Sunday, March 28, 2010

UJERUMANI KUANZA MAZUNGUMZO KUHUSU WAFUNGWA WA GUANTANAMO

Wizara ya ndani ya Ujerumani imethibitisha imeanza tena mazungumzo na Marekani kuhusu uwezekano wa kuwakubali wafungwa wa zamani wa gereza la Guantanamo.

Karibu mwaka mmoja sasa,Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa akijaribu kulifunga gereza hilo lililoko katika eneo la Cuba lililo kwenye mamlaka ya Marekani lakini amekumbana na matatizo ya kupata nchi zitakazowakubali wafungwa walioachiliwa.

Kiongozi wa ngazi ya juu wa masuala ya usalama nchini Ujerumani amelipinga hatua yĆ” kuwakubali wafungwa wa Guantanamo akionya kwamba linaweza kusababisha wasi wasi mkubwa wa usalama.

.

No comments:

Post a Comment