Sunday, January 31, 2010

WASHIKA BUNDUKI WASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI KWAO DHIDI YA MASHETANI WEKUNDU

Timu ya soka ya Arsenal leo hii walishindwa kufurukuta mbele ya Man Utd katika uwanja wao wa Emirates Stadium kwa kuchukua kipigo cha magoli matatu kwa koja.

Man Utd waliandika bao la kwanza kupitia kwa winga wake wa kulia Nani baada ya kupiga krosi iliyomfanya mlinda mlango wa Arsenal Almunia kuukwamisha mpira nyavuni, bao la pili la Man Utd lilipachikwa nyavuniu na Rooney ambapo lile la tatu lilifungwa na Park.Goli la kufutia machozi kwa upande wa Arsenal limefungwa na Vermaelen.

Kwa matokeo hayo Man Utd bado wanaendelea kushikilia nafasi ya pili kwa kuwa na alama 53, na Arsenal wamebaki nafasi ya tatu kwa alama 49 huku usukani wa ligi hio bado unashikiliwa na Chelsea wakiwa na alama 54.

Kabla ya mechi hio kulikua na mechi kati ya Man City na Portmouth ambapo City walishinda 2-0

Kwa upande wa Kombe la mataifa Afrika limemalizika leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ghana na Egypt na Egypt kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli moja kwa zero na kuwafanya Egypt kuweza kutetea ubingwa wao.

No comments:

Post a Comment