Saturday, January 30, 2010

HONGERA ZANZIBAR NA WAZANZIBARI

MUWAZA (MUSTAKBALA WA ZANZIBAR) UNATOA PONGEZI ZA DHATI KWA :

RAIS AMAN ABEID KARUME NA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KWA UJASIRI NA USHUJAA WAO ULIOJITOKEZA KATIKA KULETA KUUNGANA KWA WAZANZIBARI, KUONDOSHA UHASAMA, CHUKI, MIFARAKANO ISIOKWISHA NA UADUI USIO NA MAANA.

TUNAWAPONGEZA KWA KUTULETEA ZANZIBAR ISHARA NJEMA INAYOLETA MATUMAINI YA SALAMA NA AMANI NA KULETA MATARAJIO YA SIASA ZA KIDEMOKRASIA NA KUJENGA MISINGI YA MAENDELEO

TUNAMPONGEZA MAKAMO WA RAIS WA MUUNGANO MH. ALI MUHAMMED SHEIN NA MH. MOHAMMED GHARIB BILAL KWA KUCHUKUA JUKUMU LA KUWAHAMASISHA WANA CCM KATIKA KIKAO MAALUUM CHA NEC ZANZIBAR

TUNAMPONGEZA KIONGOZI WA UPINZANI MH. ABUBAKAR KHAMIS BAKARI KWA MAPENDEKEZO YA KHERI ALIYOYAWAKILISHA KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI

VILE VILE TUNALIPONGEZA BARAZA LA WAWALIKILISHI ZIMA KWA DHAMANA, HAMASA NA HISIA ZA KIZANZIBARI KWA UPEO WAO WA KUYAKUBALI NA KUYASHINDIKIZA MABADILIKO YA KIHISTORIA YANAYOLINDA MUSTALBAL WA ZANZIBAR

TUNAWAPONGEZA WAZANZIBARI WOTE WALIOJITOKEZA HADHARANI NA WASIOJITOKEZA ULIMWENGUNI KOTE KWA KUWA NA IMANI NA VIONGOZI WAO PAMOJA NA KUWAOMBA WAONYESHE UZANZIBARI WAO WA DHATI KWA KUSAIDIA VIONGOZI WAO NA NCHI YAO YA ZANZIBAR KWA KUCHUKUA MAJUKUMU YA KILA AINA NDANI NA NJE YA ZANZIBAR KULETA MAENDELEO YA KUDUMU ZANZIBARI

TUNAWAOMBA VIONGOZI WAKIWEMO RAIS AMANI ABEID KARUME, MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD, WAWAKILISHI, WABUNGE WA KIZANZIBARI NA WAZANZIBARI WOTE KWA JUMLA WASIMAME KIDETE NA IMARA KULINDA MUSTAKBAL WA ZANZIBAR NA KUJILINDA NA FITINA NA MAFATANI WANAOTAKA KUIANGAMIZA ZANZIBAR

ZANZIBAR IMEWEKA HISTORIA YA KUIGWA AFRIKA NA ULIMWENGUNI KOTE NA KUWEKA MFANO WA VIPI MIZOZANO YA KISIASA INAWEZA KUTATULIWA KWA SALAMA NA AMANI – HAYA NI YAKUIGWA ULIMWENGUNI KOTE

YA RABBI MOLA WABARIKI MILELELE VIONGOZI WEMA WA ZANZIBAR, WAZANZIBARI NA NCHI YA ZANZIBAR

KWA NIABA MUWAZA

Dr. Yussuf S. Salim

No comments:

Post a Comment