Thursday, July 1, 2010

WULFF NDIE RAIS MPYA WA IJERUMANI


Mgombea wa muungano wa serikali inayongozwa na Kansela Angela Merkel, Christian Wulff jana usiku amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shrikisho la UjerumUchaguzi huo ulilazimika kurudiwa mara tatu, kabla ya Bwana Wulff kupata idadi ya kura za bunge la shirikisho zinazomruhusu kuchaguliwa kuwa rais.

Christian Wulff hatimaye alifanikiwa kupata idadi hiyo ya kura dhidi ya mgombea wa mrengo wa kati kushoto anayeungwa mkono na upinzani Joachim Gauck, na Spika wa bunge, Nobert Lammert kumtangaza kuwa rais mpya wa Ujerumani.

Kurejewa mara tatu kwa uchaguzi huo, kunaonekana kama ni pigo kwa Kansela Merkel ambaye kura za maoni za hivi karibuni zimeonesha kupungua kwake umaarufu na kuzua wasi wasi kuwa ameshindwa kuidhibiti serikali ya muungano na chama cha FDP kinachowapendelea wafanyabiashara.

Christian Wulff anachukua nafasi hiyo ya urais wa Ujerumani ambayo ni ya heshima kutoka kwa Horst Koehler ambaye kujiuzulu kwake ghafla mwezi mmoja uliyopita lilikuwa ni pigo lingine kwa Kansela Merkel na serikali yake.
ani.

.

No comments:

Post a Comment