Wednesday, January 27, 2010

MAN UNITED WAPAA FAINALI CARLING CUP

Mashetani wekundu watinga fainali ya Carling Cup kwa kuwachabanga Manchester City katika mechi ya pili ya nusu fainali kwa mabao 3-1, mechi iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford.

Magoli ya mashetani wekundu yalifungwa na Paul Scholes la kwanza, Michael Carrick la pili, na lile la tatu limefungwa na Wayne Rooney na goli la kufutia machozi la City liliwekwa yavuni na Teves.

Man United watakutana na Aston Villa katika mechi ya fainali siku ya tarehe 28 Febuary katika uwanja wa Wembley.

Matokeo mengine ya mechi za leo ni kama ifuatavyo:

Premier League
Blackburn Rovers 2 - 1 Wigan Athletic
Everton 2 - 0 Sunderland
Aston Villa 0 - 0 Arsenal
Chelsea 3 - 0 Birmingham City

Coppa Italia
AC Milan 0 - 1 Udinese

No comments:

Post a Comment