Wednesday, January 20, 2010

MAMBO YA BELGIUM

Kutokana na wakaazi wa Belgium kuzungumza lugha zaidi ya lugha moja kama vile Nederlands na kifaransa basi katika baadhi ya miji hasa Brussels matangazo hulazimika kutolewa kwa lugha mbili, Nederlands ( kidachi) na kifaransa, nilibahatika kuchukua picha moja ya matangazo niliyokutana nayo pale kwenye ofisi za euro line Brussels
Tangazo kwa lugha ya kifaransa

Tangazo kwa lugha ya Nederlands a.k.a kidachi

Hawa jamaa niliwakuta jana wakiwa wamelala katika sehemu ya kusubiria mabasi ya euro line pale Brussels nilipokua nikisubiri basi la kurudi home kwa kweli jamaa hawa walikua tabaani na huyu wa chini aliye laliwa alikua kila akitaka kuinuka basi hawezi kwa jinsi pombe ilivyokua imemzidi na sijui walikua wakielekea wapi kwa sababu kila basi ninalotangaziwa kuondoka wao hata habari hawana
Soma Zaidi ...

MAMBO YA MJENGO MREFU KULIKO YOTE DUNIANI

Soma Zaidi ...

Monday, January 18, 2010

NYUZI MPYA ZA MWAKA 2010

Italy/ Brasil
Argentina
Netherland/Irland
Soma Zaidi ...

MATOKEO YA MECHI ZA JANA


Premier League:
Bolton Wanderers 0 - 2 Arsenal
Blackburn Rovers 2 - 0 Fulham
Aston Villa 0 - 0 West Ham United

African Cup of Nations:
Cameroon 3 - 2 Zambia
Gabon 0 - 0 Tunisia

La Liga :
Valencia CF 4 - 1 Villarreal CF
Atlético Madrid 3 - 2 Sporting Gijón
Real Zaragoza 0 - 0 Xerez CD
RCD Mallorca 2 - 0 Deportivo La Coruña
Málaga CF 1 - 0 Getafe CF
Racing Santander 1 - 1 Real Valladolid
UD Almería 1 - 1 CD Tenerife

Serie A:
Napoli 0 - 0 Palermo
Chievo 1 - 0 Juventus
Fiorentina 1 - 2 Bologna
Atalanta 3 - 0 Lazio
Parma 0 - 0 Udinese
AS Roma 3 - 0 Genoa
Sampdoria 1 - 1 Catania
AC Milan 4 - 0 Siena

Bundesliga:
FC Köln 2 - 3 Borussia Dortmund
Schalke 04 1 - 0 1. FC Nürnberg
Football Ligue 1 Match
Girondins Bordeaux 1 - 1 Olympique Marseille

Dutch Eredivisie:
NAC Breda 1 - 1 Ajax
FC Utrecht 0 - 0 FC Twente
NEC 2 - 1 Vitesse

Portuguese SuperLiga:
CS Marítimo 0 - 5 Benfica
Académica Coimbra 0 - 2 Sporting Braga
Rio Ave FC 0 - 2 União Leiria
Belenenses 1 - 3 Leixões SC
Soma Zaidi ...

Sunday, January 17, 2010

MENGINE NI KUJITAKIA

Jamaa huyu mwenye baskeli ya maringi matatu ikiwa imebeba mizigo na kupita katika njia ya treni je ataweza kutoka kwa ghafla mara tu treni litakapopita?na hapa inaonekana njia ipo ya kupita hata gari lakini kaiwacha. Soma Zaidi ...

MNAZI HUU UKO WAPI?

Soma Zaidi ...

BEI YA VYAKULA NDANI ZANZIBAR







Soma Zaidi ...

Friday, January 15, 2010

NAWAOMBA RADHI!!!!

NAOMBA RADHI KWA WOTE AMBAO MNAFUATILIA BLOG HII KUTOKANA NA KUSHINDWA KUKULETEENI HABARI, HII NI KUTOKANA KUA KWA KIPINDI HICHI NIKO KATIKA MATEMBEZI HUKU BELGIUM HIVYO NIMEKOSA COMPUTER YA KUFANYIA KAZI KWA KIPINDI HICHI CHOTE, LAKINI NATARAJIA KUREJEA NYUMBANI MWANZONI MWA WIKI IJAYO INSHAALLAH, HIVYO MAMBO YOTE YATAREJEA KAMA KAWAIDA.

OMMYKISS/ Soma Zaidi ...

Thursday, January 7, 2010

WANAUME WALIOOWANA MALAWI WATUPWA JELA

Mashoga wa nchini Malawi ambao walifunga ndoa hivi karibuni nchini humo walinyimwa dhamana na kurudishwa jela wakisubiria hukumu ya kesi yao ya kufanya kitendo nje ya maadili ya jamii.

Steven Monjeza akiwa na mkewe Tiwonge Chimbalanga ambaye alikuwa amevaa nguo za kike gauni na kitenge alipofikishwa mahakamani walizomewa na kupigiwa kelele na mamia ya watu waliojiotokeza mahakamani wakati walipopigwa pingu na kupandishwa kwenye karandinga kurudishwa jela baada ya jaji kukataa kuwapa dhamana.

Monjeza na Tiwonge wataendelea kuwa jela mpaka wiki ijayo wakati kesi yao itakapoanza kusikilizwa na huenda wakatupwa jela miaka 14 iwapo watapatikana na hatia.

Akiwanyima dhamana jaji Nyakwawa Usiwa-Usiwa alisema kuwa ni bora wakaendelea kukaa mahabusu ambako ni salama kuliko kukaa uraiani ambako kuna watu wengi wenye hasira kufuatia uamuzi wao wa kuoana.

"Anti Tiwonge, Anti Tiwonge", walipiga kelele mamia ya watu waliojitokeza mahakamani kushuhudia ndoa ya kwanza ya mwanaume kwa mwanaume nchini Malawi.

"Oh tunarudishwa tena kwenye jela ya Chichiri, hali ni ngumu sana kwenye jela ile", alilalama Monjeza ambaye alidai anafikiria kumtosa mkewe kufuatia hasira kali za wananchi.

Wakati huo huo wanaharakati wa kutetea haki za mashoga duniani wameijia juu serikali ya Malawi kufuatia taarifa kuwa Monjeza na Tiwonge walikaguliwa sehemu zao za siri na maafisa wa Malawi ili kujua kama wameishafanya mapenzi kinyume na maumbile.

Awali mwendesha mashtaka wa serikali alisema kuwa Monjeza na Tiwonge wamekuwa wakiishi pamoja kama mume na mke tangia mwezi agosti mwaka jana hivyo alitaka wapelekwe hospitali kupimwa kama wameishajamiiana kinyume na maumbile.

Monjeza mwenye umri wa miaka 26 na Tiwonge mwenye umri wa miaka 20 wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kufanya vitendo ambavyo si vya asili kwa wanaume na kwa mujibu wa sheria za Malawi adhabu yake ni miaka 14 jela. Soma Zaidi ...

Wednesday, January 6, 2010

MABAIBUI ASILIA YA KIZANZIBARI


Soma Zaidi ...

HAPO VIPI?


Mara nyingi mtu akifanya jambo lake huangalia faida tu atakayoipata bila ya kuangalia na hasara itakayoweza kutokezea, hivi kuna usalama uliozingatiwa katika kufanya biashara katika eneo hili au watu wanajali pesa tu?.
Soma Zaidi ...

OBAMA - UAMUZI WA KUIFUNGA GUANTANAMO BAY UKO PALE PALE

Rais Obama amekiri kwamba maafisa wa idara ya ujasusi wa Marekani walikusanya taarifa za kutosha kumzuia raia wa Nigeria dhidi ya kuabiri ndege aliyojaribu kulipua siku ya krisimasi.
Hata hivyo maafisa hao walipuuza taarifa hizo.

Akiongea baada ya kukutana na washauri wake wa usalama Rais Obama amesema taarifa za kijasusi sharti zitiliwe maanani.

Rais huyo ameongeza kulikuwa na taarifa kuhakikisha Umar Farouk Abdul mutallab, hakubaliwi kusafiria ndege hiyo.

Obama hata hivyo ameihakikishia dunia kwaba jaribio hilo halitabadilisha mpango wa utawala wake wa kufunga kizuizi cha Guantanamo Bay. Soma Zaidi ...

MV MAPINDUZI


Soma Zaidi ...

Tuesday, January 5, 2010

UZEMBE HUU HADI LINI?

Daladala hii inageuza (u-turn) sehemu ambayo haistahiki kufanya hivyo kitendo ambacho kinaweza kusababisha maafa Soma Zaidi ...

UNAIKUBUKA SKULI HII?


Soma Zaidi ...

KAHAWA ORIJINO

Soma Zaidi ...

Monday, January 4, 2010

JENGO REFU KULIKO YOTE DUNIANI LAFUNGULIWA DUBAI

Jengo lenye urefu wa mita 800 limefunguliwa Dubai na kuwa ndio jengo refu kuliko yote duniani baada ya kuvunja rekodi ya lile la mwanzo lililopo Taiwan, Taipei 101 ambalo lina urefu wa mita 508.

Kwa heshima ya mfalme wa Abudhabi ambae ndie rais wa U.A.E Skeikh Halifa bin Zayed al -Nahyan, jengo hilo limepewa jina lake kwa kuitwa "Burj Khalifa" ( Khalifa Tower).Sherehe hizo ziliongozwa na mfalme wa Dubai Skeikh Mohammad bin Rashed al-Maktoum.
Soma Zaidi ...

MAPAMBO ASILIA YA KIZANZIBARI

Haya ni baadhi ya mapambo yetu asilia ya kizanzibari na wala sio vinyago vya mpingo
Soma Zaidi ...

MAMBO MSETO


Soma Zaidi ...

WATOTO WAKIHANGAIKA KUTAFUTA MAJI KATIKA KIJIJI CHA KIZIMKAZI


Soma Zaidi ...

JACOB ZUMA KUONGEZA MKE WA TANO

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anafanya ndoa yake ya tano baadaye leo.
Harusi ya leo itafanyika kuambatana na mila na utamaduni wa jamii ya Zulu ambapo Thobeka Stacey Mabhija atakuwa mke wa tatu wa Zuma.

Wake wengine wawili wa Zuma Sizakele Khumalo-Zuma na Nompumelelo Ntuli-Zuma sharti washiriki sherehe ya leo ili kumkubali mke mwenza wao.

Rais Zuma pia amesha mposa mwanamke mwingine na tayari amelipa mahari.

Waandishi habari wamesema imani ya Zuma kuwa na wake wengi imeigawanya jamii Afrika Kusini.

Baadhi wanamuunga mkono huku vijana wengi wakisema desturi hiyo imepitwa na wakati.

Mmoja wa wake wa Zuma Kate Mantsho-Zuma alifariki dunia na rais huyo alitengana na waziri wa mambo ya ndani wa Nkosazana Dlamini Zuma. Soma Zaidi ...

TANGAZO


Soma Zaidi ...

MAMBO YA MKUKI MOYONI A.K.A NGWASUMA


Soma Zaidi ...

Sunday, January 3, 2010

MATOKEO YA MECHI ZA KUWANIA KOMBE LA FA


Tranmere Rovers 0 - 1 Wolverhampton Wanderers
West Ham United 1 - 2 Arsenal
Sheffield United 1 - 1 Queens Park Rangers
Chelsea 5 - 0 Watford
Manchester United 0 - 1 Leeds United
Soma Zaidi ...

MAPACHA WALIOUNGANA WAFARIKI DUNIA

Watoto mapacha walioungana waliozaliwa na bibi Farhat Maulid siku ya mkesha wa mwaka mpya katika hospitali ya Mnazi mmoja wamefariki dunia jana Januai 2, 2010 asubuhi katika hospitali ya taifa ya Mnazi mmoja.

Watoto hao ambao wameishi kwa siku moja tangu kuzaliwa kwao na kuhifadhiwa katika chombo maalum cha kusaidia joto (INCUBATOR) pamoja na kusaidiwa kupumua hali yao ilikua inaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa daktari amesema watoto hao wamefariki dunia saa12 asubuhi jana 2/1/2010, baada ya kuishi kwa takriban masaa 11 tangu kuzaliwa kwao na mauti yamewakuta kabla ya kutenganishwa kwa miili yao.

Mama mzazi wa marehemu hao bibi Farhat Maulid mwenye umri wa miaka (18)ambae ni mkaazi wa Mwanyanya wilaya ya Magharibi hali yake inaendelea vizuri katika hospitali ya Mnaei mmoja.

Watoto hao walikua wameungana sehemu ya kifuani na tumboni wakiwa na uzito wa kilo 3, ambao walizaliwa kwa njia ya operesheni lilikua ni tukio la kwanza kutokea katika visiwa vya Zanzibar.

Watoto hao walikua wakitumia baadhi ya viungo kama kitovu na moyo mmoja, lakini viungo vilivyobakia kila mmoja alikua akitumia chake.

Tunamuomba Allah ampe subira na afya njema mama wa marehemu hao bibi Farhat Mauli.

Amiin.
Soma Zaidi ...

MWANAZUONI KUTOKA JAMAICA AKAMATWA NCHINI KENYA

Mwanazuoni wa kiislam kutoka Jamaica ambaye aliwahi kufukuzwa kutoka Uingereza kwa makosa ya kuchochea uhasama kwa misingi ya rangi anafanyiwa uchunguzi na polisi nchini Kenya, baada ya kukamatwa na kikosi maalum cha kupambana na ugaidi akiwa katika mji wenye bandari wa Mombasa.

Mwanazuoni huyo Sheikh Abdullah al-Faisal, alishikwa katika mkesha wa mwaka mpya kwa madai ya kukiuka kanuni za uhamiaji kwa kuhubiri katika misikiti.

Kundi la kiislam la kutetea haki za binadamu nchini Kenya lilisema kuwa liliarifiwa na serikali kuwa mwanazuoni huyo atafukuzwa nchini.

Mkuu wa kundi hilo, al-Amin Kimathi, alisema mwanazuoni huyo alialikwa na makundi ya kiislam katika miji ya Mombasa na Nairobi.

Amesema kitendho cha kumkamata kilichochewa na ubaguzi, ambapo imekuwa mazoea wanazuoni wa kiislam kutiwa kizuizini na hata kufukuzwa nchini bila sababu zinazoeleweka. Soma Zaidi ...

WAPI HAPA?


Soma Zaidi ...

?????????????????????


Soma Zaidi ...

NYUMBA YA MAKAMO WA RAIS HUKO TUNGUU

Soma Zaidi ...

KAZI NI KAZI TU

Masoud chile akiwa kazini Soma Zaidi ...

Saturday, January 2, 2010

WATOTO WALIOUNGANA ZANZIBAR

Huyu ndie daktari aliyemfanyia upasuaji mama wa watoto hawa katika hospitali ya Mnazi mmoja. Soma Zaidi ...

MECHI ZA KUWANIA KOMBE LA FA KUTIMUA VUMBI LEO HII

16:00 Millwall v Derby County
16:00 Tottenham Hotspur v Peterborough United
16:00 Brentford v Doncaster Rovers
16:00 Middlesbrough v Manchester City
16:00 Stoke City v York City
16:00 Huddersfield Town v West Bromwich Albion
16:00 Milton Keynes Dons FC v Burnley
16:00 Nottingham Forest v Birmingham City
16:00 Preston North End v Colchester United
16:00 Aston Villa v Blackburn Rovers
16:00 Portsmouth v Coventry City
16:00 Sunderland v Barrow
16:00 Wigan Athletic v Hull City
16:00 Everton v Carlisle United
16:00 Sheffield Wednesday v Crystal Palace
16:00 Blackpool v Ipswich Town
16:00 Fulham v Swindon Town
16:00 Torquay United v Brighton & Hove Albion
16:00 Scunthorpe United v Barnsley
16:00 Southampton v Luton Town
16:00 Plymouth Argyle v Newcastle United
16:00 Leicester City v Swansea City
16:00 Bolton Wanderers v Lincoln City
18:15 Reading v Liverpool

NB: hii ni kwa ( CET ) Soma Zaidi ...

KIDINI INARUHUSIWA?


Soma Zaidi ...

UNANIFANYA MUME BWEGE SIO?

Soma Zaidi ...

UGOMVI WA NDUGU

Hivi karibuni tulishuhudia mkasa wa mzungu mmoja "mjeuri na fedhuli" ambae alikumbana na kijana wa kiunguja ambae alimuweka sawa jeuri zote zikamwishia.


Mkasa wenyewe ulianzia hivi:

Mzungu alikua na Kima (Tumbili) wake akitembea nae. Hapo palikua na kijana anauza matunda, zikiwemo ndizi. Yule mzungu hakumdhibiti yule kima wake na kima akarukia zile ndizi akachukua moja akala. Kijana akaomba alipwe na mzungu akalipa.

Lakini mchezo haukuishia hapo, ikawa kila mara yule kima hurukia na kuchukua ndizi nyengine, mara ya pili, ya tatu.... mwisho mzungu kwa jeuri yake tu akakataa kulipa tena, na alipoulizwa kwa nini hataki kulipa akajibu "KWANI SI KACHUKUA CHA NDUGU YAKE TU" (akimaanisha yule kijana na huyo kima ni jamii moja).


Yule kijana kusikia kwamba kajibiwa kauli hiyo kwanza alishangaa, lakini hakugombana. Alivuta akili na baada ya muda yule kima akaparamia tena meza ya yule kijana ili kuchukua ndizi nyengine. Kijana hakufanya ajizi... alimpiga kima kipanga kimoja tu, akamjeruhi vibaya sana.


Mzungu kuona hivyo alibadilika rangi akawa mweusi kwa hasira, na alipolalamika kijana akasema mwambieni mzungu - "UGOMVI WA NDUGU ASIUINGILIE"
Soma Zaidi ...

MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO WAKIWA WAMEUNGANA ZANZIBAR

Mwanamke mmoja mjini Zanzibar Farihati Maulid (18) amejifungua watoto mapacha walioungana Usiku wa Mwaka mpya.

Mwanamke huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Mnazi Mmoja leo saa tatu Asubuhi na mapacha hao wako katika chumba cha uangalizi maalum wakisaidiwa kupumua kwa mashine. Mkunga wa Hospitali hiyo, Halima Habib Abdallah, na Dk. Mwana Omar, mkuu wa Kitengo cha uzazi wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema tukio hilo ni la kwanza na wanaendelea kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wengine wa Afya.

Mapacha wote ambao ni wa kiume wenye moyo mmoja, wameunganika kuanzia kwenye kitovu hadi kwenye mfupa wa Kidari wana uzito wa kilo 2.8 na kutokana na kutumia moyo mmoja inaonekana itakuwa vigumu kuwatenganisha.

Habari zaidi zinasema mama wa watoto hao ni mkazi wa Mwanyanya, Bububu katika Manispaa ya Zanzibar na uzazi huo ulikuwa wa kwanza. Soma Zaidi ...

Friday, January 1, 2010

KAHAWA YA ZANZIBAR

Mimi kuna maswali kila siku najiuliza kuhusu hii kahawa ya Zanzibar, kwa nini asilimia kubwa ya wanyaji wa kahawa Zanzibar ni watu wazima? pia ni kwa nini vi kwa nini hivi vikombe vya kahawa vikawa vidogo na havina mikono? Soma Zaidi ...

???????????


Soma Zaidi ...

CCM OYEEEEEEEEEE


Soma Zaidi ...

ABDULMUTALLAB ALIANZA SAFARI YAKE GHANA NA WALA SI NIGERIA

Serikali ya Nigeria imesema raia wa nchi hiyo aliyejaribu kulipua ndege ya Marekani mnamo tarehe 25 mwezi desemba, alikuwa ameanzia safari yake nchini Ghana na si Nigeria kama inavyodhaniwa.

Waziri wa habari Dora Akunyili ameiambia BBC kuwa mtu huyo Umar Farouk Abdulmutallab alikuwa amesafiri kutoka Accra Ghana na kuwasili nchini Nigeria ambapo alikaa kwa muda wa nusu pekee kabla ya kupanda tena ndege kuelekea Amsterdam.

Maafisa wa Nigeria na Udachi wamesisitiza raia huyo alipitia ukaguzi wote wa usalama kwenye viwanja vya ndege. Soma Zaidi ...