Friday, December 25, 2009

HATIMAE TANI 296 ZA SAMAKI KUAZA KUGAIWA

Baada ya takriban miezi isiyopungua 10 hatimae samaki wapatao tani 296 waliokamatwa tarehe 8 machi mwaka huu wameanza kusambazwa tayari kwa mgao.

Samaki hao walikamatwa kutoka katika meli ya MV Tawariq 1 ambayo ilikua ikifanya uvuvi haram umbali wa maili 180 kutoka Dar-es-salaam eneo ambalo limetajwa kua ni Exclusive economic zone.

Inasmekana kisheria kesi inayohusiana na ukamatwaji wa meli hii ilikua iendeshwe Zanzibar na ikishindikana basi Germany kutokanana hili eneo walilokamatiwa lakini kesi hii imeendeshwa Tanganyika na hivo kufikia uamuzi kuwa samaki wanapaswa kugaiwa Nchi nzima.


Waziri wa anaeshughulika na masuala ya uvuvi na mifugo ambae ndie mwenye mamlaka ya Mgao huo bwana John Magufuli amesema serikali imegharamika Sh, bilioni 1.2 katika kuhifadhi samaki hao katika kampuni ya Bahari food limited na hadi sasa wamehalipa nusu ya fedha hizo na zilizobaki zitalipwa baada ya kumaizika kwa zoezi la ugawaji samaki hao.

Waziri Magufuli amesema pia katika mgao huo Zanzibar itafaidika na tani 80.

No comments:

Post a Comment