Monday, January 25, 2010

NDEGE YA ETHIOPIA YAANGUKA BAHARINI


Ndege moja ya abiria ya kampuni ya Ethipia Airline imeanguka katika bahari ya Mediterenian muda mfupi baada ya kuruka ikitokea Beirut.

Ndege hio ilipoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kuruka mapema asubuhi ya leo, walioishuhudia ajali hio walisema kua moto mkubwa umeonekana katika eneo la bahari pahali ambapo ndege hio imeangukia.Wakuu wa kikosi cha uokoaji cha Lebanon wamesema kua wamefanikiwa kuwaokoa watu saba.

Ndege hio aina ya Boeing 737 iliyoruka katika uwanja wa ndege wa Beirut Lebanon 2:10 am na kutarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Adis Ababa Ethiopia saa 7:50 am (local time), ilikua imbeba abiria zaidi 83 pamoja na wafanyakazi 7.

Wakuu wa Lebanon wameanzhisha zoezi la uokoaji katika ajali hio lakini zoezi hilo limekua likifanyika kwa tabu kutokana na kuwepo kwa upepo mkali pamoja na mvua kubwa.

Abiria waliokuwemo ndani ya ndege hio ni pamoja na walebanon 54 waethiopia 22 pamoja na raia kutoka mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Iraq

No comments:

Post a Comment