Tuesday, December 29, 2009

MWANAMKE ABAKWA NA WANAUME SITA

Mwanamke mmoja jina limehifadhiwa amelazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar baada ya kubakwa na wanaume wapatao sita na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri za mbele na nyuma.
Mwanamke huyo alifanyiwa unyama huo wa kusikitisha siku ya sherehe za sikukuu ya Krismas katika eneo la ufukwe wa bahari, maeneo ya Maisara mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka Makao Makuu ya Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani humo, zimesema kuwa mwanamke huyo ni mkazi wa Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar na aliokotwa na wavuvi wa eneo hilo akiwa amepoteza fahamu.

Taarifa hizo zimeelezwa kwamba msichana huyo alichukuliwa katika ukumbi wa disko wa hoteli ya Bwawani na wavulana hao, akiwa amelewa na kumpeleka katika eneo hilo la ufukweni na kuanza kumbaka kwa zamu.

Hadi kufikia jana jioni, ilidaiwa kuwa hali ya msichana huyo ilikuwa bado ni mbaya kutokana na athari kubwa alizozipata hasa katika sehemu zake za siri.

Daktari aliyempokea msichana huyo alisema, “aliletwa hapo akiwa hajitambui kabisa na sehemu zake za siri hasa sehemu ya haja kubwa zilikuwa zimeathiriwa vibaya”, alisema daktari wa zamu katika hospitali hiyo.

2 comments:

  1. Daktari amezidi kuoneshea kama athari zimetokezea kwenye haja kubwa.Anakusudia huo ni ushahidi unaotuonesha wanaume kutoka sehemu gani ya muungano wenye tabia ya kutumia haja kubwa?

    ReplyDelete
  2. Hahahahahahahaaaaaaaaa! sasa hapa kwani unaweza kujua aliebaka na kubakwa wanatoka sehemu gani ya muungano?

    ReplyDelete