Tuesday, January 26, 2010

KUIJENGA UPYA HAITI


Itachukua muongo mmoja kukarabati nchi ya Haiti ambapo kulitokea uharibifu mkubwa uliosababishwa na tetemeko la ardhi.
Hiyo ni kauli ya waziri mkuu wa Canada Stephen Herper wakati kongamano la siku moja la wafadhili wa kimataifa mjini Montreal kujadili mustakabhali wa kisiwa hicho.

Akizungumza baada ya kongamano hilo kumalizika waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema wafadhili hawapaswi kuwaachia wananchi wa Haiti jukumu la kuijenga upya nchi yao.

Naye waziri mkuu wa Haiti Jean Max Belerieve amewakumbusha wafadhili kuhusu mahitaji muhimu ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na vitanda laki mbili na huduma za afya na matibabu kwa takriban watu laki nne.

Mkasa wa tetemeko la ardhi lenye kipimo cha saba kwenye vipimo vya Richer ulisababisha vifo vya takriban watu laki mbili na kuiacha Haiti mojawapo wa nchi masikini kabisa duniani ikikabiliana na uharibifu wa kiwango cha juu.

Kongamano kuu la wafadhili litafanyika mwezi Machi nchini Marekani ili kujadili zaidi mstakabhali wa Haiti.

No comments:

Post a Comment