenye pesa zaidi bali utajali mapenzi.


.

No comments:

Post a Comment