Wednesday, December 23, 2009

ZANZIBAR KUENDE KUKAA GIZAI KWA MUDA WA MWEZI KUANZIA SASA

Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid, amesema Zanzibar itaendelea kukosa huduma ya umeme kwa muda wa mwezi mmoja baada kifaa kinachounganisha waya zinazopokea umeme kutoka Gridi ya Taifa, Tanzania Bara, kulipuka katika kituo cha Fumba, Zanzibar.

Kifaa hicho aina ya Spliter, hutumika kugawa nyaya zinazopokea umeme kutoka Gridi ya Taifa ambacho kililipuka muda mfupi juzi jioni baada ya mafundi kukamilisha matengenezo kufuatia njia moja inayopokea umeme katika kituo hicho kulipuka Desemba 10, mwaka huu.
Waziri Mansour, alisema kifaa hicho kitachelewa kutengenezwa kwa vile viwanda vinavyotengeneza wahusika wapo likizo ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Alisema kifaa hicho kinapatikana nje ya nchi na hivyo akawataka wananchi wa Zanzibar kuwa wastahimilivu.

No comments:

Post a Comment