Wednesday, January 6, 2010

OBAMA - UAMUZI WA KUIFUNGA GUANTANAMO BAY UKO PALE PALE

Rais Obama amekiri kwamba maafisa wa idara ya ujasusi wa Marekani walikusanya taarifa za kutosha kumzuia raia wa Nigeria dhidi ya kuabiri ndege aliyojaribu kulipua siku ya krisimasi.
Hata hivyo maafisa hao walipuuza taarifa hizo.

Akiongea baada ya kukutana na washauri wake wa usalama Rais Obama amesema taarifa za kijasusi sharti zitiliwe maanani.

Rais huyo ameongeza kulikuwa na taarifa kuhakikisha Umar Farouk Abdul mutallab, hakubaliwi kusafiria ndege hiyo.

Obama hata hivyo ameihakikishia dunia kwaba jaribio hilo halitabadilisha mpango wa utawala wake wa kufunga kizuizi cha Guantanamo Bay.

No comments:

Post a Comment