Tuesday, March 23, 2010

BAO HAPO NJIA MBILI

Wazee wetu, Ndugu zetu

Assalaam Alaykum

UMOJA, UHURU, UADILIFU

Nini Makusudio ya Bao Hili

Ukifika njia mbili, meli kumi ukielekea Mkokotoni kutoka mjini Zanzibar; kuna saruji (bao) limeandikwa, “Coral Cave and Slave Chambers”. Maneno haya tunaweza kuyatarjimu kama hivi, “Pango la Pwani na vyumba vya watumwa”. Hivi ni kueleza kwamba huko Mangapwani kuna pango ambalo wakiwekwa watumwa. Hivi pia ndivyo wanavyoeleza wale wanaofuatana na watalii kufika kwenye hilo pango. Inasikitisha sana kuona uwongo huu mpaka hii leo bado inatiwa kwenye vichwa vya wageni, bali zaidi wananchi wenyekuishi na kupita njiani hapa kila siku. Zanzibar yamejaa ya uwongo kama haya. Suala ni nini makusudio ya yote haya? Tujaalie haya yenye kuelezwa ni kweli, jee ni sisi kutafakhari kwa haya. Hapana shaka hili si lakutafakhari nalo na kufika kuweka bao njiani kueleza hili, bali ni kuona haya na aibu.


Kujenga Chuki Baina ya Binaadamu

Bao hili, hapana shaka halina isipokuwa kupandikiza chuki baina ya binaadamu kwa uwongo usiokuwa na msingi. Ziada ya uwongo uliojengwa na kupaliliwa kila siku, hili bao ni kuzidisha chuki hizi. Vipi tunapiga makelele kwa kusema “Umoja na Mshikamano”, haya ni maneno, lakini vitendo ni hili bao, bao linajenga chuki, maneno yanasema tuwe wamoja. Hapana shaka vitendo vinanguvu kuliko maneno.


Tunaomba Sirikali Iliondoe Bao Hili

Ili tujiepushe na aibu hii, aibu ya kutilia nguvu uwongo usiokuwa na misingi, na aibu ya kujenga chuki ambazo zinavunja umoja baina ya binaadamu, tunaiomba Sirikali ya Zanzibar ichukuwe khatuwa za haraka kuliondoa bao hili.


Wa Billahi Tawfiiq


Farouk

March 22, 2010

.

No comments:

Post a Comment