Saturday, January 23, 2010

AKATWA MKONO BAADA YA KUIBA SIMU SOMALIA


Kijana mmoja nchini Somalia anaejuilikana kwa jina la Yussuf Sheikh Ahmed amekatwa mkono baada ya kuhukumiwa kwa sheria za kiislam na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab baada ya kukamatwa akiiba simu.

Yussuf ambae ana umri wa miaka 30 mkaazi wa Merka alikatwa mkono wake wa kulia baada ya kukiri kutenda kosa hilo mahakamani na baadae aliwahishwa hositali kwa matibabu baada ya kupewa adhabu hio.

"Adhabu hii ni mojawapo ya juhudi zetu za kutokomeza uhalifu kwa sheria za kiislamu, mtu yoyote atakayeiba atakatwa mkono wake", alisema Sheikh Isa Mohamed, ambaye ni mmoja wa maafisa wa Al Shabab.

Kundi la Al Shabab linaihikilia baadhi ya miji nchini somalia na kuendesha hukumu chini ya sheria za kiislamu kwa wale wote wanaokamatwa na makosa kama ya wizi, uzinifu, ulevi n.k .

No comments:

Post a Comment