Saturday, January 30, 2010

SERENA WILLIAMS BINGWA TENA AUSTRALIAN OPEN

Mcheza tenis namba moja duniani Serena Williams(USA) leo hii ameweza kutetea ubingwa wake katika mashindano ya Australian open baada ya kumfunga Justine Henin ( BEL) kwa 6-4, 3-6, 6-2, katika mchezo uliodumu kwa masaa mawili na dakika saba.
Serena Williams anakua mchezaji wa kwanza kuweza kutetea ubingwa wake huko Melborne tangu pale Jennifer Capriati(USA) alipotwaa ubingwa mara mbili mfululizo mwaka 2001 na 2002, Capriati alimshinda Martina Hingis(SUI) mara zote mbili.

Hii itakua ni mara ya tano kwa Serena Williams kutwaa kombe la Australian Open Baada ya kuchukua 2003, 2005, 2007, 2009.

No comments:

Post a Comment