Wednesday, December 30, 2009
Tuesday, December 29, 2009
MWANAMKE ABAKWA NA WANAUME SITA
Mwanamke mmoja jina limehifadhiwa amelazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar baada ya kubakwa na wanaume wapatao sita na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri za mbele na nyuma.
Mwanamke huyo alifanyiwa unyama huo wa kusikitisha siku ya sherehe za sikukuu ya Krismas katika eneo la ufukwe wa bahari, maeneo ya Maisara mjini Zanzibar.
Taarifa kutoka Makao Makuu ya Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani humo, zimesema kuwa mwanamke huyo ni mkazi wa Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar na aliokotwa na wavuvi wa eneo hilo akiwa amepoteza fahamu.
Taarifa hizo zimeelezwa kwamba msichana huyo alichukuliwa katika ukumbi wa disko wa hoteli ya Bwawani na wavulana hao, akiwa amelewa na kumpeleka katika eneo hilo la ufukweni na kuanza kumbaka kwa zamu.
Hadi kufikia jana jioni, ilidaiwa kuwa hali ya msichana huyo ilikuwa bado ni mbaya kutokana na athari kubwa alizozipata hasa katika sehemu zake za siri.
Daktari aliyempokea msichana huyo alisema, “aliletwa hapo akiwa hajitambui kabisa na sehemu zake za siri hasa sehemu ya haja kubwa zilikuwa zimeathiriwa vibaya”, alisema daktari wa zamu katika hospitali hiyo.
Soma Zaidi ...

Monday, December 28, 2009
TASWIRA ZA BELGIUM
Hichi ni chuo kikuu kinachohusika na mambo ya umeme.
Soma Zaidi ...
Wapenzi wasomaji , kwa sasa kidogo niko hapa Belgium kwa ajili ya harusi ya ndugu yangu, itakayofanyika siku ya ijumaa, lakini nimekuja huku mapema ili nipate kutembea katika baadhi ya mitaa na hizi ndizo taswira za leo katika pita pita zangu, picha ya juu ni sehemu ya Taxi nje ya kituo cha Treni mjini Leuven.
MVUA ZAATHIRI MKOANI MOROGORO
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Kilosa zimealeta athari katika kijiji cha Mbumi na Kasiki hivyo kusababisha familia nyingi huyahama makaazi yao kufuatia nyumba zao kujaa maji
Soma Zaidi ...
Sunday, December 27, 2009
MNIGERIA ATAKA KURIPUA NDEGE MAREKANI
Umar Farouk Abdul Mutallab kijana wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 23 ambaye alitunukiwa shahada ya uhandisi katika chuo kikuu cha University College of London mwaka jana, amesababisha mtafaruku katika safari za anga baada ya kujaribu kujiripua kwenye ndege yenye abiria 278 na wahudumu 11 iliyokuwa ikielekea Marekani ikitokea Uholanzi.
Sheria kali zimewekwa kufuatia tukio hilo lililotokea siku ya krismasi ambapo Umar alijaribu kujiripua ndani ya ndege ya Northwest Airlines zikiwa zimebaki dakika 20 kabla ya ndege hiyo kutua kwenye uwanja wa ndege wa Detroit.
Umar aliungua moto robo tatu ya mwili wake kutokana na mlipuko uliotokana na kifaa chake alichokuwa amekificha ndani ya suruali yake.
Taarifa zilizotolewa zilisema kwa Umar kabla ya kufanya jaribio lake hilo la kujilipua, alienda kwenye choo cha ndege hiyo ambapo alitumia dakika nyingi na aliporudi alisema anasumbuliwa na matatizo ya tumbo na kuomba blanketi ajifunike.
Akiwa ndani ya blanketi lake, alitengeneza bomu lake kwa kuunganisha kemikali alizokuwa amezibeba na kusababisha mlipuko ulioambatana na moto.
Kabla hajatimiza azma yake ya kuseti bomu lake vizuri, abiria waliokuwa pembeni yake walimrukia na kumzuia asitimize azma yake.
Wahudumu wa ndege walifanikiwa kuuzima moto uliotokea kwenye ndege hiyo ambao uliiunguza suruali yake na kumuunguza mwenyewe robo tatu ya mwili wake.
Umar yuko chini ya ulinzi mkali katika hospitali aliyolazwa akipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyopata kufuatia moto aliousababisha.
Umar inasemekana kuwa aliwaambia maafisa wa Marekani baada ya kukamatwa kuwa ana uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda na alipata mafunzo yake nchini Yemen.
Baba yake Umar ambaye ni tajiri maarufu nchini Nigeria inasemekana alishatoa taarifa kwenye ubalozi wa Marekani nchini Nigeria miezi sita iliyopita kuhusiana na siasa kali za mwanae dhidi ya Marekani.
Kufuatia tukio hilo, sheria kali zimewekwa kwa ndege zinazoenda Marekani ambapo abiria watatakiwa kutonyanyuka kwenye siti zao kwenda kokote ndani ya lisaa limoja kabla ya ndege kutua.
Pia abiria hawatapewa tena mablanketi ya kujifunika kwenye ndege zinazoenda Marekani wakati ndege zitakapokaribia kutua.
Mbali na hatua hizo, abiria pia watatakiwa kuwa na begi moja tu la mkononi na watalazimika kufanyiwa X-ray za vifaa vyovyote vya milipuko kwenye miili yao. Soma Zaidi ...
Saturday, December 26, 2009
Friday, December 25, 2009
BASKELI UHOLANZI
Unaweza ukadhani kwamba hizi baskeli zinauzwa lakini sivyo, hapa ni karibu na kituo cha treni na mabasi hivyo watu huegesha baskeli zao ili kuchukua usafiri mwengine kulekea wenye shughuli zao.
Soma Zaidi ...
Soma Zaidi ...
HATIMAE TANI 296 ZA SAMAKI KUAZA KUGAIWA
Baada ya takriban miezi isiyopungua 10 hatimae samaki wapatao tani 296 waliokamatwa tarehe 8 machi mwaka huu wameanza kusambazwa tayari kwa mgao.
Samaki hao walikamatwa kutoka katika meli ya MV Tawariq 1 ambayo ilikua ikifanya uvuvi haram umbali wa maili 180 kutoka Dar-es-salaam eneo ambalo limetajwa kua ni Exclusive economic zone.
Inasmekana kisheria kesi inayohusiana na ukamatwaji wa meli hii ilikua iendeshwe Zanzibar na ikishindikana basi Germany kutokanana hili eneo walilokamatiwa lakini kesi hii imeendeshwa Tanganyika na hivo kufikia uamuzi kuwa samaki wanapaswa kugaiwa Nchi nzima.
Waziri wa anaeshughulika na masuala ya uvuvi na mifugo ambae ndie mwenye mamlaka ya Mgao huo bwana John Magufuli amesema serikali imegharamika Sh, bilioni 1.2 katika kuhifadhi samaki hao katika kampuni ya Bahari food limited na hadi sasa wamehalipa nusu ya fedha hizo na zilizobaki zitalipwa baada ya kumaizika kwa zoezi la ugawaji samaki hao.
Waziri Magufuli amesema pia katika mgao huo Zanzibar itafaidika na tani 80.
Soma Zaidi ...
Thursday, December 24, 2009
DO NOT RE-USE MINERAL WATER BOTTLES AGAIN
Many are unaware of poisoning caused by re-using plastic battles.Some of you may be in the habit of using and re-using of disposable mineral water battles ( e.g. Nestle, Bisleri, Aquafina Kinley, Evian etc......)keeping them in your car or at work not a good idea.
It happened in Dubai, when a 12 years old died after a long usage of (16 monthes) of AAA mineral water bottle as she used to carry the same fancy (painted by her self) bottle to her school daily.
In a nutshell, the plastic (called polyethilene therephthalate or PET) used in this bottles contains a potaintially carcinogenic element (something called diethilhydroxylamine or DEHA) the bottles are safe for one-time use only; if you must keep them longer, it should be or no more than a few days,week max, and keep them away from heat as well.
Repeated washing and rinsing can cause the plastic to break down and the carcinogens ( cancer- causing chemical agents) van leak in to the water you are drinking.Better to invest in water bottles that are really meant for mulipul euse
.
This is not something that we should be scrimping on. Those of you in family do please advise them especially children. please forward this information.
Prevention is better then cure.

Wednesday, December 23, 2009
ZANZIBAR KUENDE KUKAA GIZAI KWA MUDA WA MWEZI KUANZIA SASA
Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid, amesema Zanzibar itaendelea kukosa huduma ya umeme kwa muda wa mwezi mmoja baada kifaa kinachounganisha waya zinazopokea umeme kutoka Gridi ya Taifa, Tanzania Bara, kulipuka katika kituo cha Fumba, Zanzibar.
Kifaa hicho aina ya Spliter, hutumika kugawa nyaya zinazopokea umeme kutoka Gridi ya Taifa ambacho kililipuka muda mfupi juzi jioni baada ya mafundi kukamilisha matengenezo kufuatia njia moja inayopokea umeme katika kituo hicho kulipuka Desemba 10, mwaka huu.
Waziri Mansour, alisema kifaa hicho kitachelewa kutengenezwa kwa vile viwanda vinavyotengeneza wahusika wapo likizo ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Alisema kifaa hicho kinapatikana nje ya nchi na hivyo akawataka wananchi wa Zanzibar kuwa wastahimilivu. Soma Zaidi ...

NDEGE YA MAREKANI YAANGUKA JAMAICA
Ndege ya abiria ya kimarekani aina ya Boeing 737 imeanguka jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kingston huko Jamaica ilipokua ikitaka kutua.
Ndege hio ilianguka baada ya kukosea njia kutokana na mvua kubwa iliyokua ikinyesha na kukatika vipande viwili hivyo kusababisha abiria 40 kujeruhiwa na hakukua na habari za vifo zilizoripotiwa.

Iliondoka Miami majira ya saa 20:52 (local time) na ilitarajiwa kuwasili Kingstone saa 22:27 huku ikiwa na abiria 148 pamoja na wafanyakzi 6
Soma Zaidi ...
Tuesday, December 22, 2009
WAZANZIBARI TUMECHOKA NA MASWALI
Na mwandishi wa MZALENDO.NET
Utangulizi: Wengi wetu tushachoka na masuali, kwa muda wa miaka karibuni 50 sasa
wazanzibari tumekuwa tukijiuliza bila ya kupata majibu.Nami sitouliza zaidi ya hapo, naamini sasa ni wakati wa majibu. Japo hayatokuwa na ukamilifu,lakini yatatusaidia kutupatia muelekeo.Kwenye nia pana njia, inshallah M.Mungu atawalipa wale wote wanaodanganya na kuficha ukweli wa historia ya visiwa vyetu vya Zanzibar.Leo mzanzibari anazaliwa anakwenda skuli kusoma, badala yake anapotoshwa kwa makusudi. Kama tujuavyo kuwa mali ni fitna,ukiona vita au vurugu jua chako chaliwa kimagendo.Nenda Iraq,vita vingi watu waibiwa mafuta yao.Ukitoka hapo elekea Congo, vita havishi ujue madhahabu na almasi zaibiwa kwa njia za panya.
Ngwe ya muungano:Tukirudi visiwani Zanzibar, jee hii ni kweli kuwa vurugu zinazoendelea au zilizotokea nchini mwetu watu wanaiba nini?Suali gumu sitokuwa na majibu ya papo kwa hapo, lakini pengine na tujaribu kujiuliza ni kipi ambacho wenzetu hawa wa CCM Zanzibar kinachowapelekea kung’ang’ania mfumo wa muungano ambao unatuburuza wazanzibari na kutupotezea rasili mali zetu.Hili limekuja wazi kwenye suala la mafuta ya Zanzibar na ndipo CCM kwa CUF barazani waliamka.Wengine tukaanza kukuna vichwa na kutafuta panadoli za kutuliza
maumivu.
Tukarudi kwenye shina la tatizo, mkataba mbovu wa muungano.Zanzibar imeingizwa mkataba huu na hawa makada wa CCM ambao.Vyereje sasa wamekuwa mstari wa mbele kupiga kelele za mafuta.Walitutosa kwenye mkataba usio na maslahi kwetu bila ya ridhaa yetu.Sasa jee wanakiri kama mkataba wa muungano una makosa na unahitaji marekebisho?au hawakuona wakati mafuta na mengineyo zaidi ya yale 11 ambayo baba etu Mh.Karume alikubaliana na Nyerere.Au walipewa asilimia 10% ili mafuta yetu yaibiwe?Au wanapiga kelele kwa kuzitumia hisia zetu
kujitafutia umaarufu wa kisiasa?
Kama utapenda maoni yangu ambayo utafiti wake ni wa kubaka hapa na pale, muungano ni batili. Haukuwa na wala haujawahi kuwa na ridhaa yetu.Kila mtu ana haki ya kuwa na mawazo tofauti kwenye suala hili, mimi napenda kutumia mawazo yangu kama kijana na kubatilisha muungano na wewe unaweza kufikiria utakavyo na kama utakuja na ushahidi wa kunionesha kama vyombo vya wazanzibari vilipitisha muungano, basi naweza kubadilisha mawazo na msimamo wangu. Hadi leo bunge linakimbia kutoa mkataba huo hadharani kwa sababu wazijuazo wao pekee.Iwavyo na iwe, muungano upo. Ukitaka usitake,upende usipende muungano upo.
Hoja ya msingi sio vipi tumeingia kwenye muungano, bali ni vipi tunafaidika na muungano huu na kama hauna faida vipi kujinasua.Huu ndio mjadala ambao kila kiumbe ambae anaishi Tanganyika au Zanzibar anatakiwa kutafakari.Pengine serekali ya Muungano iko siku itatusikia kelele zetu na kufanya utafiti mzima ili tujue kwa kina nani atasaga mawe pindipo utavunjika.
Maoni yangu binafsi ni yale yale ya umoja ni nguvu, lakini ili Zanzibar inufaike na muungano na Tanganyika ni kwa njia ya shirikisho la nchi za Afrika Mashariki na si vyenginevyo.Zanzibar na Tanganyika ni majirani na hilo haliondoki, vyovyote iwavyo ni kweli umoja ni nguvu.Lakini
tukumbuke utaifa wetu wa kizanzibari ndio majivuno yetu, na katu asilani wazanzibari hatutokubali kuvaa vikofia vya kitanzania.Kwa maana nyengine wazanzibari ni kama taifa jengine hatuko tayari kupoteza utaifa wetu, mila na utamaduni wetu!Tunataka bendera ya Zanzibar ipepee milele! Hakuna mjadala CCM Zanzibar ina uongozi tata katika kusimamia maslahi yetu.Au ndio hoja ile ya mali,na ndio vurugu hazishi Zanzibar.Isijekuwa wazanzibari
tunaibiwa na wenyewe tumetulia kama tuliomwagiwa maji.
Uzalendo wa Tanganyika:Kuna kitu cha kizalendo ambacho mara nyingi nimekuwa nikiganda bila majibu, hapa ni suala la uzalendo. Unajua sijaona sehemu duniani ambayo wananchi wake hawana uzalendo na majisifu kuhusiana na utaifa wao, na hao basi ni watanganyika.Sijawahi kumuona mtanganyika akijisifu kuwa yeye ni mtanganyika, hii ni tofauti na upande wa Zanzibar.Wazanzibari wao kokote unapo wakuta wanataka kujitambulisha kwa majivuno kama ni wazanzibari, na sio watanzania. Pengine hiki ndio chanzo cha matatizo yote ya kuwa Tanganyika na wananchi wake hawana tatizo lolote kwao kukosa au kupoteza utaifa wao.Manaake mara nyingi tumekuwa tukisikia kelele za wazanzibari kukimbia kupoteza serekali yao ya mapinduzi, ambayo kwa sasa japo ipo kama pambo bila ya mamlaka yoyote.
Hapa natumia neno “pambo” kwa kuwa haina madaraka hata ya kumuuwa mbu nchini
mwake bila ya ruhusa kutoka Dodoma.Hapa utashangaa kuona kuwa CCM Zanzibar wamenyamaza kimya, wanaguna wakiwa vichochoroni kuwa rais wao hana mamlaka yoyote na wala hatambuliki duniani.Hapa tusikimbie hoja za msingi, ni uongozi mama wa CCM ndio uliongia kwenye mkataba mbovu wa muungano na ndio wao waliopunguza mamlaka ya Zanzibar kutoka 11 hadi 22.
Hapa leo tukiwaona wawakilishi wa chama tawala wakililia na mafuta, tuwaulize wabunge wenzao waliopitisha kuwa mafuta yetu yagawiwe sawa bin sawa na huku wakigonga
madeski yao kuwa wamefurahia posho watokapo bungeni! Nia na madhumuni ya sera za CCM ni kuvimeza visiwa bila ya kuchakuwa.Huu ndio ukweli mzanzibari, na sio kama tunatia kasumba.Miongoni mwa sera za CCM ni serekali moja, lakini hurusha vumbi la macho kwa kutuambia ati serekali 2 kuelekea moja.Mie binafsi yangu ningelisema sera haswa ni serekali moja, lakini hawa watu wako mawindoni.Mtu anapowinda, hakurupuki na kuanza kutumia
silaha zake.
Kwanza hutumia mbinu za kunyatia na kusubiria hadi muda muafaka unapowasili ndio huanza mashambulizi ili kupata kufanya mauaji na kupata kitoweo.Kwa hiyo Tanganyika mawindoni, na kusubiria ili waimeze Zanzibar kwa mkupuo mmoja!Hii ndio maana ya kuanza mkataba mdogo wa vitu 11, halafu kuongeza hadi 22 na mwishowe ni kufuta serekali ya Zanzibar na kubakia serekali ya Tanganyika ikitawala eneo la Zanzibar kama sehemu yake tokea awali. Ni wapi wameshafanikiwa hadi hapa tulipo kwa mfumo huu tulionao?Tukizingatia serekali yaTanganyika imevaa koti la Tanzania,na kuviburuza visiwa vyetu!
Woga ni udhaifu:Si lengo langu kuingia kwenye siasa, mimi binafsi yangu sifati mlengo wowote.Sababu yangu ya msingi ni kupinga muungano, nahakuna chama kinachounga mkono sera yangu.Lakini inauma kumuona kiongozi wetu akisema Zanzibari ni nchi ukiwa ndani ya Zanzibar, na ukitoka nje basi si nchi.Inaniuma kumuona mzanzibari anasherehekea shangwe za siasa huku nchi yake inamezwa na Tanganyika kwa kisingizio cha muungano.
Haki ya kuunga mkono chama fulani ni ya msingi kwa kila mzanzibari, lakini tungeliomba tafadhalini mukatafakari sera za vyama hivyo kabla ya kuviunga mkono.CCM na hii sera ya serekali 2 kuelekea moja ni dhahir kuwa si njema kwa visiwa vyetu vya Zanzibar.Na kila mzanzibari hana budi kusimama kidete kuwa ifutwe, na kama haifutiki basi wazanzibari musikiunge mkono chama hicho!
Tumekuwa tukiona CCM Bara wakipiga kelele za ufisadi hadharani, ni kipi CCM wetu wa Zanzibar wanachoogopa kusema sera hii ya serekali moja haina maslahi kwa Zanzibar?Unaponyamaza kimya manaake umeikubali, waingereza wamesema “big silence means YES”.Sasa CCM wa Zanzibar tunataka mutoke hadharani kupinga sera hii kwa maslahi ya Zanzibar.Sasa siku ikifika na kikao cha NEC kikisema kinatekeleza sera hii, mutasema nini?Niliahidi kuwa huu ni muda wa majibu, sio masuali kwa hivyo hapa jibu letu la kuwa hawa CCM Zanzibar walionyamazia kimya manaake wanaifurahia na kuiunga mkono!Wasitupumbaze
pale wanaposema ati hakuna CCM Zanzibar atakae kubali serekali moja, hiyo ni danganya toto tuu.
Nishawahi kumsikia kada wa CCM kutoka Zanzibar akisema kuwa hakuna CCM wa Zanzibar atakae ikubali sera hii, sasa kwanini hawaikemei?Kama hawakemei basi wanafaidika kwa aina moja au nyengine.Vyovyote iwavyo wana sababu zao za msingi za ukimya huu, cha msingi ni kwetu wazanzibari kufanya maamuzi kuwa sasa tumechoka na ukimya na woga usiokuwa na misingi yoyote.Huu sio muda wa kukaa na kutishana, muda ushafika wa kila mtu kutoa maoni yake kwa uwazi kabisa na wote tukajua kila mmoja wetu anachokitetea kama kina maslahi na visiwa vyetu ili tukiunge mkono au tukikatae.
Misho:Matatizo ya Zanzibar na suluhisho zake ziko mikononi mwa wazanzibari wenyewe, na wewe kama mwananchi una uwezo wa kutafakari sera ya kila chama kabla ya kukiunga mkono.Kama utahitaji mawazo yangu, basi Zanzibar tunahitaji uongozi mwengine ambao utakuja kurekebisha na kujadili masuali mazito tuliyonayo.
Tusijidanganye ati Mh.Kikwete anajadili kero za muungano, kipindi cha mwanzo kimekwisha na hana alilofanya badala ya kumtuma Mh.Pinda kututonesha vidonda vyetu.Anakimbia hoja za msingi,kwa kuunda kamati nje ya bunge.Hapa anatengeneza kero nyengine na kukiuka taratibu za utawala bora.Bunge ndio linatuwakilisha sisi wananchi na sio vijikamati,hivi kweli hivi vikamati vinaweza kutetea maslahi yetu wazanzibari? Kheri ndugu yangu ukaamka kutoka katika usingizi mzito wa CUF-CCM na ukasimama kidete kutetea maslahi ya Zanzibar.Kumbuka kuwa sisi tutaondoka duniani, na vizazi vyetu vitakuja kuturithi kile tulichowaachia.Uko tayari kuwaona wanao wakitanga njia bila ya kuwa na kwao? Soma Zaidi ...

MESSI MCHEZAJI BOWA WA DUNIA
Baada ya kunyakua tunzo ya mchezaji bora barani Ulaya, Messi ametajwa tena kuwa ndio mchezaji bora wa Dunia wa mwaka 2010 kutoka katika Shirikisho la soka Duniani FIFA.
Soma Zaidi ...
Messi kwa msimu huu ameiwezesha timu yake ya Barcalona kuchukua vikombe vinne vikiwa ni pamoja na Champions league, kombe la dunia kwa vilabu, kombe la La liga pamoja na Copa del Rey.
Mchezaji huyo ambae inasadikiwa kuwa alijiunga na Barcalona akiwa na umri wa miaka 13 mwaka 2000, anakua mchezaji wa mwanzo kutoka Argentina kuchukua tunzo hio,katika kura zote zilizopigwa Mesi alipata alama (1,073) akifuatiwa na aliehukua tunzo hio mwaka jana Christiano Ronaldo kwa kupata alama (352), akifuatiwa na kiungo wa Barcalona Xavi kwa alama (196).
Katika mashindano ya Champions league 2008-2009 Mesi alimaliza mashindano hayo kwa kuibuka mfungaji bora akiwa amefunga magoli 9 likiwemo goli moja kati ya mawili walioshinda katika fainali dhidi ya Manchester United.
Mesi kabla ya sherehe hio alielezea kuhusu kutucheza kwa kiwango chake cha kawaida katika mechi za kufuzu kombe la Dunia alisema "sijui kwani najaribu kucheza kama ninavyocheza nikiwa na Barcalona lakini mechi za kufuzu kombe la Dunia ni ngumu, hata hivyo tumefanya juhudi kubwa kufuzu, lakini naamini kombe la Dunia itakua ni tofauti, itakua ni nzuri kwangu mimi na kwa Argentina pia
Kwa upande wa wanawake Marta ndio mwanasoka bora wa Dunia kutoka Shirikisho la soka Duniani FIFA, Marta ni mchezaji kutoka nchini Bazil
Monday, December 21, 2009
GHASIA ZAIBUKA MAZISHI YA AYATOLLAH
Polisi nchini Iran wanapambana na waandamanaji baada ya mazishi ya kiongozi mmoja wa kidini Ayatollah Hoseyn Ali Montazeri ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya nchi hiyo.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Iran mwezi Juni, Ayatollah Montazeri aliutaja kuwa wizi kuchaguliwa tena kwa Rais Mahmoud Ahmadinejad.
Maelfu ya waombolezaji walifanya maandamano wakati wa mazishi hayo kwenye mji mtakatifu wa Qom.
Ayatollah Montazeri alifariki dunia akiwa na miaka 87.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye mtandao wa Jaras, waombolezaji hao walikuwa wakiimba sifa za Ayatollah Montazeri na pia kiongozi wa upinzani Hossein Mousavi.
Bwana Mousavi na mwenzake wa upinzani Mehdi Karroubi walishiriki katika maandamano hayo. Soma Zaidi ...

Sunday, December 20, 2009
ELECTRIC FENCE
Seems a sheep farmer was puzzled about the disappearance
of some sheep on his farm. After a few weeks the farmer
decided to put up an electric fence.
About a week later, this is what he found!

Now, I know we've all heard of people being eaten by
snakes & I bet most of us have said, 'If a snake tried to
eat me, I'd blah, blah, blah & get away..'
Well, this is a Python & they're extremely aggressive &
have a few teeth that they use to hold their prey while
they wrap around them & then constrict.
Could you get away if this one bit you & held on with it's
'few teeth?'
Soma Zaidi ...
KARUME AWATUNUKU VYETI WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA FEDHA CHWAKA
Bimaka Abdallah Mohammed akipokea shahada ya kwanza kutoka kwa Rais Amani Karume katika mahafali ya sita ya chuo cha uongozi wa fedha Chwaka
Philemon Pius Mechel akipokea shahada ya kwanza kutoka kwa Rais wa Amani Karume katika mahafali ya sita ya chuo cha uongozi wa fedha Chwaka
Soma Zaidi ...
MAPINDUZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII DAIMAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Zikiwa zimebakia siku chache tu ili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar isherehekee mapinduzi yake wakaazi wa Zanzibar bado wanaendelea kuhangaika kwa kuyasaka maji kufuatia tatizo la ukosefu wa umume visiwani humo.
Soma Zaidi ...
RWANDA MSHINDI MISS EAST AFRICA 2009
Mrembo kutoka Rwaanda Cynthia Akazuba usiku wa kuamkia leo amenyakua taji la miss East Africa wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na mrembo Dalysha Doorga kutoka Mauritius na mwanadada Victoria Martin wa Tanzania alichukua nafasi ya tatu,mashindano hayo yalifanyika katika ukumb wa Mlimani City jijini Dar-es salaam
Soma Zaidi ...
Saturday, December 19, 2009
MATOKEO YA LEO LIGI KUU UINGEREZA
Arsenal 3 - 0 Hull City
Aston Villa 1 - 0 Stoke City
Blackburn Rovers 0 - 2 Tottenham Hotspur
Fulham 3 - 0 Manchester United
Manchester City 4 - 3 Sunderland
Portsmouth 2 - 0 Liverpool

Subscribe to:
Posts (Atom)