Monday, December 21, 2009

GHASIA ZAIBUKA MAZISHI YA AYATOLLAH

Polisi nchini Iran wanapambana na waandamanaji baada ya mazishi ya kiongozi mmoja wa kidini Ayatollah Hoseyn Ali Montazeri ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya nchi hiyo.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Iran mwezi Juni, Ayatollah Montazeri aliutaja kuwa wizi kuchaguliwa tena kwa Rais Mahmoud Ahmadinejad.

Maelfu ya waombolezaji walifanya maandamano wakati wa mazishi hayo kwenye mji mtakatifu wa Qom.

Ayatollah Montazeri alifariki dunia akiwa na miaka 87.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye mtandao wa Jaras, waombolezaji hao walikuwa wakiimba sifa za Ayatollah Montazeri na pia kiongozi wa upinzani Hossein Mousavi.

Bwana Mousavi na mwenzake wa upinzani Mehdi Karroubi walishiriki katika maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment