Tuesday, December 22, 2009

MESSI MCHEZAJI BOWA WA DUNIA


Baada ya kunyakua tunzo ya mchezaji bora barani Ulaya, Messi ametajwa tena kuwa ndio mchezaji bora wa Dunia wa mwaka 2010 kutoka katika Shirikisho la soka Duniani FIFA.

Messi kwa msimu huu ameiwezesha timu yake ya Barcalona kuchukua vikombe vinne vikiwa ni pamoja na Champions league, kombe la dunia kwa vilabu, kombe la La liga pamoja na Copa del Rey.

Mchezaji huyo ambae inasadikiwa kuwa alijiunga na Barcalona akiwa na umri wa miaka 13 mwaka 2000, anakua mchezaji wa mwanzo kutoka Argentina kuchukua tunzo hio,katika kura zote zilizopigwa Mesi alipata alama (1,073) akifuatiwa na aliehukua tunzo hio mwaka jana Christiano Ronaldo kwa kupata alama (352), akifuatiwa na kiungo wa Barcalona Xavi kwa alama (196).

Katika mashindano ya Champions league 2008-2009 Mesi alimaliza mashindano hayo kwa kuibuka mfungaji bora akiwa amefunga magoli 9 likiwemo goli moja kati ya mawili walioshinda katika fainali dhidi ya Manchester United.

Mesi kabla ya sherehe hio alielezea kuhusu kutucheza kwa kiwango chake cha kawaida katika mechi za kufuzu kombe la Dunia alisema "sijui kwani najaribu kucheza kama ninavyocheza nikiwa na Barcalona lakini mechi za kufuzu kombe la Dunia ni ngumu, hata hivyo tumefanya juhudi kubwa kufuzu, lakini naamini kombe la Dunia itakua ni tofauti, itakua ni nzuri kwangu mimi na kwa Argentina pia

Kwa upande wa wanawake Marta ndio mwanasoka bora wa Dunia kutoka Shirikisho la soka Duniani FIFA, Marta ni mchezaji kutoka nchini Bazil

No comments:

Post a Comment