Sunday, January 24, 2010

UONEVU HUU MPAKA LINI?

Kwa muda mrefu sasa tumekua tukishuhudia mateso na dhuluma zinazofanywa na vyombo vya usalama kama vile Jeshi la polisi, JWTZ na wengine.

Ninavyojua mimi ni kuwa hivi vyombo vya dola vipo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi pamoja na mali zao lakini hali hii imekua ni kinyume, walinzi wetu hawa wamekua wakijipandia magari ya abiria bure,wamekua wakiwavua na kuwanyang'anya watu nguo zao, wanawapiga watu wasio na hatia na wengine kuwasababishia vifo na ulemavu wa maisha.


Swetu Fundikira aliezaliwa tarehe 28/06/1962 ni mmoja wa watu waliokutwa na mikasa ya kupigwa na wanajeshi wa JWTZ siku ya ijumaa usiku katika maeneo ya kinondoni na kupelekea kulazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na hatimae kuaga dunia leo asubuhi kutokana na majeraha aliyoyapata.

Marehemu kaacha mke, watoto wawili na mjukuu mmoja, Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema.......................Ameen.

Kwa kweli hii hali imekua inatisha na haionekani kama kuna mtu ambae anaweza kuizuia kwa kuwachukulia hatua hawa wanajeshi, maana kama wangelikua wanachukuliwa hatua za kisheria na wakuu wao wa kazi na Serikali kwa ujumla pindi wanapofanya makosa basi wasingekua wakifanya mambo hayo kwa hayo kila siku, lakini hapa unaeza kusikia wahusikawamehamishwa sehemu zao za kazi na kupelekwa mkoa mwengine.

Lakini ifahamike kua kuna siku watu watachoka na kuanza kujichukulia hatua mikononi mwao kwa kupambana na vyombo vya dola iwapo tu Serikali haikulifanyia ufumbuzi hili tatizo

1 comment:

  1. Hawa wanafanya hivi kutokana na kuwa hawana kazi wanachukua pesa za bure hasa hawa JWTZ na badala yake ndio kuonea raia wasio na hatia.

    Sasa kama huyu weshamuua sijui serikali itachukua hatua gani.

    ReplyDelete