Thursday, March 25, 2010

APRILFOOL, 2010

Wazee wetu, Ndugu zetu,

Assalaam Alaaykum

UMOJA, UHURU, UADILIFU

Wazanzibari Tushikamane Tugombea Wattani Wetu

Aprilfool, April 1964

Wazanzibari tulifanyiwa Aprilfool siku ile ya April 24, 1964 pale Nyerere kwa mbinu zake ovu alipomlaghai Mzee Karume na kuleta zile Articles of Union, 1964; akaimeza na kuifutisha Dola Huru ya Zanzibar kwa huu wenyekuitwa muungano.

“Articles of Union, 1964”,

a. The Constitution and Government of the United Republic;

Katiba na Sirikali ya Jamhuri ya Muungano

b. External Affairs;

Mambo ya Nje

c. Defence;

Jeshi


d. Police;

Polisi


e. Emergency Powers;

Uwezo wa kutangaza hali ya khatari


f. Citizenship;

Uraia


g. Immigration;

Uhamiaji


h. External trade and borrowing;

Biashara za nje na mikop0


i. The Public service of the United Republic;

Utumishi wa Sirikali ya Jamhuri ya Muungano


j. Income tax, corporation tax, customs and excise;

Mapato, kodi, kastamu


k. Harbours, civil aviation, posts and telegraphs;

Bandari, huduma za anga, posta na telegram


Vifungu Kumi na Moja hivi ni Utiwamgongo wa Nchi

Hapana shaka sote tunatambuwa kwamba mambo kumi na moja haya ndio utiwamgongo wa Dola yoyote ile, bila ya haya haiwi Dola. Vifungu hivi vimekuwa vikiongezwa na Tanganyika mara baada ya mara bila ya hata kushauriwa, licha ya kuwafiqiwa na Zanzibar. Muhimu mno katika vifungu vilivyo ongezwa ni “Ilimu ya Juu, “Higher Education”. Mafuta, gesi na mali asili hapana shaka ni katika mambo muhimu, ni uchumi wa Nchi. Kuongezwa huku huwa ni kwa kutolewa katika Sirikali ya Zanzibar na kutiwa katika Sirikali ya Tanganyika.

Wazalendo wa Kizanzibari Hawataridhia

Tangu sikumosi ya khiyana hii kuu Nyerere aliotufanyia Wazanzibari, Wazalendo wa Kizanzibari wamekanya vikali uovu huu. Wazalendo wa Kizanzibari wataendelea kukanya uovu huu na kufanya kila waliwezalo kuhakikisha kwamba Dola Huru Kaamili ya Zanzibar inarejea kama ilivyokuwa siku ile ya December 10, 1963 ilipopata Uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Wazalendo Unajidhatiti

Kwa kukaribia siku hii, siku ya giza, siku Zanzibar ilipofanyiwa Aprilfool, Umoja wa Wazalendo unajidhatiti kuendeleza harakati za kuikataa dhulma hii na kuwania kurejea Dola Huru ya Zanzibar. Umoja wa Wazalendo unawanadia Wazanzibari tushikamane na kwa umoja wetu tuendeleze harakati za ukombozi wa Nchi yetu, Zanzibar kutokana na ukoloni wa mvamizi mkoloni Tanganyika.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa TaƔala atujaalie kila kheri na atuepushe na kila shari na atujaalie ufunguzi wa karibu, Aamyn.

Wa Billahi Tawfiiq

Umoja wa Wazalendo

Zanzibar, March 25, 2010

.

No comments:

Post a Comment