Wednesday, January 27, 2010

TAMKO LA MUWAZA KUHUSU MARIDHIANO NA MUSTAKBAL WA ZANZIBAR

MUWAZA inalaani vikali njama za viongozi wa Bara na vitimbakwiri vyake kutaka kuridisha uhasama baina ya Wazanzibari baada ya Wazanzibari kufikia hatua ya Maridhiano

MUWAZA inalaani kuingiliwa kati na Viongozi wa Bara katika maamuzi ya Wazanzibari

MUWAZA inalaani kudharau kwa Viongozi wa Bara maamuzi ya Rais na serikali ya Zanzibar na kufanya njama ya kutaka kuyaweka kando maamuzi ya Rais

MUWAZA inalaani kutaka kutayarisha mbinu za kuingilia kati maamuzi ya Baraza la Wawakilishi

MUWAZA inalaani njama za Bara kwa lengo la kuchelewesha kwa makusudi na kukwamisha kwa makusudi kutekelezwa kwa MUAFAKA wa tatu

MUWAZA inalaani kauli za Makamba, Msekwa na Chilingati za kuwaamulia Wazanzibari kuhusu Maridhiano yao na Mustakbal wao

MUWAZA inawalaani Vibaraka na Vitimbakwiri wanaotaka kuiangamiza Zanzibar kwa maslahi yao binafsi

MUWAZA inasisitiza tena kwamba Uchaguzi uahirishwe

MUWAZA unaunga mkono MAAMUZI YA BARAZA LA WAWAKILISHI yatoshe kuwa kama kura ya maoni ya Wazanzibari

MUWAZA inapendekeza kuundwe Serikali ya mpito kabla ya Uchaguzi ili kuyashughulikia maridhiano na kutengeneza misingi bora ya Uchaguzi

MUWAZA inalishauri Baraza la Wawakilishi lihakikishe kwamba Maslahi ya Zanzibar na Mustakbal wake wanayaweke mbele na :

1 Lirekibishe Katiba ili kuunda serikali ya mpito

2 Lirekibishe Katiba ili kulinda na kuendeleza mbinu za Maridhiano

3 Lirekibishe Katiba irekibishwe ili Katiba ya Muungano ipitiwe upya na hatimae ikibidi iundwe Katiba mpya ya Muungano

MUWAZA inawanasihi Wawakilishi wahakikishe kwamba:

I Mamlaka ya Zanzibar yanabaki katika mikono ya Zanzibar

II Wadhifa wa Waziri Kiongozi ubadilishwe na badala yake uwe wa Waziri Mkuu

III Rais wa Zanzibar awe moja kwa moja Makamu wa Rais wa Tanzania

IV Urais wa Tanzania uwe wa zamu baina ya Tanganyika na Zanzibar

V Baraza la Mawaziri la Zanzibar liwe sawa na Baraza la Mawaziri jengine lolote Ulimwenguni

VI Baraza la Wawakilishi liwe na nguvu sawa na Bunge lolote Ulimwnguni

VII Mungano uwe wa Serikali Tatu

MUWAZA inampogeza Rais Amani Abeid Karume kwa kuheshimu Katiba ya leo na kutotaka kuongeza muda wake wa Urais chini ya Katiba leo

MUWAZA inampongeza Maalim Seif Shariff Hamad kwa kutokuwa na uroho wa Madaraka na kuwa tayari kumuachia Rais Amani kundelea madarakani ikibidi.

Mungu Ibariki Zanzibar – Amiin !!!

No comments:

Post a Comment