Wednesday, March 31, 2010

RUFAA YAKATALIWA KUUSHITAKI UM

Wakati huo huo , mahakama ya rufaa nchini Uholanzi imekubali hukumu iliyotolewa hapo kabla kuwa ndugu wa wahanga wa mauaji ya mjini Srebrenica hawataweza kuushtaki umoja wa mataifa kutokana na mauaji hayo.

Watu karibu 6,000 walionusurika na mauaji hayo pamoja na jamaa zao wamo katika kundi linalojulikana kama akina mama wa Srebrenica na wanasema kuwa umoja wa mataifa unahusika na mauaji hayo kutokana na kushindwa kuyazuwia.

Mawakili wanaowakilisha kundi hilo la watu walionusurika wanasema kuwa watakata rufaa katika mahakama kuu ya Uholanzi ili kulipeleka suala hilo katika mahakama kuu ya umoja wa Ulaya..

No comments:

Post a Comment